Pre GE2025 Kagera: CV za Wabunge mwaka 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Pre GE2025 Kagera: CV za Wabunge mwaka 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu,

1. Ezra John Chewelsea – Mbunge wa Biharamulo Magharibi

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Kura katika Uchaguzi wa 2020: 40,526 (alishinda dhidi ya Mbelwa Petro Zimbia wa CHADEMA)

Elimu

Shule ya Msingi Umoja (1995)
Shule ya Ufundi ya Bwiru Boys, Mwanza (CSEE, 1999)
Shule ya Sekondari ya Moshi (ACSEE, 2002)
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (2003-2007) – Bachelor of Science in Production and Mechanical Engineering

Kazi za Nje ya Siasa

Cabin Crew katika Air Tanzania (2003)
Mechanical Engineer, Tanzania Steel Pipes Ltd (2007)
Sales Engineer, General Motors Investment Ltd (2008-2014)
Sales Manager, Pipe Industries Co. Ltd (2014-2020)

Michango Bungeni

Michango 43 na maswali 54.
Akiwa katika Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira (2021-2023)


2. Stephen Lwujahuka Byabato – Mbunge wa Bukoba Mjini

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Kura katika Uchaguzi wa 2020: 29,208 (alishinda dhidi ya Chief Adronicus Karumuna wa CHADEMA)

Elimu

Shule ya Msingi Rumuli (1992-1998)
Shule ya Sekondari ya Iluhya na Forest Hill (ASCEE)
Tumaini University - Iringa (2005-2008) – Bachelor Degree
Law School of Tanzania (2009-2010) – Postgraduate Diploma
Mzumbe University - Morogoro (2014-2016) – Master's Degree

Kazi za Nje ya Siasa:

Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Sekretarieti ya Mkoa wa Kagera (2011-2016)
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba (2018)

Michango Bungeni:

Michango 5 na maswali 118 ya msingi, pamoja na maswali ya ziada 322.

Kazi za Kisiasa

Alihudumu kama Naibu Waziri wa Nishati (2020-2023) na sasa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (2023-sasa)


3. Jason Samson Rweikiza – Mbunge wa Bukoba Vijijini

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Kura katika Uchaguzi wa 2020: 44,509 (alishinda dhidi ya Conchesta Leone Rwendeza wa CHADEMA)

Elimu

Shule ya Msingi Nyakabanga (1966-1972) na Nyarubale (1973) – CPEE
Shule ya Sekondari Milambo (1974-1977) – CSEE
Shule ya Sekondari Mzumbe (1978-1980) – ACSEE
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1986) – Shahada ya Sheria
Postgraduate Diploma in Business Administration, SSPA University, Italia (1990)
Diploma in Transport, Ubelgiji (1993-1994)

Uzoefu wa Kazi:

Mwalimu wa Sekondari, KCU Ltd (1981-1983)
Wakili wa Serikali, Wizara ya Sheria na Katiba (1986)
Naibu Katibu, Shirika la Uchukuzi (1987-1995)
Wakili huru (1993-2010)
Mkurugenzi Mtendaji, St. Anne Marie Ac. Ltd (2001-sasa)

Nafasi za Uongozi CCM:

Mwenyekiti wa Wilaya, Jumuiya ya Wazazi CCM (2007)
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (2008-2020)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (2016-2018)
Katibu wa Wabunge wa CCM (2016-2020)


4. Innocent Lugha Bashungwa – Mbunge wa Karagwe

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Kura katika Uchaguzi wa 2015: Chaguliwa kuwa Mbunge wa Karagwe

Elimu

Shule ya Msingi Ahakishaka (1987-1990) na Ubungo Kisiwani (1991-1993) – CPEE
Azania Secondary School (1994-1997) – CSEE
Lake Region State College (1998-2000) – Shahada ya Sanaa
St. John's University (2000-2002) – Bachelor ya Uchumi
Columbia University (2008-2010) – Master's Degree, Sera za Kiuchumi
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (2016-2023) – Master's Degree, Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo

Uzoefu wa Kazi:

Meneja wa Programu, Taasisi ya Uongozi na Usimamizi Barani Afrika (2002-2008)
Meneja wa Mahusiano na Wateja, Africa Biofuel and Emission Reduction Ltd (2005-2006)
Mshauri, Benki ya Dunia (2009-2010)
Mkurugenzi Mtendaji, AKTZ Industries Ltd (2010-2011)
Kiongozi wa Programu ya TEITI, Wizara ya Nishati na Madini (2012-2014)
Mkurugenzi Mtendaji, Extractive Industries Consultancies (2015-2018)

Nafasi za Uongozi:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (2015-2020)
Waziri wa Ulinzi (2020)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (2022)
Waziri wa Ujenzi (2023-sasa)

5. Innocent Sebba Bilakwate – Mbunge wa Bukoba Vijijini

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Alishinda kwa kupata kura 61,848, akimshinda Anatropia Lwahikila Theonest kutoka CHADEMA aliyetapata kura 45,893.

Elimu

CPEE kutoka Shule ya Msingi ya Kaisho (1991)
CSEE kutoka Shule ya Sekondari ya Kaisho (2005)
Cheti cha Teknolojia ya Habari kutoka Information Technology LTD (1996) na Modern Commercial Institute (1999).


Kazi Zilizowahi Kufanya nje ya Siasa:

Mwalimu wa Kompyuta katika Information Technologies LTD (1998)
Mhandisi na Mchoraji wa Picha katika GEMA International (2007)
Mkurugenzi wa Michoro katika I&J Graphic Designs LTD (2008-2015).


6. Oscar Ishengoma Kikoyo – Mbunge wa Muleba Kusini

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Alishinda kwa zaidi ya asilimia 65, akimchukua nafasi Profesa Anna Tibaijuka.

Elimu

Shahada ya Uzamili katika Biashara za Kimataifa kutoka The Indian Institute of Foreign Trade (2006).
Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1998-2001).
PhD kutoka The Open University of Tanzania (2008-2014).

Kazi Zilizowahi Kufanya

Mwanachama wa Kamati ya Uwekezaji wa Umma na Kamati ya Miongozo ya Kudumu katika Bunge la Tanzania.
Anaongeza juhudi za kuboresha mazingira ya elimu na sheria nchini.


7. Ndaisaba George Ruhoro – Mbunge wa Ngara

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Alishinda kwa kura 78,776, akimshinda Dedan Joachim Rajab kutoka CHADEMA ambaye alipata kura 7,913.

Elimu

Shule ya Msingi ya Nyarusange (1995-2000)
Shule ya Sekondari ya Kahororo (2002-2005)
Shule ya Sekondari ya Kwiro (2006-2008)
Shahada ya Sheria (Bachelor of Laws) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (2008-2012)
Shahada ya Uzamili (Masters) katika The Open University of Tanzania, akijishughulisha na masomo ya Project Management (2019 – sasa).

Kuingia Kwenye Siasa:

Mwanachama wa CCM na aliyehudumu kama mwanachama wa Kongamano la Mkoa na Wilaya (2017-2022).

Kazi Zilizowahi Kufanya:

Ofisa wa Rasilimali Watu na Usimamizi wa Jamii katika Tanzania Rural Empowerment and Poverty Alleviation Agency (2010-2011).
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa People Development Forum.


8. Flaurent Laurent Kyombo – Mbunge wa Nkenge

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Alishinda kwa kura 58,051, akimshinda Magreth Domitian Kyai kutoka CHADEMA ambaye alipata kura 4,803.

Elimu

Shule ya Msingi ya Kitobo (1982-1988)
Shule ya Sekondari ya Ihungo (1989-1992)
Shule ya Sekondari ya Pugu (1993-1995)
Shahada ya Pharmacy (B.PHARM) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1997-2001)
Shahada ya Uzamili (MBA) kutoka The Open University (2014)
Mafunzo ya ziada kutoka Interpol (Uganda), Manzin (Swaziland), na Dar es Salaam.

Kazi Zilizowahi Kufanya:

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero (2016-2020).
Meneja katika Kituo cha Kanda cha Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (2011-2016).
Mkaguzi wa Dawa katika Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (2007-2011).
Pharmacist wa Wilaya katika Halmashauri ya Kibaha (2006-2007).
 
Kuna hiyo ng'ombe ya kwanza kuitaja kwenye bandiko lako sijui hata imewahi kufanya nini pale Biharamulo, anyway kwa sasa sipo pale kwahiyo simfahamu kinacho endelea
 
Back
Top Bottom