JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limesema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Byamtemba, Kata ya Nsunga Wilayani Missenyi Mkoani Kagera, Jonathan Bunyaga alipata ajali na hajauawa na watu wasiojulikana kama inavyoelezwa.
Mwili wa Jonathan uliokotwa ukiwa umetelekezwa kando ya barabara inayotoka Bukoba kuelekea Mtukula mpakani mwa Tanzania na Uganda, Julai 30, 2022.
Familia ya Mwenyekiti huyo imeeleza kusikitishwa na kifo cha ndugu yao ambaye wanadai aliuawa na watu wasiojulikana na kisha mwili wake kutelekezwa kando kando mwa barabara.
Ndugu hao wanasdema ndugu yao alipigiwa simu saa tatu usiku na kuondoka akiwa na pikipipiki ambapo hakurudi nyumbani hadi walipopigiwa simu baada ya mwili wake kuonekana kandokando mwa barabara, na kwamba walipofika eneo la tukio walikuta marehemu amevaa kiatu kimoja huku kiatu kingine kikiokotwa sehemu nyingine kwenye shamba la miti ambako pia kulionekana kuwa na damu.
Aidha wanafamilia hao wamedai kuwa wakati wa kuosha mwili huo walibaini kuwepo kwa majeraha shingoni na sehemu nyingine za mwili yaliyoonesha kama amechomwa kwa kitu chenye ncha kali.
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Wilson Sakulo amekiri kuwepo kwa kifo hicho lakini akadai chanzo chake bado hakijafahamika na polisi wanaendelea na uchunguzi.
"Ni kweli kuna tukio la kifo cha Mwenyekiti wa Kijiji cha Byamtemba lakini chanzo cha kifo chake mimi kama Mkuu wa wilaya sifahamu, polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo" amesema mkuu wa wilaya.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema kuwa mwenyekiti huyo alipata ajali ya pikipiki. "Haijajulikana kama yeye ndiye aligonga au aligongwa, lakini mhusika mwingine katika ajali hiyo alikimbia baada ya tukio.
"Hiyo ndiyo taarifa rasmi ya Polisi, kama kuna watu wengine wanasema ameuawa hizo taarifa hatuna na si za kweli," anasema RPC Mwampaghale.
Source: EATV