Kutoka Kagera-Bunazi, Mji Mkuu wa Wilaya ya Missenyi nawaomba wenye Mamlaka kuweka Taa za Barabarani maana imekuwa kero kwa Wananchi eneo la Mnada (mjajaro) kuanzia njia panda kwenda Kagera Sugar mpaka Ofisi za Halmashauri.
Nyakati za usiku kiza kinene na Barabara hiyo ndio kuu ya watembea kwa miguu wakiwemo wanaotokea Mnadani, pia ni njia inayotumiwa na Bodaboda, Magari yaendayo Uganda etc.
Uwepo wa giza unaweza kuchangia uwepo wa wahalifu maeneo hayo, pia inaweza kuwachanganya wanaotembea na wanaotumia vyombo vya usafiri na kusababisha ajali.