Kagera Sugar Yamtimua Kocha Francis Baraza

Kagera Sugar Yamtimua Kocha Francis Baraza

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
FB_IMG_16670482636954020.jpg

π—§π—›π—”π—‘π—ž 𝗬𝗒𝗨 | 𝗙π—₯π—”π—‘π—–π—œπ—¦ 𝗕𝗔π—₯𝗔𝗭𝗔

Uongozi wa Kagera Sugar Football Club umefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Fransic Otieno Baraza.

Uongozi wa klabu unapenda kumshukuru Kocha Fransic kwa mchango wake mkubwa aliyouonesha ndani ya klabu kwa muda wote wa utumishi wake hadi leo tunafikia makubaliano haya ya kusitisha mkataba wake kwa maslahi mapana ya klabu yetu na pia uongozi unamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya.

Kuelekea mchezo wetu wa mzunguko wa 10 dhidi ya KMC ambao tunatarajia kucheza siku ya Jumanne Tar 01, Novemba jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba, kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha msaidizi Marwa Chacha.

WE WISH YOU ALL THE BEST COACH. πŸ™πŸ™πŸ™
#wanankurukumbi
 
Wale wanaojifanyaga wanajuwa kocha gani kafukuzwa mbona hawakuandika hii tangu Jana?
 
Uyu lilikuwa ni suala la muda tu,,, toka msimu umeanz timu haina matokeo mazuri
 
Ngoja tuone na wale wazee wa kuvunja rekodi ya kufukuza makocha wengi ndani ya msimu mmoja, watafanya nini!

Maana walishaanza mapema kabisa mwanzoni mwa msimu.
 
Kuna timu muda si mrefu itafukuza kocha wake chibonge
 
Back
Top Bottom