Kagera yaongoza kilimo cha kahawa Tanzania,aslimia 50 ya Kahawa yote inazalishwa kagera

Kagera yaongoza kilimo cha kahawa Tanzania,aslimia 50 ya Kahawa yote inazalishwa kagera

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Mkoa wa Kagera unatajwa kuwa kinara wa kilimo cha kahawa Nchini Tanzania ikizalisha aslimia 50 ya Kahawa yote inayolimwa Nchini humo.

Kagera pia inatajwa kama mkoa ambao kwa Sasa wakulima wake wanuza kahawa kwa mfumo wa kidijitali mfumo unaotaiwa kuwa Bora na usiokuwa na ujanjaujanja kutoka kwa makarani wa vyama vya msingi vya mazao (AMCOS)

Mwenyekit wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB),Profesa Aurelia Kamzola anasema mfumo huo wa Kidigitali umekuwa na mafanikio makubwa katika mkoa wa Kagera na umekuwa rafiki mkubwa wa wakulima

Profesa Kamzola alikuwa akitoa salamu za Bodi ya Kahawa wakati wa ufunguzi rasmi wa Tamasha kubwa la Saba la uhamasishaji wa unywaji wa kahawa (kahawa Festival )kwenye kiwanda Cha kukoboa kahawa Cha Tanganyika Coffee Curring mjini Moshi October 8 mwaka huu.
Profesa Kamzola akatoa wito kwa mikoa mingine kuingia kwenye mfumo huo wa kidijitali katika uuzaji wa kahawa .
Profesa Kamzola amepongeza ongezeko kubwa la washiriiki wa Tamasha hilo zikiwamo Taasisi za fedha hapa namaanisha mabenki

Hapa nakuletea taarifa fupi ya mikoa inayolima kahawa nchini Tanzania na aina ya Kahawa inayolima

Mikoa 17 Nchini Tanzania inalima kahawa kwa jumla, lakini imegawanyika kwa aina 2:

1. ARABICA - Inachangia 70% ya kahawa yote ya Tanzania
Inahitaji baridi na mwinuko mita 1,200 - 2,000. Ndio kahawa ya bei juu zaidi.

Mikoa 12 inayolima Arabica:

Kaskazini:

Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga

Nyanda za Juu Kusini:

Mbeya, Songwe, Ruvuma, Iringa, Njombe, Morogoro

Magharibi / Kati Magharibi:

Kigoma, Katavi, Rukwa (inajaribiwa)

Wazalishaji wakubwa ni

Mbeya, Songwe, Ruvuma na Kilimanjaro.

2. ROBUSTA - Inachangia 30% ya kahawa yote

Inahitaji joto na mwinuko chini ya mita 1,000. Ina caffeine nyingi.

Mikoa 3-5 inayolima Robusta:

Msingi mkuu:

Kagera😛eke yake inazalisha zaidi ya 50% ya Robusta yote ya Tanzania

-Ziwa: Geita, Mwanza, Kigoma

Kwa ufupi:

Arabica = Mikoa ya Milimani (12)

Robusta = Mikoa ya Ziwa Victoria (Kagera, Geita, Mwanza)

Kwa mujinbu ya Bodi ya Kahawa Nchini Tanzania(TCB) familia zaidi ya 450,000 nchini Tanzania zinategemea zao la kahawa
 

Attachments

  • FB_IMG_1791537322999.jpg
    FB_IMG_1791537322999.jpg
    61.5 KB · Views: 8
  • FB_IMG_1791537415159.jpg
    FB_IMG_1791537415159.jpg
    62.9 KB · Views: 9
  • FB_IMG_1791537394512.jpg
    FB_IMG_1791537394512.jpg
    53.5 KB · Views: 9
  • FB_IMG_1791537438365.jpg
    FB_IMG_1791537438365.jpg
    46.8 KB · Views: 8
  • FB_IMG_1791537491185.jpg
    FB_IMG_1791537491185.jpg
    67.4 KB · Views: 8
  • FB_IMG_1791537451298.jpg
    FB_IMG_1791537451298.jpg
    70.7 KB · Views: 12
  • FB_IMG_1791537344207.jpg
    FB_IMG_1791537344207.jpg
    71 KB · Views: 10
  • FB_IMG_1791537382971.jpg
    FB_IMG_1791537382971.jpg
    67.1 KB · Views: 11
  • FB_IMG_1791537335277.jpg
    FB_IMG_1791537335277.jpg
    75 KB · Views: 12
  • IMG_20261008_125638_983.jpg
    IMG_20261008_125638_983.jpg
    812.8 KB · Views: 12
  • IMG_20261008_125108_867.jpg
    IMG_20261008_125108_867.jpg
    1.1 MB · Views: 13
  • IMG_20261008_124948_449.jpg
    IMG_20261008_124948_449.jpg
    973.5 KB · Views: 9
  • IMG_20261008_124844_276.jpg
    IMG_20261008_124844_276.jpg
    871 KB · Views: 12
  • IMG_20261008_124759_263.jpg
    IMG_20261008_124759_263.jpg
    732.5 KB · Views: 11
Back
Top Bottom