Kagueni magari yenu yakitoka kufanyiwa marekebisho.

Kagueni magari yenu yakitoka kufanyiwa marekebisho.

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
IMG_20230402_172137.jpg

IMG_20230402_172100.jpg

Gari inagonga fundi anasema ni shock up. Anapewa hela ya kununua shock up zingine.

Kinyume chake anaweka hizo rubber kwenye Coil.

Kifuatacho badala ya Impact kubwa kuishia kwenye Coil na shock absorbers. Impact kubwa inaishia kwenye bodi.
 
Kwanza usimuamini fundi cha pili usiwe mlalamishi sana ukienda service na usiondoke mpka gari yako ipone.

Siku moja nilienda garage moja nikawapa gari watengeneze na fundi sio mgeni kwangu basi jamaa akaweka gari sawa nikaondoka nikarudi ndani ya dakika kadhaa naona wanahangaika kuipandisha gari juu bahati nzuri kulikua na coaster private dereva kalala ndani nikazama nikawa nimekaa mbele pale nikamtonya dereva soma mchezo nn kinafanyika pale jamaa wakaanza kukata masega nikawa nimeshamstua mwanangu yupo kituo kimoja town akaja fasta akawapa gari kama anataka lifunguliwe miguu alafu naye akapotea akaja akapanda kwenye coaster nilipo jamaa alipojiridhisha kuwa walikua na nia ya kuiba masega akashuka akawatia nguvuni wakarushwa utuo chap pale wakajieleza wenyewe na wakataja gari ngapi washaiba masega wakalipa nikawaachia polisi mtu wao ki masihara jamaa akapotea mwaka ametoka kila akiniona hapo garage anawaambia wenzake hii gari nahudumia mimi asiguse mtu mwingine ni yamoto hii gari. Ila ilisaidia kupunguza uwizi wa masega kizembe
 
View attachment 2574165

View attachment 2574166

Gari inagonga fundi anasema ni shock up. Anapewa hela ya kununua shock up zingine.

Kinyume chake anaweka hizo rubber kwenye Coil.

Kifuatacho badala ya Impact kubwa kuishia kwenye Coil na shock absorbers. Impact kubwa inaishia kwenye bodi.
Nilipoamua kuwa fundi wa gari langu mwenyewe watu walimibeza....

Leo sina ugomvi na mafundi..

Kama huwezi kuwa fundi wa gari lako, nakushauri simamia mafundi, wafungue kitu chenye hitilafu, uende dukani mwenyewe...

Na hata siku moja, usiache kifaa chako kilichotolewa kwenye gari garage....

Labda kama umejiridhisha kuwa kimeharibika kabisaa....

Hawa mafundi nyundo, huwa nawaachiaga kazi za kulala huko chini huku nimewasimamia vilivyo..
 
Dar mna Mafundi mashetani sana..lakini Mwenye gari nae anakuwa wapi haulizi hata shock up mpya zilizofungwa ziko wapi na zilizotolewa ziko wapi
Mkuu kuna watu hawataki kujitesa, akifika kazini anampigia kijana aje achukue gari akalioshe,
Au anampigia fundi aje achukue gari akalifanyie service...hayo ndiyo matokeo yake....

Au pengine mwenye gari alishauriwa hivyo, naye akakubali kimbuzi mbuzi..
 
Mafundi Mafundi sijui wana shida gani, Fundi ujenzi shida, Fundi Magari ndo usiseme, Fundi Nguo ndo sikwambii, Fundi Simu huyu ndo weka mbali na Watoto yaani Mtu akiwa Fundi sijui anakuwaje!!!!
Fundi wengi ni wezi wezi tu.Ikiwa kazi ni kubwa na usimamizi wako ni mdogo au hakuna basi nendeni kwa mwanasheria mkabidhiane kazi
 
Shida ya mafundi wanatamaaa mmi binafsii uwa namsimamia fundi ad ananiita boss kipereee juzi naenda kubadili hydraulic ya gear box ATF ajaja na ya Toyota OG anasema 90k kwakuwa mm nilikuwepo nkaend dukn kutafuta io ATF nikaipata kwa 65k sasa tamaaa x ndo zinafany hivyo usimamiz muhimu
 
Wewe ndio ulipigwa ATF ya Toyota type yoyote Ile inauzwa si chini ya 100k Sasa hiyo ya 65k ni zile za kutengenezwa kariakoo Ila Zina madumu ya Toyota
 
Back
Top Bottom