Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, amezifariji familia mbili zilizopoteza watoto wanne, wakati wakiogelea kwenye bwawa lililokuwa likitumika katika ujenzi.
Tukio hilo limetokea Februari 15, mwaka huu, majira ya jioni, wakati watoto hao wakitoka shambani kata ya Bulige, Halmashauri ya Msalala na kupita kwenye bawawa hilo kuogelea, na maji kuwazidi nguvu na kuzama.
Mhita amesema, maeneo yote yenye madimbwi au visima vya maji viwekewe uzio na mlango wa kuingilia na kutokea, ili kuwazuia watoto kuingia ovyo.
Aidha amewataka, TARURA na TANROAD, wanapomaliza ujenzi wa barabara, kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali za vijiji na kata juu ya mashimo waliyoacha wakati wakichimba molamu, ili waangalie namna ya kudhibiti lisileta maafa.
Source: Nipashe