Kahama: Diamond atua kwa helikopter . Amwaga noti 'live'

Kahama: Diamond atua kwa helikopter . Amwaga noti 'live'

exalioth

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
2,263
Reaction score
3,897
Haijawai kutokea kwa maeneo yetu huku
Msanii diamond platnumz alipotinga viwanja vya masumbwe ilikua nishida, hata kupumua sababu vumbi lililokuepo pale na ukichanganya na nyomi ya watu waliokuepo,

tunakuombea upige kazi kuiwakilisha nchi yetu kwani mtaji wako ni shabiki,

Ila mimi sio shabiki wa mziki wa dizaini hii ukiendelea na ubunifu katka mziki wako utafika mbali.

Imetumwa na Exalioth
Natumia jamiiforum
Screenshot_2019-06-05-11-38-41.jpeg
Screenshot_2019-06-05-11-38-36.jpeg
Screenshot_2019-06-05-11-37-37.jpeg
Screenshot_2019-06-05-11-37-55.jpeg
 
Kwa zaidi ya saa 24 mji wa Kahama, Shinyanga umetawaliwa na mwanamuziki Diamond Platnumz ambaye leo atafanya onyesho lake la One Mic, One Man katika uwanja wa mpira wa Kahama.


Katika maeneo mbalimbali ameonekana akifuatwa na msafara wa bodaboda, bajaji, magari na waendao kwa miguu wakimshangilia huku wakisema ‘Simba’, ‘Simba’, ‘Simba’.


Jana aliwasili katika mji huo kwa usafiri wa helkopta na kutua katika Kijiji cha Masumbwe ambapo alilakiwa na mamia wa mashabiki.
Katika kusherehesha mkusanyiko huo, Diamond alifungua burungutu la noti na kuanza kuzimwaga kwa mashabiki hali iliyougeuza eneo hilo kufunikwa kwa vumbi kutokana na mashabiki kuzirukia kila mmoja akijaribu bahati yake.


Mwanamuziki huyo anayetamba na wimbo Inama, katika Uwanja wa Kahama jana alimwaga noti kwa mashabiki waliofika kumshuhudia ikiwa ni takribani saa 24 kabla ya onyesho lake hilo la kwanza katika Mji huo katika kipindi cha miaka saba.


Meneja wa mwanamuziki huyo, Babu Tale amesema WCB ilitenga fedha nyingi kwaajili ya onyesho hilo na lengo kubwa likiwa ni kurudisha shukrani kwa jamii.
Amesema mbali na fedha zilioonekana wazi, Diamond ametoa misaada ikiwamo katika kituo kinacholea watoto wenye ualbino, Buhangija.



“Ukipiga hesabu za kila kitu tulichofanya tangu mwanzo mpaka sasa unaweza kuta inafika Sh100 milioni lakini hilo sio muhimu kwetu, kikubwa ni kurudisha fadhila kwa jamii ambayo imemuunga mkono msanii wetu miaka mingi,” alieleza.


Diamond pia aliandaa futari maalumu jana jioni ambayo iliwakutanisha watu mbalimbali katika mji huo.

My take:

Diamond aliruka na helkopter akitokea Dsm ?
diamondpic.jpeg
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Soma ile comment yako na hii alafu utafakari vizuri.
Sina cha kutafakari bongo fleva mahali kwake ni ukumbini siyo kwenye viwanja vya soka.

Labda kwa sababu huko usukumani wanachotaka ni kumuona Dai na si kupata burudani yenye " viwango"!!!
 
Back
Top Bottom