Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Roho mbaya ni hatari kwa Afya yako...!Ameanza kufanya show kwenye viwanja vya kandanda?........nadhani anamfuata Mr Nice!
"Atakuwa na marafiki wengi, lakini watakatifu kwake itakuwa ngumu"mtu mwenye pesaaa [kwa sauti ya marehemu banza stone]
Kwakumwaga mihela Nayeye anataka aitwe Askofu kama Mollel wa madini aliye rest majuziKwa zaidi ya saa 24 mji wa Kahama, Shinyanga umetawaliwa na mwanamuziki Diamond Platnumz ambaye leo atafanya onyesho lake la One Mic, One Man katika uwanja wa mpira wa Kahama.
Katika maeneo mbalimbali ameonekana akifuatwa na msafara wa bodaboda, bajaji, magari na waendao kwa miguu wakimshangilia huku wakisema ‘Simba’, ‘Simba’, ‘Simba’.
Jana aliwasili katika mji huo kwa usafiri wa helkopta na kutua katika Kijiji cha Masumbwe ambapo alilakiwa na mamia wa mashabiki.
Katika kusherehesha mkusanyiko huo, Diamond alifungua burungutu la noti na kuanza kuzimwaga kwa mashabiki hali iliyougeuza eneo hilo kufunikwa kwa vumbi kutokana na mashabiki kuzirukia kila mmoja akijaribu bahati yake.
Mwanamuziki huyo anayetamba na wimbo Inama, katika Uwanja wa Kahama jana alimwaga noti kwa mashabiki waliofika kumshuhudia ikiwa ni takribani saa 24 kabla ya onyesho lake hilo la kwanza katika Mji huo katika kipindi cha miaka saba.
Meneja wa mwanamuziki huyo, Babu Tale amesema WCB ilitenga fedha nyingi kwaajili ya onyesho hilo na lengo kubwa likiwa ni kurudisha shukrani kwa jamii.
Amesema mbali na fedha zilioonekana wazi, Diamond ametoa misaada ikiwamo katika kituo kinacholea watoto wenye ualbino, Buhangija.
“Ukipiga hesabu za kila kitu tulichofanya tangu mwanzo mpaka sasa unaweza kuta inafika Sh100 milioni lakini hilo sio muhimu kwetu, kikubwa ni kurudisha fadhila kwa jamii ambayo imemuunga mkono msanii wetu miaka mingi,” alieleza.
Diamond pia aliandaa futari maalumu jana jioni ambayo iliwakutanisha watu mbalimbali katika mji huo.
My take:
Diamond aliruka na helkopter akitokea Dsm ?View attachment 1118443
Kumbi zinawafaa akina Kiba...yule kumbi haitoshiHapo Kahama mmekosa kumbi za kisasa?!!!
Kwani hapo kwenye uwanja wa Ndondo kiingilio ni bei gani?!!Kumbi zinawafaa akina Kiba...yule kumbi haitoshi
'hukumu ya kifo ipo pale paleeeee'"Atakuwa na marafiki wengi, lakini watakatifu kwake itakuwa ngumu"
'hukumu ya kifo ipo pale paleeeee'
Hawezi kuishi milele, oooh!! Milele.'hukumu ya kifo ipo pale paleeeee'
Drake huwa anatoa hela... Mbona kawaida tuHivi Mayweather naye huwa anamwaga hela kwa mashabiki,au yule JZ ambaye ametangazwa na forbes kuwa billionare wa hip hop artist mbona sijawahi kusikia akirusha mahela kwa mashabiki?au hii ni kibongobongo zaidi...!