Kahama VS Njombe/Mafinga

WAcha wawekezaji waendelee kupiga vitu vya Tano kwenda juu
 

Askofu na bashungwa wapo sahihi ukiangalia hapo tayar mnategemea taasisi zije ziwekeze Waka miji ya wenzenu kusini watu wanawekeza wenyewe mfano niliangalia mall unayosema inajengwa na tasisi ya kislam nikafananisha na project ya business complex ya mfanyabiashara wa kati makambako ni kaona almost zinaendan kamakuizidi ni sq mita chache Sana na ndio maana tuliwambia Huku watu Wana pesa na saiz wanazidi kuonyesha pesa zao kwenye uwekezaji wa mijengo ya biashara na viwanda
 

Attachments

  • IMG_20231209_103411_338~2.jpg
    133 KB · Views: 1
Uwekezaji wa plaza huo ndani ya makambako tc kazi inaendelea wanamaanisha Sasa kuwa ni mji wa biashara na viwanda
 
Disclaimer... please husifananishe hayo majengo Yako na Bakwata commercial complex mkuu...mradi wenye square meter karibu 5000...majengo kama hayo yamejaa Bukoba...siwezi kuanza kupost moja moja hapa...ila mkoa wa Kagera uko top ten katika mikoa yenye nyumba za ghorofa ikiwa na ghorofa zaidi ya 700

Eti taasisi? Hiv unajua NHC Wana viwanja vingapi hapo Bukoba mjini kati? Eneo lote la old Bukoba linamilikiwa na NHC...so si vibaya kwao kujenga majengo ya kisasa
Hapa Tanzania ni miradi mingapi ni ya watu binafsi ni mikubwa? Tazama hata hapa Dar...majengo yote marefu na makubwa ni mashirika...

Kuhusu kuwekeza nyumbani juzi waziri wa mambo ya nje kasema hakuna mkoa unaongoza kwa Remittance kama Kagera.... hayo wanayosema bashungwa ni kukazia tu....lakin kuwekeza nyumbani Kagera haina mpinzani nchi...
 
Uwekezaji wa plaza huo ndani ya makambako tc kazi inaendelea wanamaanisha Sasa kuwa ni mji wa biashara na viwanda
View attachment 2853224View attachment 2853225View attachment 2853226
Kimsingi napitaga hapo makambako ni mji wa kawaida tu tena huwezi linganisha na kahama au hata nzega huko Tabora...
Hiyo plaza ni fremu tu hizo...

Hebu leteni vijiji vyenu kwanza tuvione maana sijawahi kuona mnapost vijiji

View: https://www.instagram.com/p/C1SiHfkNl8C/?igsh=MzRlODBiNWFlZA==
 
Leta vijiji vyenu tuone.... Bukoba watu wanajenga vijijini kwao aisee...

View: https://www.instagram.com/reel/C1R8-cbNwD1/?igsh=MTc4MmM1YmI2Ng==
Shida yenu bukoba mnapenda sifa ila maendeleo ya kujisifia yanawa kataa ndio maana ukifatilia nyuz zote za humu we jamaa picha zako ni zilezile hazibadiliki na maneno ni yaleyale kitu ambacho unapaswa kujua watu saiz uchumi ulisha badilika na elimu now ipo Kila Kona ndo maana saiz kama unatembea maeneo mengi kwenye ujenzi yamebadilika kutokana kwa kuimarika miundombinu saiz tunachoangalia kwenye miji mji una dira Gani ya kimaendeleo full stop
 
Dira ya mji wenu ndo itawatoa huko mlipo na si maneno ya kujisifia tu Kagera Kuna haja kujifunza mikoa mingine safi Sana mkoa wa njombe unaendelea kujipambanua zaidi
 
S
Stend imewashinda kusimamia hadi tamisemi inaingilia kati nyie mjitafakari
 
Yan we jamaa unachekesha nyumba za aina HiYo kwa mkoa wa njombe zimetapakaa Kila Kona

S

Stend imewashinda kusimamia hadi tamisemi inaingilia kati nyie mjitafakari
Watu mnaongelea Stendi tu mkianza kuongelea Bukoba....ile ni sehemu tu ya kupark magari.....Tamisemi inaingiliaje wakati ndo majukumu yake...
Nyinyi mbona hatuwasemi huko kusini kukosa viwanja vya ndege, hakuna viwanja vya mpira, miji yenu ni slums, Barbara mbovu tukianza na mbeya tu...vijumba Hadi vya udongo mijini...
 
Eti maendeleo yanawakataa.... Maendeleo ni Nini kwanza tuanzie hapa...

Mimi nilitembelea huko kusini mwaka huu Bado Kuna umaskini mkubwa..huko ludewa Kuna vijiji havina Barbara kabisa na hata gari hawajahi ona...halafu eti ndo mkoa wenye kipato...kwanza una watu lakin saba tu sawa ni Wilaya tu ya muleba

Huku ndo muleba kama haya ndo maendeleo yanayowakataa wahaya then utakuwa unamatatizo
 

Attachments

  • 43b888ccc4c1fc12579f9bbcf1f04df9.mp4
    4.8 MB
Tafiti zinaongea si maneno ya kujifariji fanyeni kazi mkoa wenu uwe na dira mnataka mkoa wenu ukue kwa mfumo gan
 
Shida ni ujuaji mwingi Kila mmoja anijiona anajua ndo yanawapeleka Huko👇👇👇👇👇WAZIRI MCHENGERWA AKEMEA WANASIASA WANAOKWAMISHA MIRADI YA MAENDELEO

OR -TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amekemea tabia ya wanasiasa na watumishi wa serikali kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Amesema wakati wa uongozi wake watu wa aina hiyo atawashughulikia bila kuwamuonea haya.

Mchengerwa ameyasema hayo mjini Bukoba wakati wa hafla ya utiliaji Saini mikata ya usanifu wa miradi ya uboreshaji miundombinu ya miji Tanzania (TACTIC) kwa ajili ya miji 15 ya kundi la pili (Tier2) ambayo utekelezaji wake utagharimu Sh bilioni 8.25.

Amesema taarifa alizonazo ni kuwa, kumekuwapo na baadhi ya wanasiasa ambao kwa maslahi yao binafsi na ya kisiasa wamekuwa wakikwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Bukoba na maeneo mengine mkoani Kagera.

"Ninatambua wako baadhi ya wanasiasa wanaojali matumbo yao ambao wanaokwamisha kwa makusudi utekelezaji wa miradi hivyo sitowavumilia kwani wanakwamisha jitihada za Mhe. Rais za kuleta maendeleo". Mhe. amesisitiza.

Amesema wapo baadhi ya madiwani wanakwamisha miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Bukoba na kuonya kuwa hatasita kusitisha vikao vya Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Bukopa mpaka watakapokamilisha miradi.

“Kiongozi yeyote wa kisiasa anayepanga kukwamisha utekelezaji wa miradi hii ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia ameamua kuwakomboa wana Bukoba kiongozi huyo nitamshughulikia ipasavyo,”

Amesema Mkoa wa Kagera unachelewa kupata maendeleo kwasababu kuna baadhi ya watu wanauhujumu kwa kujali maslahi yao binafsi hususani ya kisiasa.

Ameongeza kuwa, kuna baadhi ya maeneo miradi haitekelezwi vizuri kwasababu baadhi ya viongozi wa Serikali wanaingilia mchakato wa zabuni na kuzipatia kampuni zao.

Awali, akitoa maelezo ya mradi wa TACTIC, Mratibu wa Kikundikazi kinachosimamia miradi inayopata fedha kutoka Benki ya Dunia Bw. Humphrey Kanyenye, alisema mradi unagharamiwa na serikali kuu kwa Shilingi trilioni moja kupitia masharti ya nafuu ya mkopo kutoka Benki ya Dunia na utanufaisha Miji 45.

“Mradi utatekelezwa kwa miaka sita kuanzia mwaka wa fedha 2022/23, lengo kuu ni kuboresha usimamizi wa ukuaji wa miji pamoja na kuwezesha Halmashauri za Miji na Majiji kutoa huduma bora kwa wananchi, na kuongeza kuwa maeneo ya utekelezaji ni ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwamo barabara na miundombinu mingine kulingana na vipaumbele vya halmashauri husika.”

Amesema kundi la kwanza linahusisha Miji 12 ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma, Morogoro, Kahama, Kigoma, Songea, Sumbawanga, Tabora, Geita na utekelezaji wake umeanza mwaka huu wa fedha 2023/24.

Amefafanua kuwa, kundi la pili litahusisha Miji 15 ya Tanga, Korogwe, Moshi, Kibaha, Iringa, Bukoba, Singida, Bariadi, Shinyanga, Musoma, Lindi, Mpanda, Njombe, Mtwara na Babati na utekelezaji wake utaanza mwaka ujao wa fedha 2024/25 mara baada ya usanifu kukamilika.

“Kundi la tatu linahusisha Miji 18 ya Kasulu, Tunduma, Vwawa, Ifaraka, Masasi, Nanyamba, Handeni, Bagamoyo, Mafinga, Tarime, Chato, Bunda, Mbinga,Mbulu, Nzega, Kondoa, Newala ambao utekelezaji utaanza mwaka wa fedha 2024/25,” Bw. Kanyenye ameanisha.

Alieleza kuwa, kundi la kwanza wakandarasi wameshapatikana na kundi la tatu zabuni zinatarajiwa kutangazwa ili kuwapata wasanifu mwezi Januari 2024.

“Leo tutashuhudia utiaji saini wa mikataba kwa ajili ya usanifu wa miundombinu ya kipaumbele katika kundi la pili ambapo miundombinu mbalimbali itafanyiwa usanifu ikiwamo stendi ya mabasi, masoko na mitaro ya kupitisha maji ya mvua na inagharimu Shilingi bilioni 8.25 kwa Miji 15 ikihusisha gharama za upembuzi yakinifu, usanifu wa kina,kuandaa makisio ya ujenzi pamoja na kutangaza zabuni ili kuwapata wakandarasi ambao watatekeleza mikataba kwa muda wa miezi nane kuanzia mwezi Desemba 2023, amesema.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Denis Londo, alisema miundombinu itakayojengwa itachochea uwekezaji, kuongeza uzalishaji na kuwaondolea watanzania umaskini huku akiwahimiza wananchi kwenye Halmashauri zinazonufaika na mradi huo kuitunza miundombinu inayojengwa.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Fatuma Mwassa, alimshukuru Rais kwa kutoa fedha za uboreshaji wa Miji 15 nchini ikiwamo Manispaa ya Bukoba na kwamba hitaji la Soko na Stendi kwenye Manispaa hiyo limekuwapo kwa takriban miaka 40.
 
SITAKI UBABAISHAJI KWENYE UJENZI WA STENDI YA MABASI YA BUKOBA

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amekemea ubabaishaji katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi Kagera.

Pia amesema yeyote atakayeingiza mikono yake wakati wa utekelezaji mradi huo atachukuliwa hatua bila kujali ni mwanasiasa au wa Serikali.

Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa kukagua eneo litakalotumika kujenga stendi ya kisasa Kykailabwa manispaa ya Bukoba.

Amesema kazi hii itasimamiwa na TARURA ambao wanakuwa chini ya Mkoa, hatutaki ubabaishaji tunataka miradi itekelezwe na yeyote atakayeingiza mkono bila kujali ni mwanasiasa au serikali nadhani nimeeleweka."

"Kazi ifanyike vizuri ili kila mwana Kagera aliyopo ndani na je ya nchi warudi hapa wajionee matunda ya kazi iliyofanywa."

Amesema maelekezo ya Rais Samia ni kutaka stendi ya Kagera iwe ye mfano na kusisitiza kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI itakuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara.

"Baada ya kukagua alisema baada tu upembuzi yakinifu (feasibility study) kufanyika kwenye stendi ya mabasi ya Kyakailabwa, ripoti iwasilishwe Wizarani kwa mapitio na maoni ndipo usanifu wa kina (detailed design) ufuate, tunataka stendi ya Kagera iwe ya mfano na ndio maelekezo ya Rais."

"Usimamizi kama tulivyokubaliana TARURA watafanya usimamizi lakini wanapokuwa mikoani Tarura wanakuwa chini ya Mkoa hatutaki ubabaishaji tunataka miradi itekelezeke kikamilifu."

Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Bukoba, Amid Njovu alisema eneo hilo lina kubwa wa ekari 14 la litakuwa na Eneo la daladala, magari binafsi na mabasi ya yaendayo mikoani.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa alisema kilio cha stendi na soko kwa wanaKagera ni cha miaka 40 na kushukuru Rais Samia Suluhu Hassan katika kutimiza hilo."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…