Shida ni ujuaji mwingi Kila mmoja anijiona anajua ndo yanawapeleka Huko👇👇👇👇👇WAZIRI MCHENGERWA AKEMEA WANASIASA WANAOKWAMISHA MIRADI YA MAENDELEO
OR -TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amekemea tabia ya wanasiasa na watumishi wa serikali kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Amesema wakati wa uongozi wake watu wa aina hiyo atawashughulikia bila kuwamuonea haya.
Mchengerwa ameyasema hayo mjini Bukoba wakati wa hafla ya utiliaji Saini mikata ya usanifu wa miradi ya uboreshaji miundombinu ya miji Tanzania (TACTIC) kwa ajili ya miji 15 ya kundi la pili (Tier2) ambayo utekelezaji wake utagharimu Sh bilioni 8.25.
Amesema taarifa alizonazo ni kuwa, kumekuwapo na baadhi ya wanasiasa ambao kwa maslahi yao binafsi na ya kisiasa wamekuwa wakikwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Bukoba na maeneo mengine mkoani Kagera.
"Ninatambua wako baadhi ya wanasiasa wanaojali matumbo yao ambao wanaokwamisha kwa makusudi utekelezaji wa miradi hivyo sitowavumilia kwani wanakwamisha jitihada za Mhe. Rais za kuleta maendeleo". Mhe. amesisitiza.
Amesema wapo baadhi ya madiwani wanakwamisha miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Bukoba na kuonya kuwa hatasita kusitisha vikao vya Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Bukopa mpaka watakapokamilisha miradi.
“Kiongozi yeyote wa kisiasa anayepanga kukwamisha utekelezaji wa miradi hii ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia ameamua kuwakomboa wana Bukoba kiongozi huyo nitamshughulikia ipasavyo,”
Amesema Mkoa wa Kagera unachelewa kupata maendeleo kwasababu kuna baadhi ya watu wanauhujumu kwa kujali maslahi yao binafsi hususani ya kisiasa.
Ameongeza kuwa, kuna baadhi ya maeneo miradi haitekelezwi vizuri kwasababu baadhi ya viongozi wa Serikali wanaingilia mchakato wa zabuni na kuzipatia kampuni zao.
Awali, akitoa maelezo ya mradi wa TACTIC, Mratibu wa Kikundikazi kinachosimamia miradi inayopata fedha kutoka Benki ya Dunia Bw. Humphrey Kanyenye, alisema mradi unagharamiwa na serikali kuu kwa Shilingi trilioni moja kupitia masharti ya nafuu ya mkopo kutoka Benki ya Dunia na utanufaisha Miji 45.
“Mradi utatekelezwa kwa miaka sita kuanzia mwaka wa fedha 2022/23, lengo kuu ni kuboresha usimamizi wa ukuaji wa miji pamoja na kuwezesha Halmashauri za Miji na Majiji kutoa huduma bora kwa wananchi, na kuongeza kuwa maeneo ya utekelezaji ni ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwamo barabara na miundombinu mingine kulingana na vipaumbele vya halmashauri husika.”
Amesema kundi la kwanza linahusisha Miji 12 ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma, Morogoro, Kahama, Kigoma, Songea, Sumbawanga, Tabora, Geita na utekelezaji wake umeanza mwaka huu wa fedha 2023/24.
Amefafanua kuwa, kundi la pili litahusisha Miji 15 ya Tanga, Korogwe, Moshi, Kibaha, Iringa, Bukoba, Singida, Bariadi, Shinyanga, Musoma, Lindi, Mpanda, Njombe, Mtwara na Babati na utekelezaji wake utaanza mwaka ujao wa fedha 2024/25 mara baada ya usanifu kukamilika.
“Kundi la tatu linahusisha Miji 18 ya Kasulu, Tunduma, Vwawa, Ifaraka, Masasi, Nanyamba, Handeni, Bagamoyo, Mafinga, Tarime, Chato, Bunda, Mbinga,Mbulu, Nzega, Kondoa, Newala ambao utekelezaji utaanza mwaka wa fedha 2024/25,” Bw. Kanyenye ameanisha.
Alieleza kuwa, kundi la kwanza wakandarasi wameshapatikana na kundi la tatu zabuni zinatarajiwa kutangazwa ili kuwapata wasanifu mwezi Januari 2024.
“Leo tutashuhudia utiaji saini wa mikataba kwa ajili ya usanifu wa miundombinu ya kipaumbele katika kundi la pili ambapo miundombinu mbalimbali itafanyiwa usanifu ikiwamo stendi ya mabasi, masoko na mitaro ya kupitisha maji ya mvua na inagharimu Shilingi bilioni 8.25 kwa Miji 15 ikihusisha gharama za upembuzi yakinifu, usanifu wa kina,kuandaa makisio ya ujenzi pamoja na kutangaza zabuni ili kuwapata wakandarasi ambao watatekeleza mikataba kwa muda wa miezi nane kuanzia mwezi Desemba 2023, amesema.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Denis Londo, alisema miundombinu itakayojengwa itachochea uwekezaji, kuongeza uzalishaji na kuwaondolea watanzania umaskini huku akiwahimiza wananchi kwenye Halmashauri zinazonufaika na mradi huo kuitunza miundombinu inayojengwa.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Fatuma Mwassa, alimshukuru Rais kwa kutoa fedha za uboreshaji wa Miji 15 nchini ikiwamo Manispaa ya Bukoba na kwamba hitaji la Soko na Stendi kwenye Manispaa hiyo limekuwapo kwa takriban miaka 40.
View attachment 2853278