Kahama VS Njombe/Mafinga

RC MTAKA AMUELEZA BALOZI DKT. NCHIMBI KUWA VIONGOZI THABITI WA NJOMBE NI FAIDA YA UWEKEZAJI WA CCM

Asema Bilioni 900 zimetumika kwa maendeleo mkoani Njombe

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ndugu. Anthony Mtaka , amemueleza Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Viongozi thabiti na imara wa mkoa wa Njombe ni faida iliyotokana na zao la uwekezaji wa Chama Cha Mapinduzi kuanzia Chipukizi hadi Vijana.

RC Mtaka ameyasema hayo mbele ya Maelefu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa stendi ya zamani ya makambako kwa ajili ya ushiriki wao kwenye mkutano wa hadhara.

Pia, RC Mtaka amemueleza Balozi Dkt. Nchimbi kuwa Maendeleo yaliyopo mkoani Njombe katika kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Rais Dkt. Samia ambapo amesema kiasi cha Tsh Bilioni 900 kimetumika kwa maendeleo katika sekta mbalimbali.

"Njombe kuna matunda ya watu uliowalea ukiwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na haya yote ni mafanikio ya uwekezaji wa CCM kwa Chipukizi na Vijana"

"Tunakuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kulinda heshima ya CCM ndio maana madiwani, wabunge, wenyeviti wa serikali za mitaa na viongozi wa chama wote wana ushirikiano wa timu moja katika kazi"

"Njombe kazi kubwa imefanyika na katika kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeletwa fedha Tsh Bilioni 900 na kutumika katika sekta zote za mendeleo ya kijamii (afya, maji, umeme (85% zaidi vijiji vyote vina umeme),)

"Makambako ni eneo la uwekezaji wa kibiashara na litapelekea kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa wananchi wa Njombe"

🗓️18 Aprili, 2024
📍Makambako - Mkoani Njombe

#CCMkazini
#VitendoVinaSauti
#TuaendeleaNaMama
#KaziIendelee
 
Kumbe Kuna Barabara ya Kutoka Makambako Hadi Mgololo? Je haifiki upande wa Morogoro? Mk boy

View: https://www.instagram.com/p/C6EsJ0StVl9/?igsh=OHN1M3lxbWhxa2lv
Zipo mbili Kuna ya makambako hadi mgololo Kuna makambako igowole zote hizi Zinatoboa morogoro ndo wanadai zipo kwenye usanifu iliwapige lami ila kama ya igowole tayari Kuna vipande vingine vina lami ila Kuna baadhi ya vipande havijafunguliwa hasa upande wa morogoro ukitoka mpakani na morogoro hadi makambako ipo vizuri Na kule njia nyingi zinatumika za Sao hill Wamepanda miti mingi hadi morogoro wakiamua kuzifungua Ina fika maana makambako mlimba ni km 162 kupitia reli sawa na makambako iringa Ko itakuwa na distance fupi kwa Barabara ya kupitia igowole itakuwa 120km distance ni fupi kuliko ya lupembe na hii ya kupitia igowole tayari km 70 zinapigwa lami 30 wameshamaliza wanaendelea na kipande Cha km 40 Zina Baki kama km 20 kuunganisha na mlimba wakati ya lupembe Ile inaenda zaidi ya km 223
 
Mufindi ya Samia inasonga Mbele tunakuombea kheri Mhe. Rais @samia_suluhu_hassan unapoanza safari yako Nchini Uturuki, Sisi wana Mufindi tunakupenda na hakika Mfupa ulioshindikana na wengine kwa Miaka 60, umeanza kuutafuna kwa kasi.
Leo nitataja mambo 5 tu:

1. MAJI: Kati ya Vijiji 71 Mwaka 2021 ni Vijiji 5 vilikuwa na maji, Leo Miradi ya Maji imepelekwa kwenye Vijiji zaidi ya 50.

2. Barabara za lami: Mpaka Mwaka 2021 Wananchi walifika mahala wakachoka na ahadi za lami, lakini leo hii:
•Nyololo-Mtwango Km 40.4 Mkandarasi yuko site,
•Sawala-Luhunga mkandarasi amemaliza Km 30 na anamalizia 10,
•Igowole inapata lami Mtaani km 1.2,
•Barabara ya Mafinga Mgololo Mkataba umesainiwa tunasubiri kazi ianze muda wowote taratibu zikikamilika. •Usanifu wa kina umeanza kwa barabara ya Makambako- Mgololo

3. Elimu: Ujenzi Chuo VETA unaendelea, Ujenzi shule mpya 3 za Sekondari na za Msingi zaidi ya 20.

4. Kilimo&Mifugo:
•Tunakushukuru kwa kututua mzigo wa bei za Mbolea toka 130,000 mpaka 70,000 kupitia ruzuku,
•Ujenzi kiwanda cha parachichi Nyololo,
•Ugawaji Vifaranga vya Samaki katika Mabwawa ya Nzivi, Ngwazi na Kihanga etc
•Animal Gift, Mradi wa wadau wa ugawaji wanyama hai kwa wananchi( Takribani Ng'ombe 600, Nguruwe na Kuku zaidi ya 4,000) Ili kufikia agenda yetu ya One Family one cattle.

5. Afya: Asante kwa Vituo vya Afya Mgololo, Mninga, Mtwango na Itandula,
•ukamilikaji Hospitali ya Wilaya Mufindi,
•uboreshaji Kituo cha Afya Malangali na Mbalamaziwa
 
Kuna sms nimekuuliza hapo Juu hujajibu
 
Kuna sms nimekuuliza hapo Juu hujajibu
Ok inatoboa ila hufiki hadi mgololo unachepukia ihawaga hii inapita igowole hadi mlimba na eneo kubwa hii wamepata vipande vya lami na tayari Kuna km kama 40 zimepigwa lami na mwaka huu wamepata 40 tena ko watakuwa na 80 zitabaki km chache Sana kuunganisha na mlimba morogoro
 
Kuna sms nimekuuliza hapo Juu hujajibu
Hii ya makambako hadi mgololo kilibaki kipande cha uchindile hadi mlimba mwakajana ndo wamepata fedha za kukifungua kipande hichi kuunganisha ko itaenda kuungana na iliyotoka ifakara 👇👇👇👇👇👇👇Nao wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa wamekiri uboreshaji wa miundombinu katika halmshauri zao huku akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa kupitia TARURAna kwamba Halmashauri ya mlimba inatarajia kuchonga barabara ya Mlimba - Uchindile yenye km 80 ambayo itawasaidia kuondokana na adha ya kuzunguka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…