Aliyoyazungumza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka Mei 16, 2024 wakati akizungumza na watumishi wa Serikali na taasisi zilizopo Wilayani Ludewa.
“Mkoa mpya utakao shindana kwenye uchumi wa taifa baada ya Arusha ni Mkoa wa Njombe”.
“Mijadala kwenye vikao vya wataalamu ilenge kwenye uwekezaji mkubwa utakaoinua uchumi wa wilaya na taifa,acheni kufanya kazi kwa mazoea ,wilaya mliyo nayo ni wilaya ya pekee kwenye nchi ,akiba ya madini ya chuma na makaa ya mawe ni ya zaidi ya miaka 100.”
“Mwenyekiti wa Halmashauri endesha agenda ya maendeleo ya Halmashauri , Wilaya ni lazima tukimbie, uwekezaji wa Liganga na Mchuchuma umetajwa kwenye dira ya taifa ya 2025-2050.”
“Ludewa mko tayari?, Mhe. Rais ametoa maelekezo kwa Wizara za Viwanda na Biashara pamoja na Wizara inayohusika na uwekezaji ili mwekezaji wa Mchuchuma na Liganga apatikane haraka, Mkuu wa Wilaya anzeni kuzitambua na kuzitangaza fursa zitakazo ibuka kwenye uwekezaji huu mkubwa wa Liganga na Mchuchuma, watu waje kuwekeza kwenye Mahotel,Migahawa ya chakula,vituo vya mafuta na gesi,Maeneo ya ujenzi wa viwanda, maeneo ya biashara mbalimbali, Kilimo cha mbogamboga, Ufugaji pamoja na uwekezaji eneo la ziwa Nyasa.”
“Kuna bahati ambayo Mungu ameishusha Ludewa tuna chuma na makaa ya mawe yanayoweza kuyeyusha hiyo chuma, madini matatu ya Titaniamu, Allunium na Vanidiamu yaliyopo kwenye hiyo chuma ni madini ya thamani sana duniani”
“Kama kuna kitu kitaandikwa kwenye vitabu vya historia ya uchumi wa nchi yetu basi ni maamuzi ya Mheshimiwa Rais kuamua sasa mradi wa Mchuchuma na Liganga utekelezwe, kwani utekelezaji wa mradi huu utaendana sambamba na mageuzi makubwa ya uchumi wa Taifa letu,utekelezaji wa mradi huu pamoja na kuliingizia Taifa letu pesa utazalisha Ajira nyingi kwa vijana wa kitanzania kupitia uchimbaji wa madini yenyewe (Chuma) lakini uongezaji wa thamani kwa bidhaa za viwandani zitakazotokana na chuma itakayo chimbwa sambamba na upatikanaji wa madini mengine matatu (Titaniamu, Allunium na Vanadiamu)”.
📸📸 @chrispin_b__kalinga
#Ludewa #LudewaYetu