UWANJA WA NDEGE NDANI YA HIFADHI YA RUAHA WAZINDULIWA MBEYA
Serikali Kwa kushirikiana na wawekezaji kutoka taasisi ya Six Rivers Africa wamezindua uwanja wa ndege wenye urefu wa kilomita 1.2 ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha mkoani Mbeya, Kwa lengo la kukuza utalii Kwa ukanda wa kusini, kupitia watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani kutua kwenye uwanja huo na kutembelea vivutio Kwenye hifadhi za taifa.
Kamishna msaidizi mwandamizi wa uhifadhi Godwill Ole Meng'ataki ni mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha, anasema uwanja huo mdogo ndani ya hifadhi umekwisha sajiliwa katika mamlaka za usimamizi wa viwanja vya ndege Tanzania na tayari wamepokea maombi mbalimbali ya watalii kuanza kutua kwenye uwanja huo na kutembelea hifadhi za Taifa pamoja na vivutio vilivyopo maeneo ya ukanda wa kusini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Taasisi ya Six Rivers Africa Glenn Turner, ameipongeza serikali ya Tanzania Kwa kutenga eneo kubwa zaidi kuliko Nchi yeyote duniani ambalo limehifadhiwa, huku kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya akiwaomba wahusika kuzingatia usalama wa watu wanaotumia uwanja huo pamoja na wanyama kwakua uwanja huo upo ndani ya hifadhi.
Akimwakilisha Katibu mkuu wa Wizara ya maliasiri na utalii, mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila, ametaka uwanja huo kutunzwa ili utumike Kama uwanja wa dhararu wa kutua ndege za abiria pindi zinapotokeza hitirafu mbalimbali.
View attachment 3023302View attachment 3023303
Cc @enocksaimon
#WasafiDigital