Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

WACHINA WAMESHA SOMA FURSA ZIKO WAPI WANAFUNGUA VIWANDA BALAAA NA WANAASILI YA KUITANA NA BADO WAMEDAI WANAKUJA KUJENGA MIJI YA KIBIASHARA KO TUWE WAPOLE TU NA BADO TAZARA WAKIREKEBISHA VIWANDA VITASHAMIRI ZAIDI NAONA MBUNGE AMEANUA KWENDA KUONGEA HADI BUNGENI KASI YA ONGEZEKO LA HAWA JAMAA HASA MAKAMBAKO NA MAFINGA👇👇👇👇👇👇 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025​

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwapongeza nyote, Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri Mkuu mwenyewe, Mawaziri wote wanaomsaidia Mama Jenista Mhagama, Kaka Ndejembi, Dada Ummy na Kaka Katambi pamoja na wataalam wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa ni pamoja na Makatibu Wakuu wote wawili, Wakurugenzi, Maafisa na watumishi wote; ikiwa ni pamoja na Private Office ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Baada ya pongezi, naomba kutoa maoni na ushauri kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na kazi na ajira, ushauri wangu hususani kuhusu kukuza na kulinda ajira chache hasa katika sekta binafsi, nashauri taratibu za vibali vya kazi ziweze kuzingatiwa. Kwa ilivyo sasa kuna wimbi kubwa la raia kutoka China ambao wamegeuka wachuuzi, siyo Kariakoo tu, bali hata katika miji midogo kama Mafinga, Makambako na kadhalika. Suala hili tusipokuwa makini iko siku litazua tafrani kati ya jamii ya Wachina na Watanzania wazawa japo ni neno lisilopendwa kusikika, kuna kitu kitatokea siyo tu katika nyanja ya uchumi lakini hata kijamii na kidplomasia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ilivyo sasa kunajengeka chuki siyo dhidi ya jamii ya Wachina bali wananchi dhidi ya Serikali, wanasema kuwa Serikali kwa nini inaachia Wachina kushindana na Watanzania kwenye ajira za chini ambazo kimsingi zinapaswa kufanywa na wazawa. Ushauri wangu, tukiliacha jambo hili bila kulidhibiti iko siku litaleta mgongano ambao utatuingiza katika shida ya kimahusiano ya kidplomasia na marafiki zetu wa muda mrefu China.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu BBT; programu hii ambayo inasimamiwa na Wizara ya Kilimo inaweza kuwa msaada mkubwa katika kuongeza ajira kwa vijana. Napongeza hatua zote za awali ambazo zimeanza kuchukuliwa, ushauri wangu, washirikiane na Kilimo na JKT katika kuhakikisha kuwa vijana wanaojitolea JKT wanakuwa sehemu ya wanufaika wa BBT. Naamini watakuwa na mchango mkubwa sana si kwao binafsi tu, lakini na kwa Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kuimarisha Idara ya Tathmini na Ufuatiliaji wa Shughuli za Serikali; kwanza napongeza uamuzi wa Serikali katika kuanzishwa kwa Idara hii muhimu ambayo itasaidia sana hata katika kupunguza hoja za CAG, lakini zaidi katika kuimarisha utendaji Serikalini hususani katika kukamilika miradi kwa wakati. Hata hivyo ili kuwa na matokeo chanya na kutimia kwa malengo ya kuanzishwa kwa Idara hii muhimu, rasilimali fedha na rasilimali watu ni muhimu sana. Katika kipindi kifupi toka kuanzishwa kwa Idara hii imethibitika kuongezeka kwa umakini wa kiutendaji ndani ya Serikali kwa sababu Idara imekuwa kama watch dog ndani ya Mawizara na Taasisi zetu za Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na manufaa haya na kwa faida ya kuokoa gharama kama vile miradi kuchelewa kukamilika ambapo mara kadhaa Serikali imelazimika kuongeza fedha kwa miradi ambayo ilichelewa kukamilika kutokana na kushindwa kufuatilia utendaji wakati miradi inaendelea. Kwa hiyo kuimarisha Idara hii ni sawa na ile tunasema prevention is better than cure kwa maana kwamba kupitia Idara ya Tathmini na Ufuatiliaji tunaweza kuzuia kabla madhara makubwa hayajatokea, ushauri wangu Idara hii itazamwe kwa macho mawili kwa maana ya financing na human resources.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu EPC+F; Serikali ilisaini mikataba kadhaa na wakandarasi wa kujenga barabara kwa kiwango cha lami kwa Mfumo wa EPC+F. Mikataba hii ilisainiwa Juni, 2023 na ni zaidi ya kilometa 2,000, mpaka sasa bado hatujaanza hata kilometa moja. Tatizo tunaambiwa wakandarasi wanaomba kulipwa angalau advance payment ya 10%.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu Serikali ifanye kila linalowezekana ili walau wakandarasi walipwe hii 10% kwa kuwa pamoja na sababu za kiuchumi suala hili kisiasa linaweza kuwa na shida kutokana na ukweli kwamba kama Serikali tulilitangaza sana na kuwapa matumaini wananchi, hivyo kutokuanza kwa miradi italeta ugumu katika chaguzi zijazo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved
 
Haya Sasa china wamekuja kuwekeza kujenga miji ya kibiashara 👇👇👇👇👇👇👇👇Serikali ya Tanzania na China zimesisitiza kuimarisha ushirikiano wa kimkakati ili kuendelea kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa maslahi ya pande zote mbili.

Msisitizo huo umetolewa wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 7 Mei, 2024.

Mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kujadili utekelezaji wa maazimio na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na wakuu wa nchi hizo mbili wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika nchini China mwezi Novemba 2023.

Aidha, wameainisha maeneo mbalimbali ya kimkakati ambayo nchi hizo mbili zimedhamiria kuziendeleza na kuzisimamia kwa maenedeo ya watu wake. Maeneo hayo ni pamoja na kuanzisha na kuimarisha ushirikiano wa miji dada, kukuza ushirikiano wa biashara na uwekezaji, ujenzi wa miji ya kisasa, maendeleo ya viwanda, kilimo cha kisasa na uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo na mifugo na kuboresha mradi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
 
bbfc7f8cf8724acdbed980bef232924b.jpg
 
VIWANDA VYA BIDHAA ZA CHUMA VINAENDA KUIMARIKA ZAIDI NA UWEKEZAJI UNAENDA KUONGEZEKA 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha
asilimia 25 au dola za Marekani 300kwa kila
tani moja ya ujazo (metric ton) kutegemea
kiwango kitakachokuwa kikubwabadala ya
ushuru wa asilimia 25 au dola za Marekani 200
kwa kila tani moja ya ujazo (metric ton) kwa
mwaka mmoja kwenye bidhaa za mabati
zinazotambulika kwa HS codes 7210.49.00;
7210.61.00; 7210.69.00; 7210.70.00;
7210.90.00; na 7212.30.00. Lengo la hatua hii ni
kulinda viwanda vya ndani, kuongeza ajira
pamoja na mapato ya Serikali;
m.Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha
asilimia 25au dola za Marekani 300kwa kila
tani moja ya ujazo (metric ton) kutegemea
kiwango kitakachokuwa kikubwabadala ya
asilimia 35kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za
mabati zinazotambulika kwa HS codes
7212.40.00; na 7212.50.00. Lengo la hatua hii ni
kulinda viwanda vya ndani, kuongeza ajira
pamoja na mapato ya Serikali;
n.Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha
asilimia 10au dola za Marekani 300kwa kila
tani moja ya ujazo (metric ton) kutegemea
kiwango kitakachokuwa kikubwabadala ya
asilimia 10kwa mwaka mmo
 
Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amejinasibu kwamba mkoa huo unautajiri kushinda Ruvuma kwasababu una Madini ya kutosha na udongo wenye rutuba unaostawisha kila zao hivyo wakae mkao wa kula kuona Njombe ikiwapiku kwenye machimbo ya makaa ya mawe pindi mikataba ya Maganga matitu itakaposainiwa pamoja na ule mradi wa Chuma ambao unatajwa kuwa utakapo anaza utatoa ajira za kutosha kwa Watanzania na pia ujenzi wa viwanda vya nondo.

Kauli hiyo ametoa wakati wa mapokezi ya mwenge waa Uhuru kutoka Ruvuma ambako umekagua miradi 72 kabla ya kuwasili Njombe unakokagua miradi 40 yenye thamani ya bil 15.9 @a

View: https://www.instagram.com/p/C8SzL1JtoH4/?igsh=aGF0YWpscGM0c2h4
1702003519700~3.jpg
FmfkrrFWQAE9n_s~2.jpg
 
Back
Top Bottom