Kahama VS Njombe/Mafinga

Makambako
Karibuni kwenye mada.

Nawiwa kuilinganisha na kushindanisha mji wa Kahama na Njombe au Mafinga.

Je, ni mji gani mzuri na una future kubwa kifursa kuliko mwenzie in terms of maendeleo na ukuaji?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka hadi baas lol, sjui nimewaza nn hapa.
 
Iringa kwa kitu gani Bro, ambacho Iringa inaizidi Bukoba ni Makumbusho ya Mkwawa na Uwepo wa vyuo Vikuu basii....ebu tupe Ratiba z Ndege hapo Iringa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibuni kwenye mada.

Nawiwa kuilinganisha na kushindanisha mji wa Kahama na Njombe au Mafinga.

Je, ni mji gani mzuri na una future kubwa kifursa kuliko mwenzie in terms of maendeleo na ukuaji?
Ukiondoa wilaya zote zilizopo kwenye majiji ya Dar na Mwanza..wilaya za pembeni zote hakuna iliyo mfano wa Kahama nchi nzima.
 
Kwahiyo ushetu na msalala kuna watu 900,000 kwahiyo hesabu ya 1.2
Hizi takwim zinahaitaji uthibitisho. Pamoja na ukweli kuwa Kahama iko vizuri, kwa Takwim za watu hao basi ilicheleweshwa kuwa Manispaa. Hii inaweza kuwa sawa na Tunduma, ambako popolation ni kubwa sana hasa mchana
 
Maghorofa sio ukubwa wa mji.. unakaulimbukeni design.. hahahaha

"Njombe + Mafinga + Makambako ndio Kahama moja.".. Chukua hiyo statement peleka bank.. nakuahidi unakopesheka.
Kinachotokea hazijatolewa makusanyo ya kila mji ili kujua ukweli. Na makusanyo hayo yawe ya Domestic(isiwe zile za Makampuni ya Wazungu ya madini), naweza nikasema Njombe na Kahama, bado Njombe ni bora sana, sekta ya madini imeibeba Kahama. Kwa ufupi Kahama kiukubwa haipishani sana na Mafinga au Tunduma(miji iliyokua kwa sababu ya ukubwa wa biashara)
 
Hizi takwim zinahaitaji uthibitisho. Pamoja na ukweli kuwa Kahama iko vizuri, kwa Takwim za watu hao basi ilicheleweshwa kuwa Manispaa. Hii inaweza kuwa sawa na Tunduma, ambako popolation ni kubwa sana hasa mchana
Usemalo ndio ukweli,takwimu hizo ni kubwa sana istoshe kahama mji peke yake inaweza kufikisha wakazi laki 5 mana inaanzia kagongwa...pia muingiliano wa watu ni mkubwa sana malori yote ya kwenda magharibi yanapita hapo
 
Kahama inabebwa na biashara ya mpunga na madini,mpunga,maduka,viwanda vya kuchenjua dhahabu,vituo vya mafuta vinaweza kufika 100
 
Usiisahau Masasi mdau, Korogwe na Katoro.
 
Ukiondoa wilaya zote zilizopo kwenye majiji ya Dar na Mwanza..wilaya za pembeni zote hakuna iliyo mfano wa Kahama nchi nzima.
Tunduma munaiweza?
Ni kwa vile tu mambo ya Kiusalama haiswihi kuweka mji mubwa Tunduma,lakini jmaaa wako juu sana, kwenye hilo tutabishana hadi mwisho.
 
Tunduma munaiweza?
Ni kwa vile tu mambo ya Kiusalama haiswihi kuweka mji mubwa Tunduma,lakini jmaaa wako juu sana, kwenye hilo tutabishana hadi mwisho.
Stand ya Mabasi madogo na kituo cha kushusha mizigo ya malori - Kahama

Stand Kuu ya Kahama, ambayo inahamishiwa nje ya mji, kutoka katikati mwa mji



Mchoro wa stand mpya Kahama itakavyokuwa


Parking ya Malori Kahama


Stand ya Mabasi Tunduma


Stand ya mabasi Njombe
 
Kwahiyo wakuu, mji wenye fursa kwa vijana wanaoanza maisha wenye biashara ndogondogo kama (kuuza nguo,bodaboda,kuuza chips,kutembeza matunda etc) ......kati ya Njombe na Kahama ni upi?
Nguo kahma sawa,,chips usijaribu kule wanakula ugali sana,,matunda matunda,vyuku etc nenda singida,
Njombe kama unajua kulishika jembe sawa sawa nenda
 
Duuuh Kahama hata barabara za mitaa shida. Ukianzia Iringa hadi unaingia Mbeya ni ulaya Africa ile.
Hujui kitu, tofauti ya Kahama na Njombe kwenye barabara kuu ni hii, na bado Ilani ya Chama tawala miradi ya kuinganisha Kahama na Wilaya nyingine ni mingi kuliko hata Njombe yenyewe. Tunaanza na taarifa za google kuhusu mtandao wa barabara kuu zenye lami na uhakika wa lami kati ya Njombe na Kahama.

KAHAMA


NJOMBE


Miradi ya barabara kuu Kahama ni mingi kwa miaka hii mitano kuliko hata Njombe

KAHAMA (KM 1003.31)
Geita – Bukoli – Kahama (km 107);
Tabora – Mambali – Bukene – Itobo – Kahama (km 149);
Mwanangwa – Misasi – Salawe – Kahama (km 149);
Mpanda - Ugala - Kaliua - Ulyankulu - Kahama (km 428);
Kahama – Nyamilangano – Uyogo (km 54);
Mambali – Bukumbi - Ishilimulwa – Shitage– Kahama (105km)
Kagongwa – Bukooba (Kahama) - (km 11.31)

NJOMBE (KM 479.5)
Njombe – Ndulamo – Makete;
 Sehemu ya Njombe – Moronga (km 22.9);
 Sehemu ya Moronga – Makete (km 37.65);

Njombe (Kibena) – Lupembe – Madeke (Mfuji) – Morogoro/Njombe Border (km 125);
Njombe (Ramadhani) – Iyayi (km 74);
Ifakara – Mlimba – Njombe (km 220)

 
Nimeangalia hizo picha nikaona worth nothing, hazina chochote cha kujivunia au kufanya ulinganifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…