Kahama VS Njombe/Mafinga

Hizi takwim zinahaitaji uthibitisho. Pamoja na ukweli kuwa Kahama iko vizuri, kwa Takwim za watu hao basi ilicheleweshwa kuwa Manispaa. Hii inaweza kuwa sawa na Tunduma, ambako popolation ni kubwa sana hasa mchana
Tunduma Bado Sana kwa idadi ya watu ila inaweza lingana na Kahama maana miji yote ni ya kichuuzi na iko shaghalabaghala no ustaarabu kabisa
 
Ukiondoa wilaya zote zilizopo kwenye majiji ya Dar na Mwanza..wilaya za pembeni zote hakuna iliyo mfano wa Kahama nchi nzima.
Njombe,Kasulu,Ifakara,Mbinga,Tunduma,Mafinga nk yote hiyo ni zaidi au sawa na Kahama
 
Iringa kwa kitu gani Bro, ambacho Iringa inaizidi Bukoba ni Makumbusho ya Mkwawa na Uwepo wa vyuo Vikuu basii....ebu tupe Ratiba z Ndege hapo Iringa...

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo ulivyotaja ni baadhi tu ya mambo mengi yanayoizidi BK mengine ni kama yafuatayo,
1.Viwanda
2.Mapato
3.Magorofa/Hotel
4.Miundombinu mizuri eg Stand
5.Utalii hifadhi ya Ruaha
6.Taasisi za elimu kama Vyuo nk
 
Tunduma munaiweza?
Ni kwa vile tu mambo ya Kiusalama haiswihi kuweka mji mubwa Tunduma,lakini jmaaa wako juu sana, kwenye hilo tutabishana hadi mwisho.
Mkuu hiyo sio sababu yenye mashiko kwamba sijui haifai kuwekwa Mji mkubwa unless ufafanue unachotaka kusema hapo
 
Ukiangalia tuu hizo picha unaona Kahama imechoka kweli kweli

Kuna mbuzi mmja humu anaitwa Lofa Tin ,alikuwa anasema eti huwezi jenga stend 2 kubwa Mji usio makao makuu ya mkoa nadhani kwa hiyo render ya stand ya Kahama atajua hajui
 
Mkuu wingi wa miradi sio utekelezaji wake afu nyingi ya hizo barabara za Khm ni regional roads wakati kwa Njombe barabara zote Kati ya ulizozitaja ni Trunk road kwa maana hiyo hata ujenzi wake utamalizika upande wa Njombe kuliko huko na akitoka Magu ndio msahau kabisa kwa sababu ya factor niliyokwambia.

By the way kama watajenga hizo zote itasaidia kuifanya Khm ifikike kirahisi kutoka miji mingine
 
UKITAKA KUJUA KAHAMA BABA LAO ANGALIA HATA SHOW MONDI HUJA KAHAMA MARA NYINGI ZIDI YA HUKO CHAKA
Hizo show zinaendana na ushamba na wingi wa washabiki ,,huku Njombe watu wamestaarabika huwezi wakuta kwenye ushamba huo
 
Hivi njombe sikuhizi si Mkoa lakini!?? Sasa tunalinganisha vipi Mkoa na Wilaya!??


Au Mimi mwenzenu haya Mambo siyaelewi elewi vizuri kwakuwa GS nlpiga FAFAFA!!


Sujawahi fika Njombe Wala sijui huko makambako!! But First time naingia KAHAMA pale mwanzoni tu naona kile kiwanja Cha ndege karibu na mgodi then yakafata minengo haswaa ya raia kusema kweli Nilihisi naingia Mkoani na sio Wilayani kabisa!!

Kila mji una Fursa zake na ndio zinazofanya paonekane Bora kwa kundi flan la watu wanaoishi Hapo Kama kahama madini, mpunga shughuli za uchuuzi ndio zinaibeba usilazimishe nawao wapasue sijui mbao Mara wasafirishe parachichi na vitu Kama hivyo!!

Japo sapajui njombe Wala huko sijui Tunduma na asili ya mtu ni kuvutia upande wake mimi hata unieleze Nini KAHAMA naona ndio the best na Sizani Hapa TANZANIA kuna Wilaya iliyombali kidogo na makao makuu ya Mkoa iliyojengeka na yenye hadhi ya kimkoa Kama KAHAMA sizani
 
Ungefika kote kwanza ndio ungepata ulinganisho ulio fair but hiyo Kahama bila shaka imeendelea kushinda huko lalago ,Hungumalwa au mwigumbi ulipotoka [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Hata hivyo tunalinganisha Njombe Mji na Kahama Mji (Manispaa uchwara) na sio Mkoa wa Njombe as a whole

Karibu Sana Njombe hutojuta hii ni nchi ya ahadi iliko bustani ya Mungu
 
Nadhan unapafahamu Katoro, panapishana kidogo sana na Geita mjini na hata Kahama
 
Kahama kwamujibu wa taarifa za mpango kabambe (Master plan) iliyoandaliwa kahama imekuwa along Rwanda-Isaka Highway kwa km 13 kupelekea Isaka na kilomita 10 kuelekea Rwanda. Pia imekuwa kwa upande wa kuelekea tabora kwa kilomita 5 na kuelekea Mwanza(Mhongolo) kwa kilomita 8

Unless utaniambia kahama watu wanakata mashambani there is no way kahama itakuwa na housing unit chache kuliko NJOMBE huku ikiwa na idadi ya watu mara mbili ya NJOMBE!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…