Hili gazeti limejaa mahaba zaidi kuliko uhalisia,Kama miji hiyo Ina sifa unazozitaja kwa nini hakuna hotel kali na nyingi si unadai Kuna pesa huko?
Mkuu hiyo miji umeitaja ndio sampuli ya Kahama yaani imejaa wachuuzi Kama gulioni,mambo ya idadi ya sheli sijui nini sio kigezo,,kwa mfano tufanye Makambako ina vituo vingi vya mafuta(sheli) kuliko Sumbawanga sasa nijibu je Makambako au Tunduma inaizidi Sumbawanga kwa kipi? Usilinganishe miji ya Njombe na Mafinga yenye Uchumi stable na ya wastaarabu Kama hayo magulio yakiongizwa na Kahama
Miji inajengwa kulingana na jiografia ya mji ulipo kwa mfano Mafinga inaambaa kulingana na barabara kuu,Njombe inajengwa kufuata barabara kubwa zote Ila huoni kwa sababu jiografia yake ni mabonde na milima na iko covered na uoto wa miti tofauti na Makambako ambayo ni tambarare na imejaa kipara,typical uchuuzi towns
Kahama Unaifahamu!? Au unaisikia!?
Kahama ina makadirio ya Watu laki 300+
Kahama imegeuka kuwa kitovu cha uzalishaji ambapo viwanda vinaendelea kujengwa kila uchwao
Kinaendelea kutengeneza formal jobs kueleka kuwa manispaa
Kumeendelea kuwa kitovu cha biashara za ndani na nje ya nchi.. ambapo wafanya biashara wa Kahama na wengi wa kariakoo wamesogea Kahama kuhudumia soko la kimataifa (Rwanda Burundi na Congo)
Uzalishaji umeendelea kukua huku Kahama ikiwa mzalishaji mkubwa zaidi wa mchele nchini for the past 5years.. na the largest exporter pia.
Soko la huduma Kahama huwezi linganisha na vijiji unavyovitaja.. Kahama inapokea usafiri wa anga mara mbili kwa week, na hii ni kutokana na kukosekana muundombinu bora na watoa huduma wa uhakika... Kuna Maagent wa TKT za Ndege zaidi ya 15 na wanafanya kazi kila siku na mara nyingi watu wanakuwa shuttled to Mwanza kwa huduma hii (shows you people are affluent and can spend)
Shule za Standard ya kitaifa na kimataifa ziko kila kona, (Elimu) vyuo vya upili vya serikali na binafsi, Na sasa Makampuni ya Game and Tours yameanza kujipenyeza kuona kama yanaweza kuset kambi kwa wanaohitaji kufanya uwindaji..
Construction businesses and makampuni ya wazawa kibao yameanzishwa headquartered Kahama ambayo yana parangana kupata regional recognition... Magarage makubwa yanayoservice mpaka Rwanda na Burundi.. na maengineer wengine wengi wameanza tayari ujenzi wa viwanda vidogo vya ndani vya fabrication ya vifaa vya kilimo.
Kahama its waaaaaay ahead of njox na Kagongwa labda ndio uiweke na Mafinga.
Sent from my Infinix X650 using
JamiiForums mobile app