Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

Swax Mc
Screenshot_20240708-190412.png
 
MOJA YA ENEO LENYE KASI YA ONGEZEKO LA WATU MAJI YALIKUWA NI KERO KUBWA SASA NAONA PROGRAM YAO WAMEUNGANISHA MBARALI ,MAKAMBAKO NA WANGINGOMBE NJOMBE DC NA MUFINDI KUSIN HUKU TAYARI WALISHA PATA MAJI HILI ENEO KUTOKANA NA KUWA TAMBALALE ENEO KUBWA UKIJUMLISHA IDADA YA WATU KATIKA MAJIMBO HAYA MATANO WAPO ZAIDI YA MILIONI MOJA NA KWA UTEKELEZAJI WA PROGRAM HII BASI ENEO HILI LOTE MAKAZI YANAENDA KUUNGANA MAANA NDO ILIKUWA SHIDA KUBWA KWA WAWEKEZAJI 👇👇👇👇👇👇👇Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kanali Denis Filangali Mwila siku ya leo Julai 10, 2024, imefanya ziara ya kutembelea mradi wa Maji unaotekelezwa katika Mji wa Rujewa ikiwa ni moja ya miradi inayotekelezwa katika Miji 28 Tanzania bara na Mbarali ikiwa ni miongoni mwa wanaufaika wa program hiyo katika Mji wa Rujewa, kata ya Lugelele.

Mradi huo unaogharimu kiasi cha Dola Milion 20,379,000.58 ambazo sawa na Shilingi 50, 927,124,011.00. Mradi unatajia kuzalisha maji kiasi cha lita za ujazo 41,000,000 kwa siku. Hata hivyo Eng. Lestus Linda ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Rujewa (RUJUWASA) amesema mradi huo unategema kunufaisha Mji wa Rujewa, Kata ya Ubaruku, Imalilo-songwe na Igava. Pia Mji wa Wanging'ombe na Makambako ni miongoni mwa wanaufaika wa program hiyo.

Mradi huo unatekelezwa kupitia Mkandarasi M/S Larsen and Toubro Kampuni ya India chini ya Mshauri WAPCOS wa India. Mradi unategemea kukamilika mwaka 2025 ikiwa ni muda wa awali wa mkataba. Mradi huu ni kazi kubwa anayoendelea kuifanya Raisi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuhakikisha changamoto za maji zinapungua kwa kiasi kikubwa.

#NasimamanaRaisimheshimiwaDaktSamiaSuluhuHassan
1720751198451.jpg
1720751221530.jpg
1720751209126-jpg.3039935
 

Attachments

  • 1720751209126.jpg
    1720751209126.jpg
    193.8 KB · Views: 10
KAZI YA KUUPANGA MJI WA MAKAMBAKO KIVIWANDA NA BIASHARA INAENDELEA WANAENDELEA KUKUTANA NA WADAU MBALIMBALI 👇👇👇👇👇Mashine za kusaga sembe kuhamishiwa idofi na Majengo,Siku saba zatolewa kwa wafanyabiashara wa mazao walio nje ya soko kuu Makambako kurejea Soko la Mazao Kiumba, Viazi kushushwa soko la Magegele na Matunda soko la Maguvani kuanzia leo.

Na. Lina Sanga

Uongozi wa Halmashauri ya Mji Makambako umetoa wito kwa wamiliki wa mashine za kusaga sembe, kununua viwanja vilivyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya viwanda vidogo eneo la majengo na Idofi,ili kuanza ujenzi kabla ya agizo la kuhama halijatolewa.

Mhe. Hanana Mfikwa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako amesema kuwa, kama walivyohamishwa wenye mashine za kukoboa mpunga muda wa kuhamisha mashine za kusaga sembe pia utafika, hivyo ni wakati sasa kwa wamiliki wa mashine za kusaga sembe kununua viwanja mahususi kwa ajili ya viwanja vilivyotengwa na Halmashauri.

Ametoa wito kwa wamiliki wa mashine hizo kufika katika ofisi ya mkurugenzi ili wapewe maeneo kwa ajili ya ujenzi wa mashine za kusaga sembe na wakabidhiwe hati baada ya kukamilisha malipo , lakini pia Halmashauri itatenga eneo kwa ajili ya kiwanda cha kuzalisha sembe katika eneo la Kiumba ili mtu akinunua mahindi asage sembe papo hapo.

Ametoa rai kwa wafanyabiashara wa mazao wote walio nje ya soko kuu kuhamisha mazao yote soko la kiumba ndani ya siku saba kuanzia leo julai 15,2024 na magari ya mizigo ya viazi kuanza kushusha viazi katika soko la Magegele na Matunda katika soko la Maguvani zaidi ya hapo mfanyabiashara au dereva wa gari litalokamatwa atalazimika kulipa faini isiyopungua Mil. 1.

Leo julai 15,2024 kimefanyika kikao cha timu ya menejimenti na wafanyabiashara wajenzi wa maghala na vizimba katika soko la mazao la Kiumba,kukubaliana muda wa kurejea sokoni ambapo siku saba zimetolewa kwa wafanyabiashara hao kurejea soko rasmi la mazao la Kiumba,magari ya mizigo ya viazi kuanza kushusha viazi soko la Magegele na magari ya mizigo ya matunda kushusha matunda katika soko la Maguvani.
1721055100702.jpg
 
🔥🔥
 

Attachments

  • 0a43ff94e1194a31bdee7a7143f0ad60.jpg
    0a43ff94e1194a31bdee7a7143f0ad60.jpg
    60.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom