Kahawa ya Tanzania kukuza ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Italia

Kahawa ya Tanzania kukuza ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Italia

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Kahawa ya Tanzania kukuza ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Italia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameshiriki katika Mdahalo wa Wadau wa kukuza mnyororo wa thamani wa kahawa inayozalishwa barani Afrika uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa Mpango wa Mattei kwa Afrika na Lango la Kimataifa (The Mattei Plan for Africa and the Global Gateway) uliofanyika jijini Roma, Italia.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali ya Italia, Umoja wa Ulaya, kampuni kubwa za kahawa zikiwemo Illy na Lavazza, taasisi za fedha kama IFC na Chedepe, na wawakilishi kutoka FAO na IFAD.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mhe. Waziri Kombo ametoa wito kwa wadau hao kuongeza uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa zao la kawaha barani. “Kukiwa na ustawi barani Afrika, tunaweza kutatua changamoto za hali ya hewa kwani misitu mikubwa barani Afrika inatumika kama nyenzo muhimu ya kunyonya kaboni na kwamba kuongezeka kwa uzalishaji wa kahawa kunaweza kuongeza nguvu katika kulinda mazingira lakini pia kutengeneza fursa za ajira kwa vijana.”

Mhe. Kombo alieleza mazingira rafiki ya uwekezaji katika zao la kahawa nchini, na kuwakaribisha wadau kuwekeza katika uzalishaji na uongezaji thamani wa zao linalopatikana kwa wingi nchini hali itayosaidia kuinua kipato cha wakulima. “Lavazza na Illy kila mara mnaongelea punje ya kahawa kwenda kinywaji, hamzungumzii kutoka ardhini hadi kuwa punje kwani usipokuwa na punje hakuna Lavazza hakuna Illy.

“Msiwe wanasiasa. Tuweke mpango kazi, tuweke ratiba ya utekelezaji. Tuweke ratiba ya ukamilishaji. Na hili linaweza kufanyika,” amesisitiza Mhe. Kombo.

Aidha, Katibu Mtendaji wa Shirika la Kahawa la InterAfrican, Solomon Rutega ameipongeza Tanzania kwa kufanikisha Mkutano wa Kahawa wa G25 ambao maazimio yake ya kuliongezea thamani zao la kahama kuanzia kwenye kilimo, uchakataji, uokaji wa mbegu hadi kumfikia mtumiaji wa mwisho vinalandana na maazimio ya ushirikiano wa Italia na Afrika katika zao la kahawa.
 

Attachments

  • IMG-20250328-WA0089.jpg
    IMG-20250328-WA0089.jpg
    27.5 KB · Views: 43
  • IMG-20250328-WA0096.jpg
    IMG-20250328-WA0096.jpg
    443 KB · Views: 35
  • IMG-20250328-WA0093.jpg
    IMG-20250328-WA0093.jpg
    408.2 KB · Views: 41
  • IMG-20250328-WA0092.jpg
    IMG-20250328-WA0092.jpg
    265.6 KB · Views: 36
  • IMG-20250328-WA0120.jpg
    IMG-20250328-WA0120.jpg
    480.9 KB · Views: 41
  • IMG-20250328-WA0109.jpg
    IMG-20250328-WA0109.jpg
    339.2 KB · Views: 39
  • IMG-20250328-WA0103.jpg
    IMG-20250328-WA0103.jpg
    213 KB · Views: 39
  • IMG-20250328-WA0101.jpg
    IMG-20250328-WA0101.jpg
    313.1 KB · Views: 40
  • IMG-20250328-WA0099.jpg
    IMG-20250328-WA0099.jpg
    314.7 KB · Views: 35
  • IMG-20250328-WA0110.jpg
    IMG-20250328-WA0110.jpg
    407.9 KB · Views: 32
  • IMG-20250328-WA0104.jpg
    IMG-20250328-WA0104.jpg
    198.9 KB · Views: 35
  • IMG-20250328-WA0105.jpg
    IMG-20250328-WA0105.jpg
    278.8 KB · Views: 34
  • IMG-20250328-WA0115.jpg
    IMG-20250328-WA0115.jpg
    376.3 KB · Views: 35
  • IMG-20250328-WA0114.jpg
    IMG-20250328-WA0114.jpg
    435 KB · Views: 35
  • IMG-20250328-WA0119.jpg
    IMG-20250328-WA0119.jpg
    293.6 KB · Views: 37
  • IMG-20250328-WA0112.jpg
    IMG-20250328-WA0112.jpg
    444.7 KB · Views: 38
  • IMG-20250328-WA0118.jpg
    IMG-20250328-WA0118.jpg
    418.9 KB · Views: 34
Ushirikiano wowote unaofanywa kati ya nchi za Afrika na nchi za Ulaya beneficiaries ni nchi za Ulaya, hao watu wangekua wanatuthamini tungekua hata na 1/3 ya uchumi wao. Lkn my friend, eg eti tuna mahusiano mazuri na Japan na wanatupa misaada, kiini macho na danganya toto, Leo tanzania ndio tunapata terni ya umeme, Japan wanakitu wanaita Bullet train my friend, wale wakija kwetu wanatuchora tu hawana chochote cha kutusaidia zaidi ya kutafuta masoko yao, Nawaza tu I we independent kweli au naota tu

BIG UP IBTRAHIM TRAORE FOR WHAT YOU ARE DOING, najua kutoka na njaa za viongozi wa Africa asilimia kiduchu watamsupport Traore lkn Dogo ni mwamba na anajikubali kwamba yeye ni pure African na tukiamua kwa pamoja tunaweza
 
Back
Top Bottom