KERO Kaimu Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Mugundu ni tatizo, mamlaka ziingilie kati

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naandika hii kwa masikitiko sana kwani tangu tumekuwa tukiripoti yanayojiri shule ya msingi Mugundu ilioko wilaya ya Iramba kata ya Kyengege mkoani Singida hakuna hatua yoyote inayochukuliwa

Narudia tena kusema huyu Kaimu Mwl Mkuu amekuwa tatizo kubwa hapa, tunaomba mamlaka husika zifike shuleni ikiwezekana zifanye kikao na wazazi ili wapate kujua vizuri kero za hapo shuleni.

Mwl huyu anathubutu kuwarudisha wanafunzi wa darasa la saba nyumbani wasipate masomo kwa ajili ya kufuata pesa ya mahafali na amefanya hivyo mara kwa mara sasa si atapelekea watoto kufeli!

Tunaomba mamlaka husika zitusaidie. Mimi ni mzazi wa mwanafunzi na mkazi wa Mugundu.

Asante
 
Kuna vitu vya kulalamikia na siyo huu upumbavu.Mnachangia milioni ngapi hayo mahafali?
 
Hela ya mahafali ni kiasi gani mpaka usimlipie mwanao? Suala dogo kama hili unafungua Uzi kweliiiiiiiiiii! Ungelipoti Kwa mamlaka husika lingeisha ila Kwa hili Nina mashaka na jinsia Yako.
Kwanini uliwahi kuzaa, unashindwa hata kumtolea mwanao pesa ya mahafali.
Huyuatakuwa wale wa misimamo mikali isiyo na tija. Wajuaji sana huko vijijini na wakwamisha maendeleo. Sidhani kama mwanao alikuwa anakula shule
Kuna vitu vya kulalamikia na siyo huu upumbavu.Mnachangia milioni ngapi hayo mahafali?
Hivi,mnakomenti tu au mmetulia na kutumia busara?Fedha ya mchango wa mahafali ndiyo watoto wapotezewe muda wa masomo?Nani anapaswa kutoa huo mchango?Mzazi au mtoto?Mwalimu ameshindwa kufanya mawasiliano na wazazi/walezi ili wabanwe na kuchangia?Kwa nini watoto waadhibiwe kwa shauri lisilo lao?Huo muda utafidiwa vipi ili kwenda na wakati na watoto wasome na kupata utulivu?
 
Darasa la saba wapo wa ngapi ns mchango wa mahafali ni kiasi gani?
NB. Kwa suala kama hilo mzazi unakuja lalamika mitandao hao watoto si watakuwa na pro nidhamu ya woga?. Amewasoma amewaingiza kwenye mfumo. Take action.
 
Naandika hii kwa masikitiko sana kwani tangu tumekuwa tukiripoti yanayojiri shule ya msingi Mugundu ilioko wilaya ya Iramba kata ya Kyengege mkoani Singida hakuna hatua yoyote inayochukuliwa

Narudia tena kusema huyu Kaimu Mwl Mkuu amekuwa tatizo kubwa hapa, tunaomba mamlaka husika zifike shuleni ikiwezekana zifanye kikao na wazazi ili wapate kujua vizuri kero za hapo shuleni.

Mwl huyu anathubutu kuwarudisha wanafunzi wa darasa la saba nyumbani wasipate masomo kwa ajili ya kufuata pesa ya mahafali na amefanya hivyo mara kwa mara sasa si atapelekea watoto kufeli!

Tunaomba mamlaka husika zitusaidie. Mimi ni mzazi wa mwanafunzi na mkazi wa Mugundu.

Asante
Wazazi timizeni wajibu wenu
 
Darasa la saba wapo wa ngapi ns mchango wa mahafali ni kiasi gani?
NB. Kwa suala kama hilo mzazi unakuja lalamika mitandao hao watoto si watakuwa na pro nidhamu ya woga?. Amewasoma amewaingiza kwenye mfumo. Take action.
Hali za watanzania wengi kiuchumi/kifedha ni chokambaya.Walimu hawapaswi kuwarudisha watoto nyumbani kufuata michango yoyote na waache kujifunza ambalo ndiyo lengo mahsusi.Na walimu walishakatazwa kuwafukuza,kuwarudisha au kutoa adhabu kwa changamoto zitokanazo na wazazi au walezi wao.Wanalijua hilo.Kwa nini wanakaidi?Wakiadhibiwa kinidhamu ndiyo wataelewa somo?Watafute namna ya kuwabana wazazi na walezi bila kuleta athari kwa wanafunzi.
 
Muanzisha Uzi ndugu GUEST ulishaleta Uzi humu mwezi Mei kuhusu mwalimu huyohuyo,nahisi mna visa vyenu binafsi pengine mmechukuliana Mwanamke
Iwe vyovyote vile,kama kweli huyo mwalimu ana tabia ya kuwarudisha watoto nyumbani wakati wa vipindi darasani anafanya makosa kiutendaji/kiutumishi.Aheshimu mamlaka zinazokataza usumbufu,adhabu zisizofaa na kujianzishia masuala yaliyo kinyume na miongozo ya kazi yake.That is insubordination!
 
Nyie, yaani kweli umeshindwa kumlipia mwanao hizo hela, kweli ataenda mbele?
 
Naomba hizo gharama za jumla za mahafali.
Nilipe tuendelee na mada nyingine zenye ulazima.
 
Hela ya mahafali ni kiasi gani mpaka usimlipie mwanao? Suala dogo kama hili unafungua Uzi kweliiiiiiiiiii! Ungelipoti Kwa mamlaka husika lingeisha ila Kwa hili Nina mashaka na jinsia Yako.
Mzee tulio ishi kijijini na maisha ya kijijini tunajua watu walikosa hata viatu nguo ikitoboka mnashona kwa mkono
 
Ila Walimu Kuna baadhi ya mambo hayapendezi japo hatupendi Muonewe, kwani Kuna ulazima wa Mwanafunzi kushiriki Sherehe ya Mahafali ikiwa hajaridhia?
Kama wamegoma kutoa hela achana nao, ghairisha zoezi pambana na mambo mengine yenye tija. Au Mwalimu ana maslahi binafsi na hiyo Sherehe?
 
Una uhakika gani kwamba mwalimu hakuwasiliana na wazazi unahisi yeye ni mjinga kiasi hicho
Hivi,mnakomenti tu au mmetulia na kutumia busara?Fedha ya mchango wa mahafali ndiyo watoto wapotezewe muda wa masomo?Nani anapaswa kutoa huo mchango?Mzazi au mtoto?Mwalimu ameshindwa kufanya mawasiliano na wazazi/walezi ili wabanwe na kuchangia?Kwa nini watoto waadhibiwe kwa shauri lisilo lao?Huo muda utafidiwa vipi ili kwenda na wakati na watoto wasome na kupata utulivu?
I
 
Una uhakika gani kwamba mwalimu hakuwasiliana na wazazi unahisi yeye ni mjinga kiasi hicho

I
Kuwasiliana na wazazi hakumpi mamlaka ya kutimua wanafunzi muda wa masomo wakafuate michango ambayo wazazi au walezi ndiyo wanawajibika kuitoa.Lengo mahsusi la wanafunzi kuwa shuleni ni kupata elimu/ujifunzaji na si hafla wala mahafali.Kwa nini wasiweke mipango ya uchangiaji kidogokidogo kwa muda mrefu/utakaotosha kulingana na hali zao?Miongozo ya kazi kiualimu inamuelekeza awatimue wanafunzi warudi nyumbani kufuata michango ya mahafali?
 
Back
Top Bottom