Tumechoka kufanywa Mangumbaru / Wajinga kila uchao juu ya Usajili hewa wa Niyonzima na Manula. Na hili bomu nililonalo ambalo wakifanya mzaha nitalilipua kweli waumbuke na waaibike nimelipata kutoka kwa wenzao hao hao waliopo katika Kamati za Utendaji na Usajili.
Kinachonipandisha hasira juu yao ni kwamba kwa muda wa wiki mbili kama siyo tatu nimekuwa nikiwananga / kuwatania sana wana Yanga sehemu mbalimbali kila ninapokutana nao kiasi kwamba hadi wengine wamekuwa wakiniona tu wananikimbia kwani wimbo wangu wa kuwaringishia umekuwa ni ujio wa Haruna Niyonzima na Aishi Manula sasa nawaza tu kama taarifa hii niliyoipata ni ya ukweli nitaficha wapi msura wangu huu?
Na hakuna Watu wanaojua kutania vibaya kama Wapenzi wa Yanga na kama kweli Niyonzima na Manula hawaji au hawajasajili Simba SC hakika nitawakoma!