GE2025 Kaiza: Hakuna mwana CHADEMA aliekuja Chaumma aliesema anarudi nyumbani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Agness Kaiza, leo tarehe 27 Agosti 2025 amerejesha fomu yake ya kugombea na kusema Tume ya Uchaguzi imeridhia kuwa anazo haki zote za kushiriki uchaguzi huo.

Akizungumza na wananchi wa Segerea, Kaiza aliahidi kuwatumikia kwa moyo na bila kuwaangusha, huku akiwaasa wananchi kuwa walinzi wa demokrasia kwa kulinda vitambulisho vyao vya kupigia kura akisema, “Vitambulisho vyenu vilindeni kama mboni za macho yenu.”

Aidha, alisisitiza mshikamano ndani ya chama chake kwa kueleza kuwa hakuna mwanachama aliyehama kutoka CHADEMA kwenda CHAUMA akajutia hatua hiyo, jambo linaloashiria kujiimarisha kwa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

GfF9ragacAAWv7q.jpeg
 
Back
Top Bottom