Kajala: Natamani kupatana na Wema

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
SIKU chache baada ya mtangazaji Penniel Mungilwa ' VJ Penny ' kupatana na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu , mwigizaji Kajala Masanja ' Kay' naye ameibuka na kuweka bayana kuwa hata yeye yupo radhi na anatamani kupatana na Wema ambaye wameogelea kwenye bifu miezi kadhaa sasa .

Kajala alifunguka hayo mara baada ya paparazi wetu kumuuliza kuhusiana na mtazamo wake juu ya Wema na Penny kupatana ndipo aliposema amefurahi mno na hata watu wengine watakuwa wamejifunza kitu kutokana na kupatana kwao.

Akizidi kushusha ' vesi ' mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi , Kajala alisema anaamini siku zote bifu zinarudisha nyuma maendeleo hivyo Wema kupatana na Penny ni jambo la busara kwani ni moja ya chachu ya kufanya mambo mengine yaendelee kwani hata yeye hapendezwi na mabifu . Wema Sepetu akipozi .

"Hata mimi natamani kupatana na Wema . Mabifu ni mambo ya kitoto sana, kwa kweli nimefurahi sana kuona Penny na Wema wamepatana kwani ni marafiki wa siku nyingi sana na wanastahili ifike sehemu vitu viishe na maisha yaendelee kama kawaida , " alisema Kajala .

Alipoulizwa Kajala kama kweli yupo tayari kupatana na Wema na uwezekano huo upo, Kajala alisema muda wowote wanaweza kukaa na kumaliza tofauti zao. "Hata mimi siku si nyingi tutaweka mambo sawa kwa sababu bifu hazijengi , hazina maana hata kidogo ni kufanya mambo yasiende mbele tu , inabidi tubadilike ," alisema Kajala .

Wema na Kajala walikuwa mashosti wa damu lakini mwaka jana mwishoni waligombana huku chanzo kikitajwa kuwa ni kugombea mwanaume ambaye alifahamika kwa jina la CK.
 
kuna wakati unafikiria kuwa wanajitambua na kusoma alama za nyakati wataitana na kukumbatiana hapo waungwana mtajua yamekwisha.Tatizo mmoja apate bwana mwenye pesa ohooo! kamati za usuluhishi lazima zitafutwe urafiki wao wa mashaka mashaka.
 
Wapatane tu maana ye aliingia kwenye mkenge wa Ck kumbe ye kamtumia kama chambo ya revenge kwa Wema. Ck kambwaga, shoga kageuka adui..
 
Anataka wapatane ili amchukulie tena bwana...
 
Anataka wapatane ili amchukulie tena bwana...

Mngejuaga siri ya Wema na mabwana na mashosti zake mngeongea tofauti....

Ndio maana wenyewe hata hawasemagi wazi ila wapambe sasa....
 
Kwani Kajala bado yuko na CK,au ilikuwa nafasi ya kumuumiza Wema kuwa ukisema cha nini wenzio wanawaza watakipata lini?
 
kuna wakati unafikiria kuwa wanajitambua na kusoma alama za nyakati wataitana na kukumbatiana hapo waungwana mtajua yamekwisha.Tatizo mmoja apate bwana mwenye pesa ohooo! kamati za usuluhishi lazima zitafutwe urafiki wao wa mashaka mashaka.

Dah, yan umeongea point sana mkuu
 
Wapatane tu maana ye aliingia kwenye mkenge wa Ck kumbe ye kamtumia kama chambo ya revenge kwa Wema. Ck kambwaga, shoga kageuka adui..

Mmh ila kajala anayaweza kujipendekeza gani uko, yan wanamuona mama ubaya kama mungu wao, watutolee nuksi apa
 
Mmh ila kajala anayaweza kujipendekeza gani uko, yan wanamuona mama ubaya kama mungu wao, watutolee nuksi apa

Labda wema anawawezesha kula wangekua wanapatana halaf kila mtu anakua kivyakee,,sasa hivi utasikia penny kagombana na wema, urafiki wa ukaribu ukaribu lazima mkosane haswa muwe wengi,,bora muwe wawili
 
Mmh ila kajala anayaweza kujipendekeza gani uko, yan wanamuona mama ubaya kama mungu wao, watutolee nuksi apa

Embu niambie binamu nasikia Kajala kafulia mbaya hata kodi inasumbua kweli? napenda umbea ila unanishinda itabidi unifundishe.
 
Embu niambie binamu nasikia Kajala kafulia mbaya hata kodi inasumbua kweli? napenda umbea ila unanishinda itabidi unifundishe.

We Zavi acha masihara lile ghorofa hajalipia mwaka mzima kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…