Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Na Shani Ramadhani na Mayasa Mariwata/Uwazi
MWANADADA anayefanya vizuri kunako soko la filamu za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay' ameweka wazi kuwa yuko tayari kugharamia sherehe ya harusi ya Manaiki Sanga na Jacqueline Wolper Massawe kama mambo yataenda sawa.
Akipiga stori na Uwazi, Kajala alisema kutokana na ukaribu alionao kwa watu hao basi mambo yote yanayohusiana na sherehe yatakuwa chini yake kwa maana ya gharama zote na kikubwa ni kuwaombea tu maana ni muda mrefu sana Manaiki alikuwa na ndoto za kumuoa Wolper.



