Kaka Magical power umeamkaje na familia yako.

Kaka Magical power umeamkaje na familia yako.

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Kaka Magical power umeamkaje na familia yako

Kaka naomba kuwaambia watu hasa wadada wenzangu wajifunze kukoment positive kuna faida kama kuna post unaona huwezi kuandika kitu achana nayo. Mimi ni mfuasi wako mzuri sana nipokufollow nikawa nasoma komenti za wanaume walioko humu wengi nikaona ni watu wanaojielewa sana nikasema moyoni nitapata mtu humu kwenye page yako. Nikawa nasoma komenti za wanaume nijue wana mtazamo gan

Basi nikapost picha mbili moja profile yangu na nyingine moja mpya kisha nikaunlock profile nikaanza kukoment kwenye post zenye kugusa watu wengi. Najua kuna watu kazi yao ni kusoma komenti na kuview profile za watu😀

Nikasema acha wasome komenti zangu na waview profile yangu na lazima nimpate mume wangu humu kwenye Uzi zako, Nikawa mtu hai kwenye Uzi zako ili wale wakaka wanaosoma komenti za watu na kuview profile tukutane mbele ya safari walikuja wengi ila kuna mmoja alikuja nikamuelewa si kwamba hao wengine walikuwa hawana sifa Ila namna walivyokuwa wanakuja inbox eti pande zipi mrembo, niaje, walikuwa wananitumia sms za kihuni nikawa nawapotezea wapo waliokuja na njia nzuri ila tulipoanza mawasiliano nikaona hamna mahala tutafika nikawaachilia ila sasa akaja mkaka mwenye AKILI zake timamu na upendo mkubwa ndio niko naye na mambo ni mazuri sana. Nilipompata tu huyu basi nimefuta picha zangu zitaki kero tena na waja maana niko kwenye mahusiano tayari 😀

Sijalock profile ila nimefuta picha, picha zilikuwa na lengo maalum limetimia na Sasa nipo kujifunza tu kwenye ukurasa wako hitaji langu nimeshalipata najifunza kuongeza vitu

Ubarikiwe kwa kuanzisha Uzi hizi nimepata kitu kizuri cha thamani mkaka fulani hivi anajua kupenda na anajielewa vibaya mno.
 
Back
Top Bottom