Kisaikolojia sawa, mapenzi lazima saikolojia nayo ihusishwe hata kama sio kaka na dada wa tumbo moja. Jembe halinoleki kuwa tayari kulimia shambani mpaka kwanza psychology ipande. Hata binti awe mzuri vipi, psychology yako isipoumuka jembe haliwi ngangari. Ukipuza tu, hamna kazi siku hiyo. Hata dada naye asiponyenyua psychology yake juu yako mambo hayaendi, na kama unalazimisha utaumia wewe na yeye pia, maana mwili unakubali kuifanya kazi hiyo kwa amri kutoka upstairs.
Nilishaipata story nyingine ya mama kutoa kwa mtoto wake wa kumzaa, pia baba kibao walioonja mboga za shambani mwao kabla ya kuziuza. Sasa sikilizia kijana anapojitokeza kuchukuwa hati miliki, mzee hakubali. Mzee anakuwa mbogo na anawka masharti kemkem ili vijana washindwe naye aendelee na kitumbwike chake.
Sio vema sana kuachia ukaribu wa kupita kiasi kwa opposite gender. Kuna binti mmoja Jijini Mbeya alikuwa anasoma day school moja akikaa kwenye nyumba ya baba yake lakini wazazi walikuwa wanaishi kijijini, walikuwa wamepangisha nyumba mjini ili kujipatia chochote. Mtoto wa kaka yake mwenye binti naye alipata nafasi mahali pengine, lakini kwa sababu fulani ilibidi ahamie shule ile ile anayosoma dada yake, sababu mojawapo kuchagua shule ile ni hamasa ya baba zao mtu na mdogo wake, kwamba kwa kuwa mdogo alikuwa na nyumba mjini na tena binti anasoma shule ileile darasa moja, ingekuwa vizuri wakakae pamoja mtu na dadake wasome pamoja discussions na kupunguza gharama za maisha mjini. Kwa hiyo mmoja akienda kijijini alibeba vyakula kwa ajili ya wawili, lakini kila mmoja alikuwa anakaa chumba chake.
Mwanzoni iliwasaidia sana, maana walikuwa wanakutana chumbaa kimojawapo wanadiscuss sana hadi usiku wa manane, shule ikapanda sawia. Lakini mmoja akichoka anajinyoosha kidogo kupata nguvu, wakati mwenzake anaendelea kutafuta majibu au anafanya shughuli nyingine. Ikafika wakati wanachoka kiasi kwamba wanasoma hadi saa tisa usiku, wanataka wapumzike kidogo halafu wajiandae kwenda shule, hivyo wanaamua kujinyoosha chumba kimoja. Awali mmoja kwenye kiti mwingine kitandani, lakini walijikuta wako karibu kiasi kwamba hawaoneani aibu tena, wakaanza kuamua wakasomee chumba chochote na ni mpaka asubuhi. Ni binadamu hao, you know what came to happen in no time, wakajinyoosha pamoja kitanda kimoja na baadaye wakajifunika shuka moja na baadaye hata bila kuombana wakajitengenezea mikasi. Hapo ndipo aibu zilipoanza kujongea lakini too late, binti akaanza kutema mate hovyo na juhudi ya masomo ikashuka kwa kasi.
Watu wa jinsia tofauti wakiwa karibu sana katika mambo yao lazima utegemee hayo kutokea, kwa sababu mikasi haiangalii undugu wenu, madhali zana za kukokotoleana zipo, kinachosalia ni muda muafaka.
Hapohapo Mbeya, mwaka 2000 kuna kaka mmoja wa kisukuma alikuwa na biashara zake, akakutana na dada mwingine wa kisukuma na chemistry ikakubali nao wakaanza kulishana chips mayai na mikasi kama kawa. Binti alikuwa anashona. Baada ya miaka miwili wakakubaliana waoane maana sasa wameshajuana vya kutosha. Wakiwa wanajiandaa kwenda usukumani kujitambulisha, mama wa binti alikuja kumtembelea bintiye, naye binti hakuchelewa kumdokeza ili mama asishituke akiona mgeni wa kiume kuja pale kwake.
Kwa bahati, kijana akiwa mitaani akakutana na mama yake binti, kumbe wao walikuwa wanajuana, kijana ni mtoto wa dada yake KABISA yule mama. Walijuana kutokana na kutembeleana kina mama lakini watoto walikuwa hawajuani.Kila mtu akimshangaa mwenzake, wakapanga namna ya kukutana. Mama akamwambia kijana kwamba dadako yupo hapa ni vema mfahamiane. kesho yake kijana akaenda na chips anakoshona dada yule, kumbe binti alikuwa amekwenda hapo na mama yake ili wapelekane sokoni.
Kijana alipoingia tu akamwona mama mdogo, wakawawiana, mama akasema dada yako huyo hapo, kumbe unakuja hata hapa na hamjuani? Tayari binti na kijana wakanyong'onyea wakisaidiana na washonaji wengine wanaofahamu kinachoendelea kati ya kijana na binti!! Sikufuatilia zaidi kilichojiri baadaye.
Kwa hiyo, psychology sawa, wazazi labda, lakini chyemistry ndiyo zaidi baada ya kupata mazingira yanayoruhusu reaction ya chemicals mbili hizo tofauti regardless of origin. Bahati mbaya binadamu tuko too more sensitive kuliko viumbe wengine ambao hata mjukuu ni chakula halali kwao.