Kaka ni "Hensamu" lakini ni mchoyo!

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Salamu sana wapendwa wangu.

Kuna kaka nimemuona leo ofisi fulani ya umma, ni mzuri tena anaonekana ni "mtamu" kutia naye story. Wakati nimesimama zangu kwenye hiyo ofisi nasubiria huduma, huyo kaka aliombwa SANITAIZA na mwenzie kwa kuwa yule mwenzake alikuwa kamaliza ya kwake. Utaratibu wa hiyo ofisi kila staff ana sanitaiza yake, sasa sijui kama wamenunuliwa na ofisi au wanajinunulia wenyewe.

Sikuamini macho yangu yule kaka "mzuri" alimnyima kata kata mwenzie. Nikajiuliza maswali mie mwenyewe kichwani, hivi sasa anavyomnyima huyo na wamekaa desks jirani haoni kwamba huyo akipata korona hata yeye ana hatari ya kuambikizwa. Nilidhani anatania lakini, alimfungia vioo mwanzo mwisho.

Kumbe wenyeji na wazaliwa wa mkoa uleee wanavyowasema ni wachoyo, wabinafsi, but waroho wa kupenda vya wenzao kuna ukweli ndani yake.


Yooooo! Iwe booojoooo kaziroooooo.

Ahsanteni, nawatakia Jumatatu njema.
 
navyokujua Nak,ulishalowa tayari..🏃‍♂️tulia nyumbani,corona ni hatari
Sasa nikikaa nyumbani nitakula nini, riziki iko miguuni mwangu. Yaani nawaza siku wakisema lokidauni sijui nitakuwa mgeni wa nani!
 
Kwa taarifa yako unayeniongelea ni mimi na nilimnyima huyu jamaa kwa kuwa ya kwake alihonga halafu anajisifu atatumia za kwetu. Mie sio mchoyo kama unavyodhani halafu niliona unavyoniangalia kwa jicho la tamaa sema nilikupotezea niliona haulipi, mie sipendi mademu wenye komwe na wanaotumia mkorogo . Halafu ukija ofisi za watu uwe unavaa barakoa siku nyingine hatutakuhudumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…