Kaka pamoja na kwamba umeamriwa kupenda ila hakikisha unayempenda naye anakuelewa kuna utii, baraka na matendo mema utayapata

Kaka pamoja na kwamba umeamriwa kupenda ila hakikisha unayempenda naye anakuelewa kuna utii, baraka na matendo mema utayapata

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Kaka pamoja na kwamba umeamriwa kupenda ila hakikisha unayempenda naye anakuelewa kuna utii, baraka na matendo mema utayapata

Mwanamke akupenda kuna upendo utaupata, atakusaidia na atasimama na wewe kwenye changamoto zako. Mwanamke akikupenda hata kama atakuwa na mzuri wa muonekano au atakuwa na kipato kikubwa kuliko wewe hatakunyanyasa kwa uzuri wake au mafanikio hayo aliyonayo kwenye maisha yake aliyojaliwa

Mwanamke akikupenda hana ubinafsi kabisa atakusaidia, atakuthamini na kukutii bila kujali anakuzidi nini. Kaka ukimpenda wewe tu yeye asikupende utateseka sana kwenye mahusiano hayo ila ukiwa na mwanamke anayekuelewa utafurahia haya maisha sana na hutoyajutia

Mwanamke akikupenda hana ubinafsi huwa mtoaji na mtu wa kutumia vitu vyake kwa ajili ya familia au mwanaume ampendaye kwa dhati

Wanaume wanaoenjoy maisha ya mahusiano ni wale waliowapata wanawake wawapendao

Kaka mwanamke akikupenda umeula, utafaidi vingi vizuri na vitamu ambavyo bila kukupenda usingevipata, omba sana mwanamke uliyenaye akupende kaka utaenjoy sana haya maisha .
 
Back
Top Bottom