Historia inatoa taswira ya tofauti kabisa kuhusu hii hoja. Watu wa DINI ndiyo wanaoongoza kwa kuwa na mikono yenye damu za maelfu kama siyo mamilioni ya raia wasio na hatia. Tangu kuanzishwa kwa dola la kwanza la Kiislamu (The Rashidun Caliphate) mnamo karne ya 7, hakuna amani yoyote ile ambayo ililetwa kwa watu ambao siyo waislamu.
Nabii wa waislamu, Mtume Muhammad alipigana vita zisizopungua tisini kwenye miaka yake ya mwisho ili kuweza kuunganisha ghuba nzima ya Uajemi (The Persian Gulf) kama dola moja la kiislamu. Warithi wake Khalifa Ab Bakr na Umar walianzisha vita dhidi ya madola kama Uajemi (The Sassanian Empire) na Rumi (The Eastern Roman Empire), kama mbinu za kupata ardhi na kueneza uislamu.
Wale waliovamiwa na majemedari wa vita wa kiislamu kama
Al-Qaqa-Bin-Amar,
Khalid Ibn Walid,
Amar Ibn Alas,
Ubadah n.k walipewa haya masharti magumu matatu. Mosi, jiunge na Uislamu (Convert to Islam), Pili, lipa Kodi (Pay the Jizya), na tatu, Uuawe (Death). Mnaposema Uislamu ni dini ya amani mnataka kutuambia nini labda: Hivi unadhani waislamu waliweza kutengeneza dola kubwa ambalo limeanzia kwenye mipaka ya Uchina (Tang China) hadi kufika Uhispania (Spain) kwa kuimba Kaswida na kutafuna tende ? Majambia, Mikuki, Damu na Farasi vilitumika.
Ukija kwa WAYAHUDI ndiyo usiseme, ukisoma BIBLIA unaweza ukaogopa. Hawa Torati yao inaruhusu kabisa kuua mtu kama sehemu ya Ibada. Hata BWANA YESU pamoja na mitume wake wa kanisa la kwanza hakuuwawa na wapagani, bali WAYAHUDI ambao ni wafia dini.
Mtume Paulo alikuwa ni mmoja ya wauaji wakubwa wa kiyahudi kuwahi kutokea mnamo karne ya kwanza.
Ukitaka uthibitisho wa hili, nenda kajaribu kushindana na WAZAYUNI waliotokea Ulaya ndiyo utaona. Waarabu na ukichaa wao wote, walijaribu na walichokipata hawaamini mpaka leo hii. Yule ndugu yetu muimba muziki anayejiita "YE" walimfirishi Trilioni mbili na ndani ya usiku mmoja kisa aliwakosoa. Hapa kuna amani gani bwana wewe ?
WAKRISTO, hasa wale wenye macho ya bluu na wavaa rozari ndiyo wanaogopesha zaidi. Zingatia haya matukio waliowahi kuyafanya kwenye historia :
- Theodosius Pogroms of Jews and Non-Christians.
- The Urbanite Crusades in the Holy Land.
- The Sacking of Constantinople by Crusaders.
- The Spanish Inquisition.
- The Massacre of Huguenots.
Wale wengine wanaojiita WAPROTESTANTI na WALOKOLE hawako nyuma kabisa. Mambo waliyoyafanya kwa binadamu wenzao wenye ngozi nyeusi na nyekundu kule Marekani nadhani, mtu yoyote muungwana akiyafahamu lazima atazitazama hizi dini kwa jicho la kitofauti sana.
NB: Kiufupi watu wenye dini ni hatari mno kwa usalama na ustawi wa dunia.....