MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Mkuu nashukuru sana, na naomba nijibu hoja zako kama ifuatavyo.Huwa mkuu sipendi kubishana mambo ya dini ila kwa heshima yako naomba nikujibu hili, baada ya mtume kuanzisha dola ya kiisilamu, ni waisilamu waliowatetea wayahudi na kuwaweka kwenye himaya yao, golden age ya waisilamu ni golden age ya wayahudi pia, wayahudi walishika nafasi mbalimbali kwenye hizi dola mpaka Salahudin anapigana vita vyote physician wake ni myahudi ambaye mpaka leo wayahudi wengi wanamuona kama best scholar wa middle age alikua akiitwa Maimon ama jina jengine Rambam
Mosi, unachokifanya wewe tunaita kuchagua historia unayoona inaunga mkono hoja zako (Cherry Picking of history). Usiyoyakubali unayaweka pembeni. Katika somo la historia haya ni makosa makubwa.
Umetoa mifano miwili mikubwa kutetea Uislamu: Umezungumzia dola la Abbas (The Abbasid Caliphate) ambalo ndilo lilileta kipindi cha Neema kwa Uislamu (The Islamic Golden Age). Ukazungumzia tena kipindi cha Salahudin ambacho Wakristo na Wayahudi waliheshimika sana. Umenena vyema kabisa lakini umetupilia ukweli muhimu nje. Sifahamu lengo hasa la wewe kufanya hivi.
Huwezi kuzungumzia kipindi cha NEEMA (The Golden Age) bila kuzungumzia kipindi kilichokuwa kabla yake, kwasababu vipindi hivi vyote ndivyo vinaunda historia ya Uislamu. Umeliruka dola la Ummay (The Ummayad Caliphate) ambalo ni sehemu ya muhimu kabisa kwenye utawala wa Uislamu. Nasema hivi kwasababu kipindi cha NEEMA kulikuwa na madola mengi ya Kiislamu yenye falsafa na siasa tofauti. Kulikuwa na The Abbasid Caliphate, The Fatimid Caliphate, The Seljuk Sultanate, Khwarazm Empire, The Nizari Empire nk.
Dola la Ummay chini ya Kalifa Hisham, ndiyo dola la mwisho kutawala Uislamu kama dola moja. Katika hoja yako ya kutetea Uislamu, hujayazungumzia mambo waliyoyafanya watawala wa kiislamu wa kipindi hiki dhidi ya raia wa majimbo ya Afrika hadi kupelekea dola la kiislamu kuvunjika na kuzaa madola mengine madogo. Mkuu hujazungumzia kabisa matukio kama THE RISE OF KARIJISM na THE GREAT BERBER/AMAZIGH REVOLT. Haya matukio ndiyo yanatupa taswira nzima kuhusu Uislamu.
Pili, Kuhusu dola la Rashidun (The Rashidun Caliphate), hujazingatia kwamba mtume pamoja na wakina Salman walichinja mamia ya mateka wa kivita wa Kiyahudi (Jewish Prisoners of war) baada ya kuwashinda kwenye vita vya shimoni (Battle of the Trench). Waislamu wengi huwa wanapenda kuleta hoja ya kusema kwamba Mtume alikataza kabisa mateka wa vita wasiguswe, wala mnyama, wala mti na kwamba waislamu ndiyo waliwatetea Wayahudi, ilhali mnasahau jambo la msingi kabisa kwamba Mtume alifanya mauaji makubwa ya mateka wa vita ambao tayari walikuwa wamekubali kuweka silaha chini kule BANU QURAYZA. Hapa ntaomba nieleweshwe zaidi labda kuna kitu sikuelewi vizuri.
Mkuu wangu unachanganya mambo, Mtume amefariki mwaka 632 na uvamizi wa Misri umeanza kufanyika mwaka 639 chini ya Kalifa wa pili, Umar. Hivyo kusema kwamba Mtume aliwahi kushirikiana na Wakristo katika kukomboa Misri, nadhani siyo sahihi sana. Kubwa zaidi ambalo unalisahau ni hili: Misri imekuwa jimbo la Rumi tokea mwaka 30 BC kipindi wanatawala Wagiriki, lakini pia Misri ilijaa Wakristo. Unaposema kwamba Wakristo wa Misri walishirikiana na Waislamu katika kuvamia Misri napata ukakasi sana kwasababu hilo sijalisoma. Ntashukuru kama utanipa mfano wa hao Wakristo ili na mimi nijifunze.Si wayahudi tu Mtume na dola ya kiisilamu ilisaidiana na wakristo kukomboa maeneo yao, mfano mzuri kabisa ni Egpty ambayo ilikuwa ikitawaliwa na Byzantine (Roman), na waisilamu kushirikiana na wakristo kuwatoa.
Binafsi ninachofahamu ni kwamba hata uvamizi wa Misri haukuruhusiwa na Kalifa Umar, Jemedari wake mdogo Amar Bin Alas (The Conqueror of Egypt) alifanya kinyume na matakwa ya Kalifa. Historia inaonyesha kwamba baada ya Battle of Yormuk kule Syria na Siege of Jerusalem , Kalifa Umar hakupenda kabisa kujitanua ndiyo maana barua ya kwanza kabisa ya Amar kuvamia aliikataa.
Mkuu mimi nimesomea masomo ya vita, lakini pia Mungu alinipa kudra ya kufanya kazi na hizi mahakama za kimataifa. Kiufupi, vita ina dhana kuu mbili tu, ambazo kilatini zinaiitwa (Jus Ad Bellum) na (Jus In Bello). Ninapozungumzia Jus Ad Bellum naangalia zaidi sababu za kisiasa na kijamii zilizosababisha vita baina ya makundi mawili, au Political reasons for recourse to war. Hapa naangalia sababu kama kujilinda (Self-Defense) kama ulivyosema hapo awali, kusaidia wanyonge (Humanitarian Intervention) au kupambana na ukoloni (Self-Determination) kama ambavyo Tanzania ilifanya na mifano ukatoa.Again mkuu unadanganya ama hujaandika crucial part ya hivi vita, mtume alipigana hivi vita ama alipigwa na kujidefend mpaka kuwatoa hao wavamizi?
Unapokuja kwenye Jus In Bello hapa tunazungumzia, mbinu na silaha za vita (Means and Methods of Warfare). Hapa tunaangalia vita tu, bila kuweka sababu za kisiasa. Mambo ya msingi kama The Principle of Military Necessity, Military Proportionality, Protection of Civilians and Their Properties na mengineyo mengi.
Sasa narudi kwenye hoja yako ya msingi ya MTUME ALIKUWA ANAJILINDA: Hapa Mtume alikuwa na haki zote za kujilinda kama binadamu wengine (Jus Ad Bellum), hivyo hapa sina la kusema na kamwe siwezi kuwa mnafiki. Ambalo ninalo la kusema ni hili kuhusu mbinu (Jus In Bello) Kulikuwa na umuhimu gani wa kuwachinja wale Wayahudi ambao tayari walikuwa wameshaweka silaha zao chini kule Medina ?
Ndugu yangu, unaniita mimi muongo ilhali wewe unazungumza kitu ambacho hakipo kabisa kwenye historia. Mtume hajawahi kupambana na Warumi. Ila kuwekana sawa, ni dhahiri ufahamu hili kwamba kufika mwaka 212 AD Kaisari wa Roma Caracalla aliwagawia Uraia wa Rumi watu wote walioishi ndani ya dola la Mrumi. Tena kukupasha habari tu hili lilifanyika kwasababu Kaisari huyu wa Roma alikuwa ni mwafrika (Berber) kutoka Libya.Rumi walikuwa ni watawala wa kigeni ambao walikalia kimabavu maeneo yasiyo yao, mtume alipigana nao na kuwatoa kwa msaada mkubwa wa locals, vita vingi hivi vilipigwana hali ya kuwa waisilamu ni wachache sana dhidi ya mkoloni huyu wa zamani.
Lakini kukupasha zaidi habari, ni kwamba baada ya kila mtu kupewa Uraia wa Roma, miaka 32 baadaye baada ya Kaisari Caracalla, Dola la Roma lilikuwa na Kaisari Mwarabu aitwaye Filipo (Phillip The Arab). Hivyo Rumi kufika kipindi cha dola la Kiislamu, Rumi lilikuwa ni dola la Kikristo ambapo utumwa ulikuwa umefutwa kabisa. Hilo la kusema watu walionewa na kukaliwa kimabavu na Roma bado linanipa ukakasi.
Ndugu yangu, haya ndiyo madhara ya kuchagua historia (Cherry Picking History) kwasababu huwezi kupata taswira halisi. Kama nilivyosema hapo mwanzoni kabisa, usingeruka matukio muhimu kwenye historia ya Uislamu basi hii hoja isingetusumbua. Hebu turudi kwenye historia sasa: The Jizya haikuwa kodi nzuri hivyo kama unavyotaka kuipamba. Naomba nikupe sababu za kwanini nasema hivi:Nitajie nchi moja tu duniani ambayo unaweza ukaenda na usilipe kodi, jizya ni ndogo sana compare na tunacholipa sasa. Na hii sheria haimhusu mtu asie muisilamu tu hata muisilamu analipa zaka, pia Jizya iliwahusu wenye uwezo tu, Masikini, wazee,na wengine wasiojiweza hawakuwa wakilipa. Uki convert kwa hela za sasa matajiri walikuwa wakilipa around 1.5m, na wenye maisha ya kati around 100,000.
Mosi, Jizya ni kodi iliyowalenga MAKAFFIR peke yao na siyo WAISLAMU. Makaffir walitakiwa wafanye hivyo ili kulinda uhai na mali zao. Duniani kote kodi yoyote ambayo inalilenga kundi moja la watu ndani ya taifa ili kulinufaisha kundi moja dhidi ya jingine ni ya kinyonyaji. The Jizya haina utofauti na The Colonial Kipande System. Ndiyo maana watu wengi ili kukwepa Jizya walijifanya waislamu kitu ambacho kilipelekea dola la Ummay kukosa mapato na kuanza kuwatoza Jizya waislamu wa Afrika (Berbers).
Pili, kama Jizya ilikuwa ni nzuri kama unavyotanabaisha hapa, kwanini Waislamu wa Afrika waliigomea hadi kupambana vita baada ya kuambiwa walipe ? Nikupashe tena, mwaka 720 AD Kalifa Malik alimchagua Yazid Ibn Abi Muslim awe gavana wa jimbo la Afrika (Ifriqiya). Jambo la kwanza alilofanya Yazid baada ya kufika Afrika ni kutoza kodi ya Jizya kwa waislamu wakazi wa Afrika (Berbers) huku akiwaacha waarabu. Hili lilipelekea yeye kuuwawa kinyama na waislamu wenzake.
Baada ya haya matukio, ndiyo unafika hadi kwenye Vita ya Bagdoura mwaka 741(The Bagdoura Battle), dhidi ya Waislamu wa Kiafrika (Berbers) na Waislamu Wakiarabu. Chanzo kikubwa kikiwa ni Jizya.
Unaonyesha kibanzi kilicho jichoni mwangu, ilhali wewe una Boriti. Unaniita muongo na kunishauri niende nikasome historia, ilhali wewe mwenyewe umeshindwa kuangalia kitu cha msingi kabisa kuhusu historia. Ukweli ni kwamba The Chinese Silk-Road imechangia kwa kiasi kikubwa kuenea kwa Uislamu kule Uchina, lakini unasahau kwamba sehemu kubwa ya hii barabara iko UAJEMI (PERSIA). Sasa hebu tujiulize haya maswali yafuatayo:Uongo mwengine huu maeneo mengi hayo karibia na China wamesilimu kwa ajili ya biashara kasome historia ya indonesia na Nchi jirani na China kama Brunei, Malyasia, Ughuyr na wengineo walikuwaje waisilamu kama sio Wafanyabiashara wa kiisilamu waliokuwa waaminifu compare na wengine na kuwashawishi local.
- Mosi, Uislamu uliingiaje kule Uajemi (Sassanid Persia) ???
- Pili, Unadhani Uislamu ungefika Uchina na India Kirahisi kama Umar asingemshinda Yezdegerd III ?
Hili silipingi kabisa, hata Zheng-He alikuwa ni Muislamu. Japo ambacho nitaendelea kukikataa ni kutaka kusema Uislamu ni AMANI ilhali kumekuwa na madola mengi ya kiislamu ambayo yamekuwa yakipigana vita na kuchinja na waislamu wenzao bila huruma. Kabla hata Salahudin hajaenda kupambana na Makaffir wa Kikristo kutoka Ulaya kule Dameski (Damascus) na Yerusalem (Jerusalem) alianza kupambana na waislamu wenzake walioko ndani ya dola la Kishia la Fatima (The Fatimid Dynasty).Baada ya Salahudin kuwachinja waislamu wenzake ndiyo akaanzisha The Ayyubin Dynasty.China wenyewe mainland kutokana na uaminifu wa waisilamu na kuwa resistance kwenye rushwa wakachukua waisilamu kibao na kuwapa position kubwa, mpaka Great wall of China imejengwa na waisilamu.
Mkuu hapa nakubaliana na wewe, japo unachanganya mambo: Ninachokisema mimi ni kwamba unaweza kuwa huna dini lakini ukaamini uwepo wa MUNGU. Binafsi nafahamu kwamba MUNGU ni zaidi ya DINI ambazo nyingi zimeharibiwa kwa mafundisho na mapokeo ya wanadamu. Tatizo langu mimi liko hapa.Kifupi watu wasiomuamini mungu ni hatari sana nikukumbushe tu karne 1 iliopita wameua watu si chini ya milioni 100, tamaa za dunia ni mbaya sana, sema unachosema hakuna vita inayozidi vita ya kwanza ya dunia, ya pili ya dunia, vita ya korea, etc watu wanauliwa kama sisimizi.
Hivyo ntakuwa sitendi haki endapo ntasema UISLAMU ni MBAYA kwasababu ya matukio machache mabaya yaliyofanywa na wafuasi wa dini kama vita za umwagaji damu mkubwa huko nyuma. Kuna mambo mengi mazuri dini ya Uislamu iliyaleta hapa duniani kipindi cha NEEMA (The Golden Age), machache yakiwa:
- The Modern Scientific Method
- Algebra
- Cubic Equations
- Negative Numbers
- Induction
- Irrational Number
- Astronomical Heliocentric Model
- Distillation
NB: Mkuu Chief-Mkwawa , mimi binafsi nakukubali sana sanaaa. Uwe na usiku mwema....