ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
Mwanamuziki Mkongwe wa kundi la Jackson 5 Tito Jackson (70) ambaye ni Kaka wa Marehemu Michael Jackson, amefariki dunia.
Siku chache kabla ya kifo chake, aliposti ujumbe akiwa nchini Ujerumani ambapo kundi lao lilitembelea eneo la kumbukumbu ya ndugu yao Michael.
Jackson 5 lilianzishwa mwaka 1964 likiwajumuisha Tito, Jackie, Jermaine, Marlon na Michael ambao ni ndugu.
Kundi hilo ambalo lilivuma sana miaka ya 60 na 70, chini ya uongozi wa baba yao marehemu Joe Jackson, limefanikiwa kuuza zaidi ya rekodi milioni 150 na kupokea tuzo mbalimbali.
Onyesho lao la mwisho wakiwa na Marehemu Tito lilikuwa tarehe 10 ya mwezi huu nchini Ujerumani,siku 5 kabla ya kifo chake kilichotokea nchini Marekani.
Ukwaju wa kitambo
0767542202