Kaka yangu ana mke

Kajole

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Posts
1,668
Reaction score
1,643
Habari?,jamani naomba msaada wa kuandika sentensi hii katika wingi: "kaka yangu ana mke"
 
Mambo mengine kuhangaika fupisha mambo ila maana iko palepale,kwani nikisema "kaka zangu wameoa" kuna ubaya gani?
 
Mambo mengine kuhangaika fupisha mambo ila maana iko palepale,kwani nikisema "kaka zangu wameoa" kuna ubaya gani?

Swali ndivyo linavyotaka?
 
Makaka yangu yana mamke
 
Itabidi uongeze kiambishi yaani
KAKA ZANGU WANA WAKE ZAO!
 
makaka yangu wana wake

Wingi wa kaka ni kama, "makaka" si wingi wa kaka.

Huyu muhuni anataka muandike "Kaka zangu wana wake".

Aulize "si wanaume?" Get it? Wana wake, wanawake?
 
Wanafunzi wengi wa Kitanzania wanadhani wanaweza kua na taaluma nzuri ya kiswahili bila kusoma kwa bidii.
Kuzaliwa Tanzania sio tiketi ya mtu kuongea kiswahili fasaha,unatakiwa kusoma kwa bidii na maarifa,Marekani
na Uingereza wapo watu wazembe wa kusoma lugha yao na hawajui lugha ya kiingereza kwa ufasaha.

"KAKA ZANGU WANA WAKE" 100%vema! Ukitaka kujua ukweli fuatilia ngeli za maneno katika sentensi hiyo.

NA SIO SAWA KUSEMA "KAKA ZANGU WANAWAKE"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…