Kaka yangu kaforwadiwa ujumbe huu kwenye simu, afanyeje?

Nime amini wanawake wengi ni wachawi na ukitaka kujua basi ingiza swala la ndugu.
Katika maisha ukitaka kuishi kama fulani utayacomplicate maisha yako sana, na hii wengi tunashindwa hili. Ukiishi kama wewe hata matatizo yako unaweza kuyakabili vizuri. Maisha ya maigizo yanatugharimu sana, unakuwa na tamaa, kila unachopata hakitoshi, mshahara wa mume pia unauona ni haki yako.
 
Ndiyo maana ndoa zinakufa...mke au mmeo ndiyo mtu wa kwanza wa kumweleza kila kitu..kumthamin pindi mnapoaga kwa wazazi wenu pande mbili. Wengine wanakuja baadae wanapokwama. Kama mke au mme sio mtu wako wa kwanza kwa kila kitu ujue ndoa yenu inakasoro.

Umekubali kuhama kwenu ukaishi na mtu ambae mtashirikiana kila kitu katika maisha yenu hadi siku mtakapokufa why asiwe mtu wa muhimu kwako??

Suala la kutokumweka kama mtu muhimu kwako litakuja pale ambapo ataonekana hana nia njema na maisha yako kama unafiki...kutokukuthamin..kukuficha masuala yake..ila kama ni mume na mke bora huyu ndiye mtu wa muhimu kwako.
 
Oyoooo.. Jipangeni kisaikolojia kabisaaaa.. Maana huyo wifi yenu naona kwa mbaaali kashaanza kuleta element za uselfish....
 
Watu mnalaumu upande mmoja mnashindwa ku guess huenda mawifi nao ni mzigo. ..kuna mawifi mke hata hana sauti ndani kwake utafikiri ni house girl. Wao wakija ni kuparagua kila kitu...maneno ya shombo....hivi wewe mdada utajiskiaje pale ambapo unadhati ya kweli na ndoa yako then watu from no where wanakuvurugia mambo??
 
Familia zetu za kiafrika bado tunaishi kwa ujamaa, hatujawa na uwezo wa kujitegemea hundred percent hivo kutegemeana na kusaidiana ni muhimu sana
 
Lazima pia ufikiri kabla ya kushauriana na huyo unayemuita mwili mmoja una jukumu kubwa la kuwalea wazee wako. Je katika hayo mashauliano akikugomea kuwalea wazee wako inavyotakiwa utachukua maamuzi gani kama mwanaume. Kumfuata mkeo au akili yako ya kuwatunza wazee wako.
 
Sawa unalosema. Ila nikuulize kidogo kwa maana hiyo wewe kuwasaidia wazazi wako ni mpaka wakwame. Huna wajibu wa kuwawezesha kabla hawajakwama kabisaaaa.
 
Huyo mwanamke anaekataa kulea wazazi wa mmewe ni mwendawazimu halafu hajielewei unashindwaj labda kuhudumia au kuwapenda wazazi walikuzalia mmeo?
hizo zitakua sio akili Bali ni matope tu kwenye kichwa chake!
 
Sawa unalosema. Ila nikuulize kidogo kwa maana hiyo wewe kuwasaidia wazazi wako ni mpaka wakwame. Huna wajibu wa kuwawezesha kabla hawajakwama kabisaaaa.
Msaada hadi mtu akwame mkuu. Vinginevyo ni zawadi. Na mzazi kusaidiwa sio kigezo cha kumuegesha mke wangu.. wanawake wa siku hizi nao wanamshara hivi utajiskiaje kama kichwa cha familia kila mke wako anapopokea mshahara 1/3 kila mwezi anatuma kwao na hakushirikishi..hayupo karibu na wewe zaidi ya ndugu zake..
 
Mkuu Shefwaa mimi nafikiri ni kila mtu kuheshimu mipaka yake tu. Mke abakie kama mke. Mama abaki kama mama. Baba abakie kama baba. Na wadogo zangu nao wabakie kama wadogo zangu. Kama ni msaada hata maofisini huwa tunatoa..njiani huwa tunatoa..mtu humjui ila unampa msaada.
 
Apo anamaanisha huyo kakako amtimizie yy kwanza mahitaj yake yote ndo aje kwenu ndugu zake...inaelekea kakako anawajali sana nyie....hao ndo wanawake wa dar
 
Inashangaza sana mtu amekutana na kijana wa watu juzi tuu.. Alimkuta na ndugu zake na wazazi wake wako na raha na upendo leo hii inataka ampangie jinsi ya kuwasaidia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…