Kaka zangu jitahidini kuulinda uanaume wenu


Hiyo gender equality ndio inasababisha ndoa nyingi za cku hizi hazidumu, na hizo changes nakubaliana nazo ila mizinga ikizidi haipendezi mimi ni mwanamke lakini mpaka nafikia kuomba ujue nimezidiwa sasa mwanaume unashindwaje kuona aibu? hata wanaume wakipata mwanamke mwenye mizinga sana wanakimbia
 
Acha kuendekeza vya bure kwani wewe mwanamke umepungukiwa na nini ambacho mwanaume anacho mpaka uwe wa kupewa vya bure. Huo ni ujinga na uvivu wa kujitafutia riziki yako mwenyewe. Ndio maana watu kama hao wanaishia kugawa peremende bila hata kupenda. Wanawake wenye mawazo hayo ndio wale wenye kupenda kwenda madsco " wanawake free". Kama wewe ni mwanamke una tabia hiyo nakushauri uachane nayo mara moja la sivyo utageuka kuwa mama huruma ili uweze kupewa ofa.
 
yani hii mada imenifurahisha sana
by then wanawake tunataka usawa kweli ila kaka zetu mmezidisha mario sas ni wengi mno mno, na hizi huwa ni sababu mojawapo za kuvunjika kwa mahusiano mengi mno, eti mkaka anakutegemea kila siku hana pesa yeye tu na out mpak umshauri tutoke at the time anapenda kumbe ni ubahili tu na mkifika anataka ulipe.
mapenzi yanashuka endapo mwanaume anashidwa kutimiza majukumu yake kama wa kiume na ndio maana mimi mmwenye kichwa cha panzi sioni sababu ya kuwa na mwanaume ninayemzidi kipato kwani ni kujitwika gunia la miba through out my life.
 

Oh Maty nikiangalia ujumbe wako unajitahidi kuwa mwanamke mwenye kulinda mapenzi ya asili pia umeangalia zaidi mapenzi kuliko mahusiano ya kijamii kati ya wapenzi (social life).

Lakini kumbuka Tz ya sasa imebadilika na inazidi kubadilika. Mahusiano ya kimapenzi siyo yale ya zamani. Akina mama wanataka usawa ndiyo maana wanajitahidi kufanya mambo ambayo zamani walikuwa hawawezi kuyafanya. Hii ndiyo sababu kubwa hata wanaume wamebadilika. Wanajitahidi kwendana na mtazamo wa wanawake kuwa wanataka usawa. Lakini bahati mbaya wengi wa wanawake hata wanaopigania usawa huu hawaelewi mipaka ya usawa wanaoutaka..Hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuangalia unataka mahusiano ya aina gani katika mapenzi na uweze kuamua ni nani anayekufaa. Vinginevyo Mapenzi ya ASILI yameshaisha sasa hivi. 50%/50% ndiyo inatawala kama ambavyo MLIPIGANIA kule Beijing. Unakumbuka?
 

Soma mada na uielewe vizuri na inaelekea we ni wale wale wapenda kupewa mliojaa humo mitaani bila aibu, mimi kama mimi hata hiyo mizinga huwa cpigi sasa iweje mwanaume uwe na mizinga? We unamuita mtu sehemu halafu unaanza kumwambia alipe bili inahusu?
 

Usawa tuliokua tunaulilia sio wa kumgeuza mwanamke mwanaume na mwanaume awe mwanamke. Tunajidanganya tu usawa usawa na hata kama upo ni baadhi ya maeneo tu. Mbona cjaona mwanaume abebe mimba na kuzaa? likitokea hili basi mi ndio nitakubali kuna usawa kati ya mwanamke na mwanaume tofauti na hapo Mwanaume ndio kichwa na itabaki kuwa hivyo kwangu lakini cjui wengine
 
napenda kusema chochote hapa.
ukweli ni kwamba mtu akikutoa anatakiwa ku-cover expenses zako lakini kwa jinsi ambavyo alipanga, kama alipanga kukununulia sada moja na maji basi unatakiwa kuendelea kujilipia kama unataka kuendelea kuweppo hapo..
swala uanaume haliuhusiani moja kwa moja, hapa tunzungumzia ubinaadamu, mwaume atabakia kuwa mwanaume hata iweje, kazliwa mwanaume ni mwanaume..
 
Hii hoja hapa sio mahala pake!!!!!!!!!!!!!!!.
Hayo ni makubariano baini ya watu, kama yamekukuta malizana nayo ki moyomoyo ili usiaibike na kupunguza hesma yako kwa kujiweka wazi kiasi hichi. POLE
 
Hii hoja hapa sio mahala pake!!!!!!!!!!!!!!!.
Hayo ni makubariano baini ya watu, kama yamekukuta malizana nayo ki moyomoyo ili usiaibike na kupunguza hesma yako kwa kujiweka wazi kiasi hichi. POLE

Pole wewe mwanaume suruali mpiga mizinga limekuchomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa unalo leo kalie lunch
 
We nawe c nilishakuambiaga kipi kilitokea? labda jumamosi hii cjui itakuwaje maana cku ile eliza alificha valuu alikasirika kwa nini kaenda na mimi akaona ka namzibia


aaa...my bad....uchaguzi umechakachua memory card yangu.....hujambo lakini?:tape:
 

The Following User Says Thank You to maty For This Useful Post:

Kaizer (Today)​
 
Hii hoja hapa sio mahala pake!!!!!!!!!!!!!!!.
Hayo ni makubariano baini ya watu, kama yamekukuta malizana nayo ki moyomoyo ili usiaibike na kupunguza hesma yako kwa kujiweka wazi kiasi hichi. POLE

Na kwa taarifa yako mwanamke akikupenda atakuwa anakupa ofa yeye, akikuuliza dear mbona hujanipigia cm unamjibu tu cm haina hela (sio nitumie vocha) ingawa kwa wale mliozoeana haina shida tena unamwambia hebu ninunulie tigo ya elfu mbili kuna mtu nataka niwacliane nae halaf credit imeisha na hapa cwezi toka kwenda nunua vocha unaongea kama mwanaume kichwa na kwa sababu mara nyingi huwa unaonyesha uanaume wako atakutumia hata ya elfu tano wakati umeomba elfu mbili lakini midume mingine anajifanya anamapenzi ya dhati mpole kumbe anakuvutia tu ili akuchune vizr ni aibu jamani mwanaume kulelewa
 
..Hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuangalia unataka mahusiano ya aina gani katika mapenzi na uweze kuamua ni nani anayekufaa....
Nimeipenda hii
 
lakini, kwni mwanaume anachuma mtini hayo mapene?

Ishu c kuchuma, kuchimba wala kuvuna mapene tatizo ni kupigana mizinga inayokera na ni kwa wote wanawake na wanaume, ingawa ikifanywa na mwanaume inashangaza zaidi.
 
Usishangae dada yangu ule usawa ambao akinamama wengi mnaudai ndiyo huo sasa!! Hivi kama ni mpenzi wangu ama mke wangu unafanya kazi nzuri tu nikakuomba uniwekee vocha ya Tshs 5,000/= kwenye simu yangu kuna ubaya gani? Mbona nyie tunawatumia sana vocha alafu hamtupigii mnaishia kututumia ujumbe wa tafadhali nipigie! Naona asifiaye mvua imemnyea yaonekana umekutana na bwana wamizinga,vumilia mtu wangu,hayo ni mambo ya kizungu we have equal rights!
 

Kuna vitu ambavyo haviwez kubadilishwa na huo usawa mnaoutafuta jamani, mimi binafsi mpenzi wangu ninaweza kumtoa out hata kumpa pesa akikwama, lakini unatakiwa ukwame kiume nilikuwa namuonaga baba akiwa hana pesa basi anakuwa mkali kama pilipili hapo mama anajua mhh leo hana kitu so mama anatoa vicenti vyake anapika tunakula na mahitaji mengine. mimi ninachopinga ni mwanaume kujitegeza kabisa kila kitu anampiga mizinga demu wengine hata kazi za maana hawataki kufanya wanataka kuletewa na mwanamke mimi naamini mwanaume kamili huwa anamwambia mke/gf wake akibanwa sana tofauti na sisi wamama ingawa c wote mizinga tu wakati wote mara nipunguzie 300 or 500 nayo wanaume hii wanaichukia vile vile. Mimi bado nina ugomvi na hao wanaume sarawili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…