Hapo umegusa penyewe, wakenya na wazanzibar ni baba mmoja na mama mmoja, wote ni wabaguzi sana, kenya ni wabaguzi wa kabila wakati Zanzibar ni wabaguzi wa eneo la mtu alikozaliwa, Unguja na Pemba.
Wewe ukienda Kenya hutobaguliwa kwa sababu wewe sio miongoni mwa makabila yao, labda kama wewe ni mjaluo wa Tanzania, hapo ukabila utakugusa japo kidogo, lakini utaona jinsi wanavyobaguana kwa misingi ya ukabila, kama hapo ulipo ni wajaluo, nasi mkikuyu hana chake, na utasikia mkikuyu akikuambia ni jinsi gani anavyonyanyasika mahali hapo, vivyo hivyo kwa mjaluo maeneo ya wakikuyu, kila eneo lazima liwe dominated na kabila moja kati ya yale big five, yaani ni shida, sio sehemu ya kuishi hiyo nchi.