IshaLubuva
JF-Expert Member
- Dec 4, 2008
- 250
- 11
Kwenye kipindi cha Bongo Star Search kinachorushwa hewani na Runinga ya ITV, jana wale vijana wawili (Msechu na mwenzake anayewakilisha DSM) ambao mmoja wao ndiyo anatarajiwa kvikwa taji la BSS wa 2009 walijikuta wakiwa kwenye Ukanda wa Hatari (Danger Zone). Kwa mujibu wa Majaji wa Kipindi hicho hiyo ilitokana na watazamaji na washabiki wao kutowatumia ujumbe wa simu wa kutosha. Lakini mimi nilipata mashaka kwa kiasi fulani kwa kuzingatia ufanisi ambao umekuwa ukionyeshwa na vijana hawa hasa Msechu ambaye hata wao Majaji wamakiri kila mara kuwa huwa anawashangaza kila wakati anapotakiwa kupanda jukwaani kwani amekuwa na kawaida ya kuweka ubunifu wa hali ya juu katika nyimbo na hivyo kuweka mvuto wa kumtazama na kumsikiliza. Siamini kama hawa vijana hawakupata kura za kutosha bali wameingizwa kwenye ukanda wa hatari kwa malendo ya kibiashara zaidi na ndo maana naona kama wamewafanyia watazamaji kiini macho kama kile kinachofanywa kenye kamari ya kakarata kekundu/ka pesa. Mnasemaje wadau