Kakobe vs Vyama vya Upinzani?

Watu wengine bana, kama hakuna upinzani kwa nini wewe mwenye akili timamu usianzishe upinzani wa kuaminika? Kukaa tu pembeni na kutegemea wengine wakufanyie kazi.

Unachosema SD ni kweli watu hapa wanasubiri upinzani sijui utoke wapi mbinguni kwani nani alizaliwa na upinzani eti wanasema hakuna upinzani eti Mbowe si Mpinzani eti Slaa si mpinzani eti Chadema si chama cha upinzani mbona wao hawaji na solution au waanzishe chama chao tuwaunge mkono

the Waberoya True & Real Political Party WTRPP au Tumain Silent Movement Party TSMP vingevyo acheni kuwabeza wenzenu if you cant fight join them but if you cant join better keep quit or choose any where to go.
 

- Saafi sana mkuu yaani ndio ukweli wenyewe huu!

Respect.


FMEs!
 

Sasa kama wanatafuna fedha za walipa kodi yani luzuku tusiwabeze??

mbona tunawabeza ccm? aah mambo haya bwana.Ama kwa vile kaluzuku wanakokula ni milioni sitini tu za walipa kodi? teh teh teh
 
Mimi naona upinzani uko safi kabisa na kwa kadri muda unavyoendelea, mapandikizi ya ccm yataondoka na wapinzani wa kweli watasimama jaribio la nyakati

Sawa mkuu
ngoja tusubiri mwezi wa 10, tuone wapinzani kwa kipindi cha miaka 5 wameongeza rate kwa asilimia ngapi.
 
siasa za Tanzania zimekosa majemedari wakwenda mstari wa mbele, inapofikia mahala pakupoteza hata uhuru wako kwa kulala ndani, kule keko, utaona wanasiasa wasivyo na ujasiri, siasa za mageuzi hazitaki watu legelege, wanaoibembeleza serikali.
Upinzani umeshindwa kutumia mianya mingi kupata umaarufu na kujijenga mongoni mwa Watanzania, CCM inapokosea, ndipo wao walitakiwa kurise.
mfano Issue ya watu kufa migodini kule Nyamongo kama nakumbka vyema, ilipasa vyama vya upinzani kutosubiri tume ya wabunge Vibogoyo, ilipasa wao waandamane kupinga yale madhara waliyoyapata watu, waangewaunganisha watu kuwadai fidaia wale jamaa wa Mgodi wa dhahabu, kinyume chake , wako kimya.
janga la umeme ZNZ, eti CUF WANABEMBELEZA MAANDAMANO KWA POLICE, ccm inawatumia POLICE kuzima harakati za kisiasa, ila katika harakati za mageuzi lazima uwe na watu ngangari, kuweza kuongoza wengine hadi kufikia mageuzi ya kweli.
hatuna Stive Biko [RIP] wetu, hatuna Mandela wetu, tunammiss Bibi Titi [RIP]wetu, tunamkosa Didan Kimath[RIP] wa hapa TZ, hatuna mtu ngangari kama Raila Odinga katika siasa za hapa nyumbani.
na kwaababu siasa zetu zimekua bariidi sana, inakua ngumu watu kuwaelewa Wapinzani, wanawaona kama ni CCM B.
 

Kuna sababu gani ya kuanzisha utitiri wa vyama vya upinzani wakati tungeweza kuvipa support hivyo ambavyo vipo tayari?
 

Mkuu kwenye maisha watu wenye akili wanajifanyia assesment wenyewe na kuchagua wawe viongozi maeneo gani nafikiri kina mbowe slaa etc walichagua baada ya kufanya asssesment zao wenyewe kwamba ni viongozi wa kitaifa wa kisiasa? sasa nasema je wanaweza kufanya alichofanya kakobe hawawezi kwasababu hawana wafuasi wanaowaamini ..then waji assses wenyewe kwamba ni failure

Mimi nimeji assses mwenyewe nikachagua kuwa kiongozi wa biashara zangu kazi ya yangu ni kuhakikisha my business inaendelea kubaki, profitable na nina uwezo wa kulipa wafanyakazi wangu..period! huko ndiko nilikochagua na hapo viongozi wenzangu (wafanyakazi) wananiamini na wananifuata siku nikishindwa kuwashawishi kwa hoja naachia ngazi hicho ndicho yardstick

Kina slaa na mbowe wamechagua siasa wakiwa hawawezi for all those years kudai mambo ya msingi kama katiba, tume huru, etc na kuwaelimisha wananchi nikiwemo mimi niwafuata naweza kusema hawano uwezo..period!
 

Mambo ya Imani hayo mkuu ni tofauti,wewe hukuona Kakobe na t-shirts zao zinasema serikali imwogope Mungu?Kwa hiyo tayari wanakuwa wameshaunganishwa na fact wanayoamini kwamba wanapigania kazi ya Mungu.
Hakuna level ambayo mwanasiasa anaweza kuwaunganisha wananchi kwa namna hiyo,the only time ni pale waananchi walipoambiwa JK ni chaguo la Mungu na kwahivyo waliamini kumchagua JK ni kazi ya Mungu...Very few times kuna scenarios kama hizo,lakini kwa ujumla ni lazima Imani iwepo kwa lolote lile linalopiganiwa being it kwa kupitia dini ama siasa.....Wananchi ama wafuasi hao ni lazima waamini kabisa kwamba kuufutilia ufisadi mbali katiba mpya ni suluhisho....Tatizo tulilonalo sisi watanzania ni kujikita zaidi kwenye issue zinazotugawanya zaidi ya zile zinazotuunganisha,ni lazima tuamini kwamba maslahi ya Taifa ni namba moja,hapo maslahi ya Taifa yanaweza kuwa imani ya kuwaunganisha watanzania bila kujali dini....Tukianzia hapo,then we'll talk.
 

Mandela alikuwa na dini gani ndugu?

Raila ni dini gani?
 

Nikijiunga nao niwe zezeta? mbona wanafukuzana hovyo, unafikiri mimi nitapona huko? yaani nisiulize Mbowe kaipa Chadema sh. ngapi na mpaka sasa ahivi amelipwa sh. ngapi,. kama wewe usiyeijua Chadema kiundani uko hivi je wenye chama?

Kubali kuwa havina sura ya kitaifa

Nimekuonya mara nyingi sentensi unazozisema ni kukosa hoja, leo wakisemwa Polisi, basi niwe polisi, au haujawahi kukosoa watendaji serikalini?

nikikomkosoa JK, basi niwe rais!, nikisema manesi hospitali ya Temeke wana roho Mbaya, kesho huyooo nikavae nguo nyeupe niwe nesi

jibu hoja!
 

If you dig deep inside you will find out that all these is due to beliefs

naamini CUF na ndio maana member wa cuf, naamini ukristo na ndio maana ni mkristo

sijaona mtu anayejiita mwanachama wa chama fulani halafu haamini katika hicho chama!!
 

Hoja hii kweli umeijibu inavyotakiwa

Kwa kuongeza tu kila mtu ana amepewa talanta tofauti. Na mara nyingi kutoka na malezi yetu waafrika ni vigumu kuitambuwa talanta hiyo, lakini unapoenda kupractisi ktk maeneo fulani unatambuwa kabisa hapo si mahala pako ama unagundua hapo ni mahala pako.

Mfano umeenda shule imeshindikana paka ukaamuwa kununua cheti huu ni ufisadi.
Ama umefanya siasa ,mafanikio hamna ila uppo pale tu kwa sababu kuna kitu kidogo huu ni ufisadi.Kwa namna nyingine anakosa uaminifu mdogo anatambua kabisa hawezi kitu ila kwa vile si mwaminifu anang'ang'ania, na tumeambiwa bayana.
Mtu asiye mwaminifu kwa vitu vidogo hakika hawezi kuwa mwaminifu kwa vitu vikubwa.
 
If you dig deep inside you will find out that all these is due to beliefs

naamini CUF na ndio maana member wa cuf, naamini ukristo na ndio maana ni mkristo

sijaona mtu anayejiita mwanachama wa chama fulani halafu haamini katika hicho chama!!

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuamini na kuwa mwanachama/mwanadini

Kuna watu ni wakristo/waislamu lakini hawana imani..msingi ya imani ni pamoja na kufuata kwa vitendo vyako vyote

Huko Chadema/CUF kuna members tu wenye malengo tofauti wengine kwa ajili ya vyeo wengine kwa ajili ya status

Kinachotakiwa ni kiongozi hasa wa kuwapa imani, na yeye mwenyewe awe na imani kwa vitendo wamfuate..wapo hakuna kwasababu hawajui wanachokiamini na vipi wakipate
 

kwa wakristo tunasema kuna ngano na magugu!

kwa hiyo naona wapinzani wengi ni magugu, tu kuna vyama ukivigusa utasikia anayekilinda chama ni mmoja au wawili!
 
kwa wakristo tunasema kuna ngano na magugu!

kwa hiyo naona wapinzani wengi ni magugu, tu kuna vyama ukivigusa utasikia anayekilinda chama ni mmoja au wawili!

Teh teh teh

Kwamba upinzani ni sawa na mbegu zilizoanguka ktk miamba, na ccm ni mbegu zilizoanguka ktk miba. teh teh the
 
Unapowalinganisha Waalimu ni lazima pia uwalinganishe na wanafunzi wao. Huwezi kusema Mwalimu fulani hodari kuliko mwenzake, eti kwa kuwa wanafunzi wake wengi wamefaulu. Je, wanafunzi waliofeli kule kwa mwenzake wakoje? Kuna wanafunzi wasioweza kufundishika hata wakipewa mwalimu gani. Pamoja nayo, huna budi pia kuyatafakari mazingira ya kufundishia na kufundishiwa.

Vivyo hivyo, kwa viongozi. Kakobe ana makanisa mangapi na waumini wangapi? Na viongozi hao wanaolaumiwa wana mashina mangapi na watu wangapi wanaowaogoza? Kisha, tusiache kutambua kinachoongozwa. Yaani siasa na imani ya dini. Wanasema, huwezi kulinganisha machungwa na malimau.

Jaribu kuleta majadiliano ya kidini hapa, uone jinsi yatakavyokwenda tofauti na majidiliano ya kisiasa. Kusema ni rahisi zaidi kuliko kutenda.
 
Kwa upande mwingine ni vyema pia kutambua kuwa watu wanaohamasishwa kwa imani ya kidini wana tofauti na wanaohamasishwa kwa misingi ya kisiasa. Waumini wa kanisa la Kakobe kama ilivyo kwa waumini wengi wa dini zingine huwa wako tayari kufia imani yao wakati kwenye mambo ya siasa pekee hakuna nguvu ya aina hiyo na kuaminiana ni kudogo sana. Hata mababu zetu wa enzi za vita ya majimaji ni imani katika nguvu ya miujiza ndiyo iliyowahamasisha kujitoa mhanga.
 

Soma post #50
 
Hakuna ubishi kwamba udhaifu wa vyama vya upinzani dhidi ya CCM uko wazi. Lakini mimi ningependa pia tuangalie juhudi za dhahiri za baadhi ya wapinzani ambazo zimetoa changamoto si kwa CCM tu bali hata kwetu wa-Tanzania wengine. Sitaki kurudia kutaja yaliyo wazi hasa kuhusu matendo ya ufisadi uliolazimisha Serikali (hatimaye) kukiri na kudai kuchukua hatua.

HATA KAMA BADO JUHUDI HIZO ZIMESHINDWA KUBADILI STATUS QUO BASI SIDHANI KAMA NI VYEMA KUWABEZA HAO WACHACHE WALIOAMUA KUBEBA BANGO LA UPINZANI KWA DHATI (These people are not a monolithic block, by the way).

Kama ni udhaifu wa upinzani, mtazamo wangu mimi, tatizo ni sisi wa-Tanzania wote. Inakuwaje katikati ya utendaji mbovu ikiwa ni pamoja na unyanyasaji unaoendelezwa katika mfumo wa ukiritimba wa chama kimoja (virtually) tunashindwa kujitoa kuimarisha uongozi na kuunga mkono chama/vyama mbadala (upinzani imara) na tunaendelea kutoa zawadi ya ushindi wa kishindo kwa chama kimoja (CCM) kwa ama kukipigia kura nyingi au kutoshiriki uchaguzi kwa tusioridhika na status quo.

Kujaribu kulinganisha upinzani (siasa) na Kakobe (dini) ni kwenda nje ya mantiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…