Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 1,809
- 1,692
MKOA MPYA NA MAKAO MAKUU MAPYA NYAKANAZI:
Anaandika Msakila M Kabende - Economist
KWA WAHESHIMIWA:-
(i). Aloyce Kamamba - Mbunge wa Jimbo la Buyungu
(ii). Ezra John Chiwelesa - Mbunge wa Jimbo la Biharamulo
(iii). Ndaisaba G. Luhoro - Mbunge wa Jimbo la Ngara
(iv). Fidel Chiza Nderego - Mwenyekiti wa H/W Kakonko
(v). Lushahu - Mwenyekiti wa H/W Biharamulo
(vi). Wilberd J Bambara - Mwenyekiti wa H/W Ngara.
YAH: PINGAMIZI LA MAKAO MAKUU YA MKOA MPYA WA CHATO KUWA CHATO
Kwanza, niwapongeze sana kwa kuendelea kutumikia wananchi wenu ktk majimbo yenu na halmashauri zenu kwa uadilifu na uaminifu.
Pili, niwaombe muunganishe nguvu zenu kukataa, kupinga na kutokuwa sehemu ya vikao vitakavyobariki ktk kuweka MAKAO makuu ya mkoa mpya wa Chato kuwa Chato. Hii ni kutokana na ukweli kwamba sisi wananchi tunaosogezewa huduma tutakuwa mbali na makao hayo makuu. Iwapo Serikali yetu ina dhamira njema i.e kuchochea maendeleo yetu, kupunguza adha kwa wananchi na ufanisi wa utoaji huduma kwa jamii basi tunapendekeza MAKAO makuu ya mkoa mpya yawekwe NYAKANAZI kwa kuwa:-
(a). Kakonko - Nyakanazi 45Kms
(b). Ngara - Nyakanazi 79Kms
(c). Biharamulo - Nyakanazi 45Kms
(d). Chato - Nyakanazi 113Km.
Sasa kwa ujumla makao makuu kuyaweka njia panda ya Nyakanazi itakuwa na tija kwa wilaya zetu zote kwa kuwa ipo katikati ya maeneo yote yanayounda mkoa mpya.
Nimewaandikia hili ili muunganishe nguvu za hoja hii ktk vikao vyote vya kisheria kama Regional Consultative Committee (RCC); District Consultative Committee (DCC); Regional Road Boards (RRB) na vikao vingine vingi.
Wananchi wa maeneo yote yanayounda mkoa mpya wa Chato tunamuunga mkono, na kumkumbuka Hayati Dkt John Pombe Magufuli lkn kumbukumbu zetu hatutaki zigeuke kero kwetu kwa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kijamii na kiuchumi.
Naamini kwa umoja wetu Mungu atatuvusha katika kipindi hiki cha kupata mkoa mpya na makao mapya ya mkoa.
Mungu awabariki sana.
Msakila M Kabende
= Mgombea ubunge kura za maoni CCM jimbo la Buyungu 2010, 2015, 2018, na 2020.
= Mgombea Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa mwaka 2017.