Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Na. M. M. Mwanakijiji
Tulipokuwa watoto wadogo tulijifunza kawimbo ambako sikuwahi kukutafakari maana yake. Ni kawimbo ambako labda watoto wengi wa Kitanzania katika sehemu mbalimbali wamekaimba na labda bado wanakaimba miongo mingi baadaye. Ni kawimbo ambako unaweza kukapotezea lakini ukitafakari falsafa kali ya haki na utawala bora iliyofichika ndani yake unaweza kuelewa kwanini leo nimekakumbuka.
Kakuu ka Mama Rhoda
Kanakula mpunga wangu
Nikitaka kukafukuza
Mama Rhoda ananikataza!!
Nimekatafakari haka kawimbo kakanirudisha kwa Rais Samia. Kwamba, inawezekana tumeanza kuwa na fikra za kukaogopa kakuku haka?
1. Mpunga ni wangu kwanini kuku wa mama Rhoda aule? Ni wazi kuwa kuna suala la matumizi mabaya ya madaraka au ukuu fulani. Yaani, mama Rhoda yuko tayari kuku wake ale mahali popote na hakuna wa kumuuliza. Ni kweli mama Rhoda alishindwa kukapa kakuku kake chakula hadi kaje kula cha kwetu? Yaani, watu waliojiriwa na serikali yetu na wanapewa mafao makubwa tu kwanini bado wanakula zaidi ya urefu wa kamba zao hadi waje kula vya wengine?
2. Mifumo yetu ya kufukuza hivi vikuku inawezekana ni mibaya sana kwani inamtegemea sana Mama Rhoda aaume mwenyewe. Yaani, hatuwezi kuvifukuza hivi vibadhirifu badala yake tunasubiri mama Rhoda avitengue mwenyewe sisi tupige makofi lakini wenyewe hatuwezi kuvifukuza?
3. Ni wazi kuwa hakuna anayependa kulisha kakuku ka kajirani. Hata kama kakuku ni kazuri kana rangi nzuri lakini kaende kula kwao!
Ni lazima kama taifa tuanze kuvikataa na kuvifukuzia hivi vikukuu hata kama Mama Rhoda anatutakataza. Ripoti za CAG kama ilivyokuwa huko nyuma zimezidi kutuonesha kuwa Bila Mama Rhoda kuvifukuzia mbali au kuvichinjilia mbali hivi vikuku haviachi kula mpunga wa taifa bila kuulizwa na sisi tutabakia kulalamika kwa kushindwa kuvifukuza.
Au tukaache kale kakichoka katabakisha?
Sipendi tena sitaki Kakuku ka Mama Rhoda kawe kama Ka Mama Samia!