Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MUDDYB MWANAHARAKATI MWANDISHI KIJANA ALIYE NA KALAMU INAYOSEMA
Kawaida ya kalamu kama itasikika basi mlio wake ni nibu inakwaruza karatasi.
Lakini si kalamu ya Muddyb.
Hii "b" ambayo haikutenganishwa na jina la kwanza nimeelezwa kuwa hiyo "b" inasimama kwa"blast."
Blast neno la Kiingereza lenye maana ya kulipua.
Kalamu ya Muddyb inazungumza.
Ukianza sentensi ya kwanza kitabu hukitui hadi umefika mwisho.
Kalamu ya Muddyb inazungumza na msomaji kwa lugha anayoielewa msomaji ikamshika mkono na kumfikisha katika mitaa hajapata kutia mguu hata siku moja.
Muddyb amejaaliwa kipaji si cha kawaida.
Muddyb katika umri huu mdogo mno wa ujana ameshaandika vitabu 10.
Ameandika vitabu 10 vya riwaya zinazoeleza ukweli wa maisha ambayo kila mtu anayajua kuwa haya ndiyo maisha yetu ambayo ni watu wachache sana wale ambao wamejaaliwa hawakuyapitia.
Mchango wa unga wa sembe wa vijana wa Vingunguti waliomaliza darasa la saba miaka mingi nyuma.
Wanachangizana hela usongwe ugali na kauzu.
Abdallah keshakabidhiwa senti aende gengeni akanunue nyanya, pilipili, ndimu kwa ajili ya kachumbari.
Kabla hajanyanyua mguu kutoka Rashid anamuonya, "Oya kwa hisani yako usituletee pilipili mboga."
Pilipili mboga ni ile si kali haiwashi.
Shabani anaongezea, "Hii biriani ya leo mwanangu ina viwango, dagaa wa Kigoma."
Nje mpita njia kasikia maneno yale akarusha maneno, 'Hadi kiama dona haliwi biriani.''
''Toa uchuro wako wewe.''
Akajibiwa kutoka ndani.
"Nenda kawange Manzese."
Hii ndiyo staili moja kati ya nyingi ya uandishi wa Muddyb.
Msomaji makini lazima utajiuliza, "Huyu Muddy anatoa ujumbe gani kwa jamii?"