MKAKA WA CHUO
Member
- Aug 13, 2022
- 11
- 6
Sisi Kama WATANZANIA au wanadamu Kila mmoja anashughuli ambayo anaifanya ili kumuingizia kipato Cha Kila siku ambacho kitamsaidia kukidhi mahitaji yake binafsi na familia yake kwa ujumla. Na Kama siyo hivyo basi ipo shughuli ambayo Kila mmoja wetu anaamini akishiriki kikamilifu katika shughuli hiyo anaweza kupata mafanikio kiasi Fulani ambacho kitamsaidia yeye kuendesha harakati zake na zile za familiya yake PAMOJA na kukidhi mahitaji yake yeye binafsi na mahitaji ya familia yake.
Katika mazingira yetu ya TANZANIA watu tofauti tofauti wanaweza kuwa na Imani juu ya shughuli tofautitofauti Kama vile kilimo, uvuvi, ufugaji, ufundi, usafirishaji au udereva, Siasa,elimu na biashara. Hivyo basi Kila mtu hujiingiza katika sehemu ile ambayo yeye binafsi ana amini atapata mafanikio iwe kwa haraka au kwa kuchelewa lakini Kila mmoja wetu anategemea mafanikio katika ile shughuli yake anayoifanya Kila siku, kiuhalisia ni jambo zuri Sana kwa Kila mtanzania mwenye uzima wa Afya kuwa ni MTU mchakarikaji ile kuhakikisha anajipatia kipato chake binafsi lakini pia kuzisaidia familia zao.
Miongoni mwa changamoto kubwa ambayo huwakumba wengi katika WATANZANIA wanapojishughulisha na shughuli mbalimbali Kama vile kilimo na biashara ni kuto kufikia malengo Yao waliojipangia au waliyoyakusudia Kama kikundi, familia au MTU mmoja mmoja. Hili ni suala linaloumiza WATANZANIA wengi katika maisha yetu ya Kila siku.
Changamoto hii inaweza kuwa inasababishwa na sababu mbalimbali lakini sababu kuu inayopelekea wengi katika sisi vijana wakitanzania na WATANZANIA walio wengi ni kuto kuisoma au kuistadi shughuli ambayo MTU au kikundi kinahitaji kuifanya shughuli hiyo ili iwe Kama chanzo Cha kuwaingizia kipato.
Kwamfano wakina mama wanaocheza michezo ya kuchangishana pesa Kama vile VIKOBA na KIBATI wengi katika hawa Huwa wanashindwa kufanikisha malengo ya shughuli zao kwasababu mtu anaweza kukopa pesa kwenye KIKOBA alafu anaenda kuanzisha bustani ya nyanya na shamba la vitunguu wakati huo anafungua mashamba hayo hajui kabisa kuhusiana na gharama zinazotakiwa kuendesha shughuli za mashamba hayo mawili, anachojua yeye ni alime nyanya na vitunguu Kisha vikue avune akimaliza akuuze mazao apate pesa ya kurudisha alikokopa na faida abaki nayo mwenyewe.
Watu wa Aina Kama hii wapo wengi Sana katika maeneo yetu tunayoishi, unaweza kumuona MTU ameanza kujenga NYUMBA yake ya tofari za kuchoma, ikifika katikati ndiyo ana iacha hapo kutokana na kuishiwa na pesa kabisa, baada ya kipindi kirefu kupita kutokana na Mvua zinazonyesha Kuna uwezekano mkumbwa wa jengo lile kuanguka au kubomoka, na hapo ndio kunatimia ile kauli ya ni Bora uchelewe kutoka lakini ufike safari yako kuliko kutoka mapema kabisa halafu ukaishia njiani.
Jambo ambalo linasikitisha zaidi ni kwamba wengi katika sisi WATANZANIA tunapokutwa na changamoto hii tunaishia kusema tumerogwa au tumekoperwa na vitu vingine Kama hivyo vinavyohusiana na Imani potofu kabisa za kishirikina, lakini unapomuuliza huyo mlalamikaji kwamba daftari lako ambalo ulikuwa ukiandika mchakato mzima wa shughuli yako likowapi, wengi wao hubakia kusema Mimi Huwa siandiki Mambo yangu kwenye madaftari, mimi huwa Nafanya tu. Mara nyingine unaweza kujiuliza Sasa Kama Huwa hawaandiki michakato ya shughuli zao watajuaje gharama zinazohitajika kuendesha shughuli hizo, hapo ndio unaweza kupata jawabu la kwanini Huwa wanashindwa kufikia malengo waliyojiwekea.
Kama mtanzania au Kama kijana kwanza ni lazima ufanye uchaguzi sahihi wa shughuli yakufanya. Miongoni mwa vigezo vya kuzingatia wakati wakuchagua shughuli ya kuifanya ili ikuingizie kipato ni kuipenda shughuli hiyo, hakikisha unaipenda iyo kazi, Kama ni kilimo, kufundisha, ufugaji au biashara hakikisha unapenda unachokichagua na siyo uchague shughuli kwa SABABU ya watu Fulani, kufanya hivyo kutapelekea kushindwa kufanya au kuendesha shughuli hiyo.
Jambo jingine ni kuchagua shughuli ambayo unaiweza kuifanya na kuisimamia shughuli hiyo, kwa mfano kilimo, inatakiwa ujue namna ya kulima kilimo bora na Uwe na uwezo wa kulima kilimo hicho. Tunapozungumzia uwezo wa kulima kilimo Bora ninamaanisha uwezo wa kifedha na Mambo mengine yanayohitajika, ni muhimu uhakikishe unafahamu gharama zinazohitajika kuendesha shughuli ambayo utaichagua.
Tija au faida itakayopatikana kutokana na shughuli utakayoifanya, kwasababu ili uifanye shughuli hiyo ni muhimu kujua matumizi yatakayo fanyika na mapato yanayo tarajiwa kupatikana. Baada ya kujua Mambo hayo ya msingi Sasa unaweza kuchagua shughuli ya kufanya kulingana na vigezo hivyo, vilevile baada ya kuanza kuendesha hiyo shughuli Kuna Mambo mbalimbali ya msingi ya kuzingatia, lakini jambo kubwa ambalo wajasiliamali wengi wanalipuuzia ni utunzaji wa kumbukumbu.
Kumbukumbu za shughuli husika ni jambo la muhimu sana kuzingatiwa katika kuimarisha ubora na uhai wa shughuli yako. Kumbukumbu hizi zinaweza kuhusisha matumizi ya kilasiku Kama vile gharama za wafanyakazi, madawa, chakula, usafiri na vitu vingine kulingana na shughuli ambayo MTU anajishughulisha nayo.
Katika mazingira ya kawaida kumbukumbu hizi zinaweza kutunzwa kwa Njia ya maandishi katika madaftari, njia hii ni rahisi zaidi kwa WATANZANIA walio wengi, lakini pia kumbukumbu za shughuli yako unaweza kuzihifadhi katika kompyuta na vifaa vingine vya kieletroniki.
Jambo lakuzingatia ni kufanya mahesabu kabla yakuanzisha shughuli yako, kufanya mahesabu mara kwa mara wakati unaendesha shughuli yako na kuzipitia kumbukumbu za biashara au shughuli yako ili kuona muelekeo hasa wa biashara yako, jambo hili litakuhakikishia usalama wa shughuli yako na litakusaidia kukurahisishia kufikia malengo yako kwa urahisi. Hapo chini nimeweka picha inayo onesha kanuni na misingi ya biashara. NDUGU ZANGU WATANZANIA, MALI BILA DAFTARI HUISHA BILA HABARI.
BY: MKAKA WA CHUO.

Upvote
1