Kalamu ya Ally Kamwe : Mkutano wa Mo Dewji

Kalamu ya Ally Kamwe : Mkutano wa Mo Dewji

Mimi Yanga napenda aendelee azidi kuwakoroga. Azidi kuwaita majina watu wa simu za Techno za elfu 70
Kwani Simu ya TEKNO ya Elfu Sabini haikamati mawasiliano ?
Kipindi hiki Elfu Sabini ni pesa ndefu sana, inatosha hata kulipia Mahari na ukapata Jiko.
Mimi TEKNO yangu ni ya Elfu Ishirini na tano, na niliipata kwa kulipa kidogokidogo kwa mhindi hadi nilipoikomboa.
Sasa hivi natanua na Tekno yangu na ndiyo niliyoitumia kuandika hii meseji.
Wewe unatumia Simu gani ?
Na ni ya Bei gani ?
Au Umepigwa hapo Kalia Koo ?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Simu ya TEKNO ya Elfu Sabini haikamati mawasiliano ?
Kipindi hiki Elfu Sabini ni pesa ndefu sana, inatosha hata kulipia Mahari na ukapata Jiko.
Mimi TEKNO yangu ni ya Elfu Ishirini na tano, na niliipata kwa kulipa kidogokidogo kwa mhindi hadi nilipoikomboa.
Sasa hivi natanua na Tekno yangu na ndiyo niliyoitumia kuandika hii meseji.
Wewe unatumia Simu gani ?
Na ni ya Bei gani ?
Au Umepigwa hapo Kalia Koo ?


Sent using Jamii Forums mobile app
Soma vizuri. Hayo maswali kuhusu elfu 70 muulizeni mtu wenu Manara. Alikuwa dalali tapeli wa magari Kariakoo. Sasa Simba imemjenga hadi anawaita wapumbavu. Maana hela anayo kwa sasa.
 
Mikia siyo Baba na mama yake ,Baba yake ni Yanga sasa mtu kuwaambia ukweli imekuwa nongwa?
 
Tatizo Haji Manara ni Mswahili sana.
Uso wa Mo Dewji katikati ya ujanja na ujinga wa Haji Manara

Kalamu ya Ally Kamwe

Kwa Jicho lingine. Kwa mtazamo mwingine, Press ya Simba Sc leo imetuonyesha kilichojifisha katikati ya ujanja na ujinga wa Haji Manara.

Ni mkutano uliobeba majibu ya viongozi juu ya sin'tofahamu iliyotokeza hivi karibuni kati ya Haji Manara na mashabiki wa Simba.

Mbele ya waandishi wa habari, Simba SC leo imesemewa na watu wawili wakubwa ndani ya klabu hiyo. Mwekezaji Mohammed Dewji na Mwenyekiti Swedi Nkwabi. Wawili tu.

Haji Manara hakushiriki kwa lolote. Si kwa kuonekana kwenye mkutano wala kupost taarifa ya mkutano huu kwenye mitandao ya kijamii. Na si kawaida yake.

Hii Tafsiri yake ni nini? Kuna kosa Haji Manara alilifanya hivi karibuni. Japo alitumia nguvu kubwa kujisafisha/ kulikanusha, lakini ukweli ni kuwa kosa lile liliacha madhara makubwa sana katika kazi yake.

Haji aligombana na mashabiki wa Simba. Watu waliowahi kumuamini kama Kibwetele alivyoaminika na wafuasi wake.

Ni mashabiki hao aliowaita "mashabiki maandazi" ndio waliibeba na kuiamini ile hoja yake kuwa Simba ingeweza kuifunga Barcelona na PSG.

Wakajazana uwanjani kwa furaha. Wakanunua jezi. Wakaimba na kucheza kila Simba ilipokuwa ikicheza hata mchana wa Jua kali.

Kukosana na watu hawa kwa kigezo 'eti ametukaniwa mzazi mitandaoni', lilikuwa ni miongoni mwa makosa kubwa kuwahi kufanywa na Haji katika maisha yake. Pengine analijutia wakati huu.

Mpira si mchezo wa kiungwana kiasi. Umekusanya mashabiki tofauti tofauti wenye hisia zisizofanana. Wakati mwingine tunasema soka ni mchezo wa wendawazimu.

Ndio. Ngoja nikupe mfano wa uwendawazimu kwenye soka.

Kwa mfano wewe ni shabiki wa Chelsea, baba ako ni shabiki wa liverpool... Mkiwa mnaangalia mechi yenu pamoja, ukakerwa na jambo na ukajikuta umetukana (ashakum sio matusi) "Hawa Liver wote wasenge tu"...

Kimaana hapa unakua umemjumlisha na baba yako. Lakini kuna mtu alishawahi kuadhiwa kwa kosa hili na mzazi wake? Pengine utastaajabu na baba ako akakujibu hivyo hivyo, mkacheka, mpira ukaisha na maisha yakaendelea.

Haji alitakiwa kuelewe vitu vidogo na vikubwa na maana yake huku kwenye mpira. Kwa vyovyote, majibishano yale kati yake na mashabiki hayakutakiwa.

Madhara yake ni kama haya tuliyoyaona leo. Imebidi Mo Dewji na Swedi Nkwabi wajitokeze mbele ya waandishi wafanye kazi yake.

Tena amewatesa kweli kweli mabosi wake!

Wamejikuta wakilazimika kueleza na mipango mingi ya siri mbele ya waandishi ili wafikie lengo lao la kutangaza viingilio vya mechi.

Yes. Ni MO DEWJI aliyetangaza kuwa mechi itachezwa saa 10 na viingilio ni Tsh 2000. Kiwango kidogo kabisa kulinganisha na thamani na ubora wa mechi yenyewe.

Ilibidi iwe hivyo kwa sababu Haji Manara haaminiki na kundi kubwa la watu kama zamani. Ameshawaga wapenzi wa Simba. Hata angetangaza kiingilio ni buku bado watu wangeacha kujadili mechi na kuanza kumshughulikia yeye.

Siamini kama huu ndio mwisho wake, ila naamini hili ni FUNZO KUBWA analoweza kujifunza kama kichwa chake kitapenda kujifunza.

"Mafuta ya taa robo tu yanaweza kuharibu Maji pipa zima."

Sent using Jamii Forums mobile app
Anafikiri anajibizana na mashabiki wa Simba wa Buguruni na Tandika kumbe wengine wanatoka Masaki.
 
Huenda wewe ndio Manara mwenyewe ila tumekuchoka mkuu. Huwezi kuanza kutusema na vitecno vyetu.
Manara endelea kuwashika, na hiyo ndiyo kazi yako.
Kazi yako ni kusema
" Simba itashinda "
Na sio
" Simba itashindwa "
Hata kama itatakiwa kucheza na Barcelona.
Hii ndiyo kazi yako.

TEKNO ya Elfu Sabini inafaa kwa matumizi ya Binadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
W
 
Manara endelea kukomaa na hao vyura! Wewe ndo saizi yao! Sasahivi mtani wa jadi wa yanga ni Manara na sio simba tena.
 
Soma vizuri. Hayo maswali kuhusu elfu 70 muulizeni mtu wenu Manara. Alikuwa dalali tapeli wa magari Kariakoo. Sasa Simba imemjenga hadi anawaita wapumbavu. Maana hela anayo kwa sasa.
Hakuna mahali Manara kawaita washabiki wa Simba sc kuwa ni wapumbavu.
Kama ni umaarufu hata wewe ni mtu maarufu pia
Jiulize Umaarufu wako umeupata wapi ?
Ulipozaliwa ulikuwa maarufu tayari ?
Kama hukuwa maarufu wakati wa utotoni kama manara, basi nyote mmeupata umaarudu mahali fulani.
Kama ni hivyo msidharauliane basi, kwani wote mmeupata umaarufu ukubwani.
Bila mahali hakuna umaarufu.
Wewe mahali pako palipokupa umaarufu ni wapi ?
Hadi unajulikana namna hii ....!





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom