Msamiati
R I P
- Mar 6, 2011
- 1,063
- 700
May I want to Be a Doctor?
Ngoja leo nifichue siri ... Elimu ya Tanzania haijafa, Imeuwawa.
Najua siri iliyofanya mtoto wa mbwa awe kibaka, siri ambayo imekosa mtu jasiri wa kuiweka hadharani ili mwenye uamuzi wa mwisho aweze kuchukuwa uamuzi wa lazima, uamuzi pekee wa kumkomboa mtoto wa kizazi chake na kizazi kijacho dhidi ya utando wa kiza, Utando uliokosa hata mwangaza hafifu sawa na miwani ya bati tuliyo valishwa wanyonge ili migongo yetu iendelee kutumika kama ngazi ya kuwapeleka juu mamwinyi ambao ni watu wenye werevu wa kuona mbali kwa kutumia kurunzi na kuendelea kutukanyaga.
Haitakuwa rahisi hata siku moja kuleta usawa kwa madai, lakini itawezekana tukilazimisha usawa kwa maamuzi. Maamuzi kwamba tumechoka kutumika na sasa hatutatumika tena, maamuzi ya kwamba tumechoka kupangiwa maisha na sasa tutapanga wenyewe, tuamue kuwa tumedhalilishwa sana na sasa tuheshimike. Tuamue mwisho wamanyanyaso, tutengeneze hatma yetu kwa fikra zetu wenyewe, tusisaidiwe kuwaza, tusisaidiwe kutenda wala tusidai usahihi tena, bali tufanye wenyewe kwa usahihi. Tuchague mabadiliko na tubadilike dakika hii.
Nataka kusema siri kubwa iliyojificha nyuma ya elimu yetu, sambamba na mipango baradhuli ya kuhakikisha kawaida enaendelea kuwa kama sheria. Mipango ya makusudi kabisa ya kuhakikisha mjinga haerevuki ili mjanja asikae matatani na hatimae uhuru, haki na usawa katika elimu viendelee kuwa ndoto kwenye kizazi cha watoto wa mmbwa ndani ya taifa hili la waota ndoto.
Nataka niseme ili sasa tuamue kusimamisha mipango yote ya migomo endelevu, dhuluma endelevu, uzalishaji wa makusudi wa Degree zinazotembelea magongo, Biashara haramu kwenye elimu, rushwa, wizi, unyonyaji na kila aina ya uharamia. Nitasema kwa vielelezo na vithibitisho katika kila kipengele. Najua haitakuwa na nguvu kufanya hivyo kwa kutumia kalamu ya mkaa lakini kwa kuwa mabadiliko ni mimi na wewe basi hii itakuwa hatua ya kwanza endapo tu, wewe uliemalizia mstari huu wa mwisho unaguswa na sanaa zinazofanywa kwenye elimu, sanaa ambazo zinaathiri wanyonge ambao ni masikini wa kipato na kuwadharirisha kwa kuiaminisha jamii kuwa wao ni tabaka mbumbumbu na wasiokuwa na uwezo wowote wa kiakiri ili yule aliye juu tuendelee kumngoja chini.
Niseme nisiseme?