Kalamu ya mkaa - Elimu ya Tanzania Imeuwawa

Kalamu ya mkaa - Elimu ya Tanzania Imeuwawa

Msamiati

R I P
Joined
Mar 6, 2011
Posts
1,063
Reaction score
700
May I want to Be a Doctor?


Ngoja leo nifichue siri ... Elimu ya Tanzania haijafa, Imeuwawa.

Najua siri iliyofanya mtoto wa mbwa awe kibaka, siri ambayo imekosa mtu jasiri wa kuiweka hadharani ili mwenye uamuzi wa mwisho aweze kuchukuwa uamuzi wa lazima, uamuzi pekee wa kumkomboa mtoto wa kizazi chake na kizazi kijacho dhidi ya utando wa kiza, Utando uliokosa hata mwangaza hafifu sawa na miwani ya bati tuliyo valishwa wanyonge ili migongo yetu iendelee kutumika kama ngazi ya kuwapeleka juu mamwinyi ambao ni watu wenye werevu wa kuona mbali kwa kutumia kurunzi na kuendelea kutukanyaga.

Haitakuwa rahisi hata siku moja kuleta usawa kwa madai, lakini itawezekana tukilazimisha usawa kwa maamuzi. Maamuzi kwamba tumechoka kutumika na sasa hatutatumika tena, maamuzi ya kwamba tumechoka kupangiwa maisha na sasa tutapanga wenyewe, tuamue kuwa tumedhalilishwa sana na sasa tuheshimike. Tuamue mwisho wamanyanyaso, tutengeneze hatma yetu kwa fikra zetu wenyewe, tusisaidiwe kuwaza, tusisaidiwe kutenda wala tusidai usahihi tena, bali tufanye wenyewe kwa usahihi. Tuchague mabadiliko na tubadilike dakika hii.

Nataka kusema siri kubwa iliyojificha nyuma ya elimu yetu, sambamba na mipango baradhuli ya kuhakikisha kawaida enaendelea kuwa kama sheria. Mipango ya makusudi kabisa ya kuhakikisha mjinga haerevuki ili mjanja asikae matatani na hatimae uhuru, haki na usawa katika elimu viendelee kuwa ndoto kwenye kizazi cha watoto wa mmbwa ndani ya taifa hili la waota ndoto.

Nataka niseme ili sasa tuamue kusimamisha mipango yote ya migomo endelevu, dhuluma endelevu, uzalishaji wa makusudi wa Degree zinazotembelea magongo, Biashara haramu kwenye elimu, rushwa, wizi, unyonyaji na kila aina ya uharamia. Nitasema kwa vielelezo na vithibitisho katika kila kipengele. Najua haitakuwa na nguvu kufanya hivyo kwa kutumia kalamu ya mkaa lakini kwa kuwa mabadiliko ni mimi na wewe basi hii itakuwa hatua ya kwanza endapo tu, wewe uliemalizia mstari huu wa mwisho unaguswa na sanaa zinazofanywa kwenye elimu, sanaa ambazo zinaathiri wanyonge ambao ni masikini wa kipato na kuwadharirisha kwa kuiaminisha jamii kuwa wao ni tabaka mbumbumbu na wasiokuwa na uwezo wowote wa kiakiri ili yule aliye juu tuendelee kumngoja chini.

Niseme nisiseme?
 

endapo tu, wewe uliemalizia mstari huu wa mwisho unaguswa na sanaa zinazofanywa kwenye elimu, sanaa ambazo zinaathiri wanyonge ambao ni masikini wa kipato na kuwadharirisha kwa kuiaminisha jamii kuwa wao ni tabaka mbumbumbu na wasiokuwa na uwezo wowote wa kiakiri ili yule aliye juu tuendelee kumngoja chini.

Kuna moja kati ya haya matatu:

(a) Wewe sio mtanzania (mkimbizi) kwahiyo harakati zozote tunazozifanya kwa ajili ya kujikomboa sisi na vizazi vyetu HAZIKUHUSU
(b)Wewe Ni Mtanzania Bendera yafata upepo (Mbumbumbu) kila unachoambiwa Tawire! Others think on your behalf POLE
(c)Wewe Unanufaika na mfumo uliopo Hufikirii kwa manufaa ya taifa, tumbo lako ni muhimu kuliko kizazi chako POLE SANA

Lakini kama bado wewe bado ni mtoto wa shule basi fikiria mara mbili mbili kwasababu hamjui nini kinaendelea huku mtaani.
 
maaajabu mtoto wa kidato cha nne kusoma diploma tena ya uwalimu
kwaninu wasifute form 6 tu dah hiii elimu innafanywa kama kitasa unanonga tu
 
Ndugu zangu, watanzaniawenzangu tunaoteseka kwa kupumbazwa na mabaradhuri wachachewaliodhamiria kabisa kuhakikisha hatuelimiki, na hata jitihada zetuza kujikwamua ili tupate ahueni wameapa kuzifanya kitega uchumi chakunenepeshea matumbo yao, naomba musome waraka huu wa kalamu ya mkaakwa umakini mkubwa.

Nimeshafanya uchunguzina kubaini mbinu zote wanazozitumia kuendeleza tabaka la matajiri nawenye uwezo huku wakitukandamiza bila sisi wenyewe kujua, miminitaweka wazi moja badala ya jingine, lakini tuanzie hapa.

Hapa hatuitaji Digreekuelewa mbinu zao za PHD. Elimu ya tia maji tia maji inatosha kabisakupambanua yafatayo:

Hawa watu wamesoma sanandugu zangu, wanajua kila kitu, Lakini mipango yao haikubalianikabisa hata na elimu ya kidato.

Hivi wenye dhamana yakusimamia elimu yetu tena ambao ni wamiliki wa sifa za kimataifa, hawajui maana ya elimu au ni sehemu ya mipango yao kujitoa ufahamu nakuiendesha taasisi ya elimu kama chama cha kidini ! ?

Yaani ni kheri wabadilike mapema sana kwani sasa tumesha shtukia nini wanafanya,hebu na wewe mwenzangu soma jifunze maana ya elimu...

NenoELIMU au Educationkwamaneo ya kingereza asili yake ni myumbuliko wa maneno tofautitofauti ya Karatini ambayo ni: educare,educere,educatum, na educatus.
Manenohaya kwa muunganiko wake yanamaanisha kuza, endeleza au toa njekilichokuwa ndani, funza.

Ukisomamara tatu tatu na kupambanua vizuri asili hiyo ya neno elimu,utagundua Tanzania na nchi nyingi za kiafrica hatuna elimu, na hiindio sababu tumeendelea kuwa masikini wa kutupa na watutunaohitaji kuongozwa katika kila jambo.

tunaongozwakwenye technolojia, tunaongozwa kwenye siasa, tunaongozwa kwenyeImani, tunaongozwa kwenye sanaa, tunaongozwa kwenye kila jambo.Tatizo ni kwamba hatuna elimu, na kutokuwa na elimu kwa Waafrika nimipango ya kimasirahi kwa baadhi ya watu. Sitalizungumzia hilikimataifa, ila nitajenga hoja yangu kitaifa zaidi kwa lengo lakuwaonesha vijana wenzangu jinsi elimu yetu inavyo haribiwa na watu wachache tuliowapa dhamana kwa manufaa yao na wale walio nyuma yao.

Leonitaishia kwa kufafanua tafsiri ya elimu ili tuone kama hikikinachofanyika hapa Tanzania ni elimu au madrassa.

Kutokanana asili ya neno elimu na maana yake, mfumo wa elimu unatakiwa uwe nakazi ya kuendeleza au kumwagia mbolea au kukuza kile ambacho mtuanacho ndani yake, ili aweze kuleta manufaa kwenye jamii. Huu ndiomsingi mkuu wa elimu na mataifa yaliyoendelea yanawekea mkazo msingihuu.

Elimumaana yake ni kudadavua kile kilichopo ndani ya ubongo wa mtukumfanya akifanyie kazi, kukiendeleza.

Sisi tuliofanywa mambumbumbuhuwa hatuaminiki wala hatuaminiani, mimi nawahamasisha kwa nguvu zotekufanya mabadiliko na sio kuyadai mabadiliko.

Na kama kwenye tafsiri hii unashindwakuniamini mimi, basi muamini Dr. ZakirHusain – "Educationis the process of the individual mind, getting to its full possibledevelopment."

Kama humuamini Dr Zakir basi muamini mwanaphilosofi mkubwa kabisa duniani Rousseau- "Educationisthe child's development from within."

KamaRousseau haaminiki basi mwamini Pestalozzi –"Educationis natural, harmonious and progressive development of man's innatepowers."

Elimu maana yake ni kuendeleza kile kitu alichonacho mtu ndani yake ili kuleta mavumbuzi mbali mbali na urahisi wamaisha katika jamii.

Vitabu ambavyo vimeandikwa na mitaara inayotumikaduniani ni kwa lengo la kuwaelekeza watu wajue nini kimesha fanyikana kimefanyikaje ili wasirudie kutumia muda mrefu kwenye tafiti. Hiipia inasaidia kuwafanya wanaofata elimu waendeleze pale walipoishiawenzao wasianze na moja.

Wenye dhamana wanajifanya hawalijui jambo hili.Wameiaminisha jamii kuwa elimu ni kukalili maandiko yaliyowekwakwenye vitabu, wametufanya tuamini kuwa mwisho wa vitabu ndio ukingowa elimu.

Tanzania hatuna Elimu, elimu ambayo mtu anatakiwa kukaririni elimu ya madrasa, elimu yetu imefanywa kuwa kama elimu ya bibliaambayo hutakiwi kuongeza wala kupunguza.

Wanachokifanya ni kinyume kabisa na matakwa yaelimu, Badala ya kuweka mkazo kwenye kuendeleza kile alicho nacho mtukutoka ndani yake, wao wanafanya jitihada zote kuua alicho nacho mtuna kulazimisha kumpakia vitu vingine kutoka nje, kutoka kwenyemavitabu na maandiko, tunapakiwa yaliyomo na yasiyokuwamo baada yahapo tunafundishwa mwisho wa yote ni Digree, hapo wanamaanisha umeshameza vyote unavyotakiwa kumeza sasa nenda mtaani kasafe salama.

Umemezeshwa makolokolo kibao kwa zaidi ya miaka15, umekosa kabisa nafasi ya kuelimika, vitu tunavyomezeshwa haviwezikutatua tatizo lolote kwenye jamii, wanafanya hivyo ili tuendeleekuwa wateja wa bidhaa na huduma zao.

Nilazima tuamue kusimama kuuondoa huu ubaradhuri, kwania ya kuleta maendeleo ya taifa letu.

Degree zetu haziwezi kutuleteanishati, haziwezi kutuondolea tatizo la mafoleni barabarani, haziwezikuleta uvumbuzi wa matatizo ya makazi, wakulima na wafugaji, haziwezikushona neti, hata kuboresha miundo mbinu.


K%@#nina !


DIGREE ZA TANZANIA ZOTE KAMA VYETI VYA KIPAIMARA


tutaendelea...

 
System has been rotten problem is how to remove it!!
 
Back
Top Bottom