Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
HII NI HUJUMA NA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA WANANCHI.
Hebu tutazame kiasi gani cha fedha zitafujwa kupitia hii Kamati kwa kitu ambacho jibu liko wazi,tozo ni "Poll Tax," kwa hiyo wananchi hawapaswi kutozwa,vitafutwe vyanzo vingine vya mapato,na vipo..
1) Hao wajumbe 200 kila mmoja atalipwa ‘allowance – per diem) ya shilingi 250,000/= kila siku. (200 ×250,000 = 50,000,000).
2) Shilingi milioni hamsini zitakuwa zinatumika kila siku ya uhai wa hiyo Kamati.
3) Hii Kamati itadumu kwa muhula wa miezi minne. Tuzidishe hiyo milioni hamsini mara siku 120, (50,000,000 × 120 = 6,000,000,000/=). Hapo hatujaweka gharama za hivyo vitendea kazi: magari na Laptops. Kuharibu kiasi hiki cha fedha kuchunguza suala ambalo lilitakiwa kufutwa bila uchunguzi ni uhujumu uchumi.
4) Ni dhahiri kuwa Mh.Mwigulu amepwaya kwenye wadhifa wake. Dalili zote zinaonyesha kuwa kazi imemshinda. Upeo huu wa wananchi kuchukia uamuzi wa Serikali yao katika suala hili la tozo haujapata kutokea tangu uhuru.Mheshimiwa Mwigulu aidha apumzishwe au ajipumzishe kwa kujiuzulu.
5) Ni kweli kuwa huo uamuzi ulipitia Bungeni, lakini Rais hawezi kuwatumbua wabunge wote waliopitisha bili iliyozaa hii tozo. Lakini Kiongozi wa juu muhusika kuwajibika au kuwajibishwa ni sawa.
6) Katika muda wa miaka mitano, hayupo Rais, tangu uhuru, ambaye alileta huduma na kujenga miradi mikubwa kwa nchi yetu kama alivyofanya Hayati Magufuli. Lakini alitekeleza hayo bila tozo yoyote.
7) Aidha, hayati Mwalimu Julius Nyerere alituachia mashirika ya umma hai 450, alitoa bure huduma za afya na elimu pamoja na ruzuku kwa wakulima. Pamoja na hayo, alisaidia kimatendo ukombozi wa bara la Afrika kuliko Rais mwingine yoyote; na upeo wa utumiaji wa natural wa raslimali zetu wakati ule ulikuwa mdogo kuliko leo.
Na yeye pia hakutumia tozo. Huu umuhimu wa tozo leo, unaletwa na nini?
8) Kadhalika, hii tozo ni sawa kabisa na “Poll tax’ ya zama za kikoloni; ambayo Mwalimu Nyerere aliifuta mwaka 1968 kwa sababu ilikuwa ni ya kisheria lakini si ya haki.
9) Tujikumbushe kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo Margaret Thatcher, alilazimishwa na Chama chake Cha Conservative ajiuzulu,baada ya kuleta tozo au “Poll tax”; tozo ambayo ingalikifanya Chama cha Conservative kisishinde uchaguzi uliokuwa unakuja. Aliyechukuwa nafasi yake John Major, alifutilia mbali hiyo tozo kabla ya uchaguzi.
USHAURI.
Hii tozo ifutwe bila kuundwa Kamati ya aina yoyote. Tozo hii inajenga chuki kali kati ya wananchi na Viongozi wa nchi yetu. Haileti maana Taifa kutumia Shilingi bilioni sita, kuchunguza kama wananchi waendelee kunyanyaswa na hii tozo ambayo si ya haki.
Tanzania tusikubali kuvuruga amani yetu ili kuhifadhi uso au nyuso za watu wachache waliobuni tozo kandamizi, tozo isiyo ya haki.