yani jamaa alipoandika barua ya kuomba msamaha Clouds kwa kosa walilomfanyia wao,kila mtu alimdharau...hadi Hashim dogo mpaka kesho anamcheka uyu jamaa..unajua kwa wasio mjua Pina wanamchukulia bonge moja la kamanda kumbe mweupe tu,utoto mwingi.
anatumia nguvu nyingi sana kuimba upuuzi.
nadhani kabla ya kuingiza vocal huwa anakunywa vladimir na makushabu ya kutosha.
Sijaelewa, huyu jamaa muimba kwaya au hiphop? Ila mistari uliyoitaja ina 'ujumbe mzito'.huwa nasikiliza nyimbo za huyu jamaa, kuna ule wa umoja ni nguvu humo ndani anasema ''siwezi kula nguruwe, siwezi kuabudu sanamu...''. wimbo wake mwingine mpya wa hivi karibuni anasema ''wanaabudu msalaba...'' .inafahamika yeye ni Muislamu sasa sijui maneno haya kwa nini anayapenda sana?
Nackia sahivi ana harakati against freemasons
Kalapina a.k.a Nabii koko...ni mdini kweli..kama alivyo Hashim dogo..na si Pina Tu kikosi chote wana itikadi hiyoo ya kidini
ila tatizo la Pina ni kujifanya yeye Frontline kila kitu
Ishu ya yeye na clouds jamaa alihaidiwa kipindi cha Tv cha Hip hop..kipindi kile anafanya Hip hop bila madawa
Kwanini Pina hayuko na Vinega?
Pina Anadai wakati yeye anafanya harakati zake za kudai haki ..eti wasanii( VINEGA)..hawakumpa sapoti...kasahau kuwa alikuwa anawapiga baadhi ya wasanii...
Nitarudi....
Hana ukali wowote me namfananisha na Mr. Blue tu.
Pamoja na kalapina kutofanikiwa sana kimuziki lakini alikuwa anaheshimika kutokana na misimamo yake against wanyonyaji wa sanaa.Amejivua nguo kujisalimisha kwa maadui wake wa longtime! Hao Clouds hawatamsaidia lolote na huu mwaka hautaisha hajarudi kule kule! Kalapina mwepesi tu hana lolote!kumbe dini inamzuia Pina kula nguruwe tu ,kijiti inamruhusu.....
huyo ndo Nabii koko beach
hadi gwalufandu??kalapina bonge la mdini,naona siku izi ameamua kujiweka wazi.eti sasa ivi anafanya harakati za kupambana na ukatoliki!
Msikilize tungo zake kwenye ngoma yake mpya "vatican ndio wanaotuchagulia viongozi"..kuna mstari mwingine anasema "sili nguruwe wala siabudu sanamu" sikiliza kwa makini 'mstari wa mbele' na 'umoja ni nguvu' utanisoma..
Ana misimamo ya kitoto sana ndio maana anaongoza kundi ambalo halipo'kikosi cha mizinga' kwenye kundi kabaki ye na mkewe tu mau,machizi wote wamemkimbia hadi mwanae msemakweri...
Watu wamekuwa wakimlilia Hashim Dogo arudi kwn game ila hataki, sijui lini atakubali atubariki hata na album moja tu. He is the king of Hip hop in TZ. Watoto wa siku hizi hawamjui. Sad!
Dogo Mwanaharamu,
Kalamu inamwaga Damu,
Nakuacha mweupe kama Mkorogo,
Chata ka' wagogo,
Wabongo acheni nyodo,
Wote mnakula Hongo,
Na hivi hii ni Serikali,
Sera ya mbali,
Au sera ya zamani kwa mbali,
Tunapokwenda pana zali,
Vichaa wangu walume, wanyaka hiyo hali,
Tujifunze tujitume,
Mwisho wa mwezi tuvune,
Kama hujipendi njoo nichune,
Kila mjuba sasa kivyake.
Na hivi nina dhiki,
Nikipata karatasi,
Wino hutoka kwa kasi,
Kwa haya nina wasiwasi,
Kiu ya jicho,
Ulichonacho ndicho ulicho,
Tokea '77 wabongo wamefunga mkanda,
(Kudadeki)
|
Sijui kwanin haya mashairi ya Hashim hayabanduki kichwani mpaka leo hii!!!