Kalenda ya mtawala Caesar na Papa Gregory

Kalenda ya mtawala Caesar na Papa Gregory

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
15727100_1405458002829941_2711283956142102584_n.jpg



Mwanzoni kabisa, dunia ilikuwa ikitumia kalenda ya mtawala wa Kiroma aliyeitwa Julius Caesar. Kalenda hiyo ilianzishwa mwaka 46 Kabla ya Kristo. Kalenda hiyo ilikuwa na siku 465 na masaa 6.

Kalenda hiyo ilikuwa na makosa machache machache kwani hata sikukuu ya Pasaka ilikuwa mbele kabisa na si mwezi wa nne kama ilivyokuwa sasa hivi. Lengo kubwa la Papa Gregory XIII kuanzisha kalenda yake mwaka 1582 ambayo ndiyo inatumika mpaka sasa hivi ni kutatua matatizo madogomadogo yaliyokuwemo katika kalenda ya Caesar.

Baada ya Aloysus Lilius kutengeneza kalenda hii na kumpa Papa Gregory, haikuwa ikitumika kwanza, ilikuwa ikiwekwa vizuri na miaka mitano baadaye ndipo ilipoanza kutumika. Katika mwaka 1582, siku kumi ziliondolewa katika kalenda hiyo, yaani October 5 mpaka 14, kwa hiyo ikawa ikitoka October 4, kesho inakuwa October 15.

Baada ya kalenda ya Gregory kutolewa, hakukuwa na mataifa mengi yaliyoipenda, hivyo ilikuwa ikitumika katika nchi ya Italia, Spain na Ureno, sehemu nyingine bado walikuwa wakitumia ile ya Caesar ikiwemo Uingereza ila ilipofika mwaka 1752 ndipo Uingereza nayo ikaanza kutumia kalenda hiyo.

Tangu nchi ya Saudi Arabia ilipoanzishwa mwaka 1932 haitumii kalenda ya Gregory, Kalenda yao inaitwa Hijri (Kalenda ya Kiislamu) lakini kwenye kuwalipa wafanyakazi mbalimbali, hutumia kalenda hii ya Gregory.

Kalenda hiyo ya Kiislamu ina siku 354, pungufu ya siku 11 kutoka katika kalenda ya Gregory.

WATU WALILALAMIKA SANA

Wakati Gregory anaanzisha kalenda yake, alizikata siku 11 kutoka katika kalenda ya Caesar. Jambo hilo lilileta malalamiko makubwa kwa watu waliokuwepo kipindi hicho kwamba je, wao watajua wamezaliwa siku gani na wakati kalenda haiwaonyeshi.

Hilo halikujibiwa, Vatican ikakaa kimya kwani walijua waliokuwa wakilalamika, kuna siku wangekufa na maisha kwenda sawa katika matumizi hayo ya kalenda hiyo. Ndivyo ilivyokuwa, kalenda haikubadilishwa, watu walipokufa, maisha yaliendelea kwa kutumia kalenda iliyokatwa siku mpaka leo hii.

KWA GREGORY, MWAKA MFUPI NA MREFU HUTOKEA SANA

Katika kalenda tunayoitumia leo hii, mara kwa mara mwaka
unakuwa na siku 365 au 366 lakini katika kalenda ya Caesar, mwaka wenye siku 366 ulikuwa ukitokea kwa kila baada ya miaka minne.

Imeandaliwa na Nyemo Chilongani
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848] Na sisi huku kibongo bongo, kabla ya ujio wa wageni(wakoloni, wamisionary, na wapelelezi) inamaana hatukuwa na calendar yetu, na kama ilikuwepo ilikuwa ikisomekaje, na kama haikuwepo tulikuwa tunaishi vp pasipo kufaham majira???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku tulitumia majira ya mvua, baridi, jua kali, joto kali, njaa, mafuriko nk
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848] Na sisi huku kibongo bongo, kabla ya ujio wa wageni(wakoloni, wamisionary, na wapelelezi) inamaana hatukuwa na calendar yetu, na kama ilikuwepo ilikuwa ikisomekaje, na kama haikuwepo tulikuwa tunaishi vp pasipo kufaham majira???

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watapiga magitaa, bendi za muziki makanisani lakini ukweli wanaufahamu kuwa Catholic ndiye babu wa maendeleo mambo mengi ya kuindesha dunia. Walokole hawawezi kwenda kuendesha misa pale Saudia au UAE au Iran, China hata Syria lakini Papa anafika na anapewa heshima zote
Hiyo ndio Katoliki, usiipende bado itaathiri japo kipengele kimoja cha maisha yako, hata ujifungie ndani itakuathiri ndani kwako.


#Nasadiki#

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watapiga magitaa, bendi za muziki makanisani lakini ukweli wanaufahamu kuwa Catholic ndiye babu wa maendeleo mambo mengi ya kuindesha dunia. Walokole hawawezi kwenda kuendesha misa pale Saudia au UAE au Iran, China hata Syria lakini Papa anafika na anapewa heshima zote

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa. Mwambie Mwingira aende China au Saudia kama hata chinjwa[emoji2] [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Calendar ya Chief Apostle D. Mutalemwa
 
Back
Top Bottom