Kalonzo aambiwa aachane na RAO

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,957
Wakuu aliyekuwa mgombea mwenza wa Urais nchini Kenya kupitia muungano wa NASA ameshauriwa aachane na Raila Odinga na badala yake ajiunge na chama Tawala cha Jubilee.
Kwa mujibu wa Wazee wa Ukambani pamoja na washauri wengine wamedai kuwa kwa sasa mashirikiano hayo hayana faida yoyote kwa jamii hiyo badala yake yameiletea jamii hiyo hasara kwa hivyo nibora ajiondoe kwenye ushirika huo.
Mhesh Kalonzo pia amepinga mpango wa kufanya maandamano nchi nzima ulioitishwa na RAO kwa kusema una lengo lakuleta ghasia na vurugu nchini humo na ni kitendo cha kuhujumu Uchumi. Aidha amekosoa uamuzi wa RAO kujitoa kwenye uchaguzi wa marudio kuwa ni wa kibinafsi na haukufanywa kwa kuzingatia maslahi mapana ya Wakenya. Ameongeza kuwa njia sahihi ya kupata Uongozi ni kupitia Uchaguzi na sivinginevyo.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.
Karibuni
 


RAO ndo nani/nini?
 
Hii ni moja ya habari mbovu kabisa kuandikwa hapa JF!!
 
Unaandika kwa haraka sana...source ya habari yako ni nini
 
Hilo Gazeti la Mwananchi, pamoja na The Citizen na The East African kamwe hayaandiki habari mbaya za Jubilee na hasa Kenya na ni tofauti sana yanavyoandika za Tanzania na Serikali.
Hawajawahi kusumbuka kufafanua in details kile NASA wanachopinga bali ni washapu sana kuandika taarifa zao mbaya kama ilivyo kwa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…