Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amekataa ombi la Naibu Rais Kithure Kindiki la kumuomba na kumshawishi ajiunga na utawala wa Rais Ruto
Haya yanajiri baada ya DP Kindiki kujaribu kumkaribisha Kalonzo katika ziara yake eneo la Ukambani, akidai kuwa bosi huyo wa Wiper anaweza kutoa ushauri mzuri kutokana na uongozi wake unaoheshimika.
Kalonzo hata hivyo amekataa kauli ya Kindiki siku ya Jumapili, akidai kuwa hawezi kujiunga na "serikali ya umwagaji damu" na hawezi kufanya kazi na uongozi usio na msimamo.
Kiongozi huyo wa Wiper alishikilia kuwa atasalia na mizizi ya "Muungano wa Upinzani" na ataendelea kufanya kazi na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kung'oa utawala unaotawala.

"Nitashirikiana na mwanamume mkweli anayeitwa Gachagua" alisema wakati wa ibada ya kanisa huko Ngong"